nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
January 28 2012
Na Grace Ndossa
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesema itatoa uamuzi wa pingamizi lililowasilishwa na Kampuni ya Dowans la kuitaka mahakama hiyo isiwape Tanesco kibali cha kukataa rufaa Febuari 16 mwaka huu .
Amri hiyo ilitolewa mahakamani hapo jana na Jaji Fauz Twalib ambapo alieleza kuwa hawawezi kusikiliza kesi hiyo leo kwani Wakili wa Kampuni ya Dowans Bw. Kennedy Fungamtama ameshawasilisha pingamizi.
Pingamizi hilo la Dowans l;inahusu kupinga Tanesco wasipewe kibali kwani hukumu iliyotolewa hawawezi kukata rufaa kutokana na makubaliano waliyokubaliana kwenye mkataba.
Jaji Twaib alidai kuwa hataweza kusikiliza kesi hiyo hadi hapo watakaposikiliza pingamizi lilowasilishwa na Kampuni Dowans.
Awali baada ya hukumu kutolewa na mahakam kuu Tanesco iliwasilisha maombi yao kuomba kibali cha kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Jaji Mushi ya kuitaka tanesco kusajili tuzo ya fidia ya sh bilioni 94 ya kampuni ya Dowans mahakama hiyo kwa njia ya maandishi
Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na wakili wa Dowans,Bw. Kennedy Fungamtama kwa ajili ya kuiomba mahakama hiyo iiweze kuisajili tuzo waliyoipewa Novemba 15 mwaka juzi na Mahakama ya Kimataifa na Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara(ICC)