Mahakama kuu imetoa hati kukamatwa Nabii na Mtume Josephati Mwingira

hata kama ni nabii wa uongo ila mimi naungana naye kwenye kauli yake. Wabunge wetu wengi wanalala makaburini hasa kikikaribia kipindi cha uchaguzi, wanavaa mapete ambayo yana picha za ajabu tena zenye maandishi ya kiarabu yaani ukiliona lazima nywele zisisimke
 
hivi kumbe haya mapete ya akina Malim@ na mkuu wa kaya ni ya kishirikina?
 
Hata kama ni bazazi, alichosema ni haki yake kukisema. And so far, kila nikiangalia vidole vya hao wanaojiita viongozi wetu sikosi kuona pete ambazo zimetajwa! Kwa nini nisiamini kuwa nchi inaongozwa na walala makaburini? No wonder mambo yako hivi yalivyo

Hufikirii chochote kuhusu pete wanazovaa maharusi?Na kifimbo cha Nyerere je mbona husemi chochote mkuu.Mwenge aliouanzisha Mtakatifu Mtarajiwa Nyerere huukumbuki.Maaskofu huvaa pete ambazo waumini huzibusu.Tuseme wakristu huongozwa na viongozi walalao makaburini kama kigezo ni kuvaa pete?TATIZO LETU NI KWAMBA HATUFIKIRI WENYEWE.TUNAFIKIRISHWA.
 
Hivi Mtume qualification yake mojawapo ni KUSHUSHIWA KITABU?
utume wake amepewa na nani...? kitabu gani ameshushiwa...? aache kudanganya watu kwa tamaa ya tumbo. huko anakoenda sasa (kuwatukana viongozi wa serikali) ajiandae kufirisika.
 
I have the right to remain silent. By the way, he claimed to have prayed to his 'GOD' to end Mwl. JK's life because the bible says 'all witches must die'

I have the right to remain silent, and so do you. Do not quote me, plz!
 
hajaijua serikali ukishaigusa kwa mabaya wkt ww ni mfanyabiashara
watakunyanganya kila kitu atabaki mtupu.
kwanza aandae fidia kubwa kulipa kiwanda alichobomaoa atauza hadi kanisa tv na bank yake kufidia
shetani kweli mbaya ameshamkamata pabaya huyu bwana anaejikweza.
 
Nabii na Mtume Joseph Mwingira amesema, yeye ni Mtume wa mitume wote duniani na hawezi kuogopa na polisi wanao mtafuta.

Amesema serikali ya Tz inaongozwa na watu wanalala makaburi na kuchanjwa chale na waganga wa kienyeji.

Amesema viongoz wakuu akiwemo rais wanavaa pete za wachawi na hirizi hivyo hawana uwezo wa kupambana naye.

Akiongea kwenye ibada alisema kama wananisaka kwa nini wasijekunikamata hapa kanisani? Nitapambana mpaka kieleweke, Nipotayari kufa. Amewataka waum huyo mtume mwingira ni mtume wa uongo,aache huo upuuzi wake.na ninafíkili kuwa na yeye ni mmoja wa hao wanao lala makaburini mwanga mkubwa huyo
 
Nabii na Mtume Joseph Mwingira amesema, yeye ni Mtume wa mitume wote duniani na hawezi kuogopa na polisi wanao mtafuta.

Amesema serikali ya Tz inaongozwa na watu wanalala makaburi na kuchanjwa chale na waganga wa kienyeji.

Amesema viongoz wakuu akiwemo rais wanavaa pete za wachawi na hirizi hivyo hawana uwezo wa kupambana naye.

Akiongea kwenye ibada alisema kama wananisaka kwa nini wasijekunikamata hapa kanisani? Nitapambana mpaka kieleweke, Nipotayari kufa. Amewataka waumini wake wasitishwe na viogozi wa serikali wanaolala Makaburini.

duh, inatupasa kuwa makini sana na Haya magazeti. Maana wanaandika habari wauze...
bahati nzuri jana nilikuwepo ibadani Efatha Mwenge...alisema anaheshimu serikali na anamuogopa Mungu peke yake. Haogopi kitu kingine chochote (sio serikali, mahakama,polisi wala mtu). na wala hakusema yuko tayari kufa kwani hakuna anayeweza kufanya hivyo isipokuwa yeye aliye juu(MUNGU)... na ndivyo ilivyo...
 
Inaonyesha wewe si muumini wa Kakobe wala Mwingira pia huweze kuwa Mkatoliki ukashauli Wapentecosti .Huna sifa za kumkosoa Kakobe.Mahubiri yake ni ya kweli na Yanalenga kuwasaidia watu

Mwamakula, nafurahi unaanza kukunjua makucha yako polepole kutuonyesha wewe ni nani. Tumeambiwa sana @Zijaribuni kila roho" Roho wa Mungu hapingani na Mungu. Ukiona hayo yanatokea, basi aliye shambani abaki shambani na aliye darini asishuke, maana hata Ibilisi alikuwa mkuu wa malaika Mbinguni mwenye kuaminiwa sana. Alipoanza kujijengea kiburi hakupewa nafasi ya kujirekebisha hata ajapo tena Mwana wa Adam kwa mara ya pili.

Lakini kweli mimi si wa Paulo wala wa Petro, ila nazungumzia habari za jiwe kuu la pembeni ambalo waashi walilikataa lakini kumbe ndilo linaloufanya msingi wa ujenzi kuwa imara zaidi. Ikifka mwisho wa siku wewe baki kwa Kakobe au Mwingira, lakini wale waliompokea ajaye kuhukumu dunia watanyakuliwa pamoja naye wala sio kupitia ukatoliki au upentekoste. Hizo ni dini za duniani tu, ambazo wakati mwingine ni chanzo cha vipato kwa walio wachache. Dini iliyo nzuri ni ile ambayo yawezekana hutapenda kuisikia ikitajwa, maana sio wote waendao makanisani wanakwenda kwa malengo yanayofanana. Ndio maana wengine hulala usingizi tangia kuanza kwa ibada hadi wakati wa kutoka nje, kisha huwasalimia wawapendao pamoja na kuwashika mikono wachungaji na mashehe na viongozi wa dini wawaone kwamba walihudhuria. Heri yao wanaojua kwa hakika wanamwamini nani na wakawa na msimamo wasiyumbishwe na mtu. Paulo alisema hata yeye alikuwa anapigana vita ili asije akawapeleka wengine Mbinguni na yeye akabaki. Rose Muhando anasema usiwe kama mpiga debe anayewaambia watu panda twende, kisha yeye anabaki palepale.

Simwamini Kakobe wala Mwingira wala binadamu yeyote awaye yote kwa habari ya kwenda mbinguni. Lakini naungana na yeyote anayeamini kama mimi ambaye tuinaweza kuongea lugha moja ya rohoni na kutiana moyo, maana kama binadamu, wote tumeoza pia, kutiana moyo ni agizo tangu enzi za manabii kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo.
 
Manabii enzi zile walikuwa wakiteuliwa na Mungu miujiza ilifanywa pasipo maandalizi roho wa Mungu aliwashukia watu wakaanguka na kujitupa huko na kunena kwa lugha cha kushangaza sasa hv miujiza inafanyiwa maandalizi mfano kuna siku ndugu yangu alienda kusali akiwa ana kidonda mguuni mhubiri ajiitaye nabii akanguruma kuwa kaoteshwa na Mungu kuwa kuna mtu atamtibu kidonda ndugu yangu alishtuka sana akanyanyuka na kuanza kuelekea mbele kwa mshangao wahudumu walimrukia na kumrudisha na kumuambia siyo wewe na mara anainuka mtu ambaye alikuwa anakidonda na kwenda mbele mtume akaanza kumuombea huku nyuma yake kuna mhudumu amejiandaa kumdaka na ghafla akampuliza na akaanguka chini akadakwa aliponyanyuliwa wakaambiwa kapona watu wakabaki kustaajabu na kusifu.Hii tabia hii sijui itakoma lini full sanaa!!!ee Mungu tuepushe na manabii na mitume wa uwongo.
 
Failed to display your comment, please change your ID or call Administrators for further help...............:lock1:
 
@kubinika... sasa wewe unamwamini huyo mwenye imani sawa na wewe je ni imani ipi hiyo. akina kakobe wanatumia biblia kumfahamu yesu kwenda mbinguni. sasa wewe ili tukusaidie tuambie. . na umesema humuamini binadamu yeyote vip tena unamtaja paulo. watumishi wa mungu wapime kwa mahubiri na matendo yao. ndio uje uzungumze.
 
Amesema serikali ya Tz inaongozwa na watu wanalala makaburi na kuchanjwa chale na waganga wa kienyeji.

Amesema viongoz wakuu akiwemo rais wanavaa pete za wachawi na hirizi hivyo hawana uwezo wa kupambana naye.

.

"Uhuru bila mipaka ni Fujo na Demokrasia bila uwajibikaji ni uwendawazimu"
 
Hata kama ni bazazi, alichosema ni haki yake kukisema. And so far, kila nikiangalia vidole vya hao wanaojiita viongozi wetu sikosi kuona pete ambazo zimetajwa! Kwa nini nisiamini kuwa nchi inaongozwa na walala makaburini? No wonder mambo yako hivi yalivyo
......... mapapa wa Kikatoliki wote wana "Pete" vidoleni mwao ambazo hupewa na Kanisa, Makadinali wote (akiwamo Pengo !) wana "Pete" wanazopewa na Kanisa. Hizi nazo vipi ? :juggle:
 
Back
Top Bottom