Mahakama kuu imetoa hati kukamatwa Nabii na Mtume Josephati Mwingira

Hivi unaweza kumkamata Nabii?

Nabii alithibitishwa na nani kuwa nabii?

Hivi mtu yeyote akijiita nabii anapata immunity?

Hapa ni masuala ya Sheria, na kama binadamu anayejiita nabii anapasika akamatwe kutokana na tuhuma za makosa ya jinai, WHY NOT?
 
watu wanafurahia matatizo ya watu wakati ukiangalia wao wanaishi katika dimbwi la umasikini na hawana mawazo ya kudhani ni kushabikia matatizo ya wengine ni faraja kwao.

Tanzania ni nchi tajiri yenye raia masikini wanaopenda kushabikia mabaya yanayowakuta wengine bila kujua wao wanamatatizo gani
 
Hao polisi wazushi wangekua wanamtafuta wangekua washampata ukienda mwenge efatha yupo sana tu waende pale wakumuarest
 
Sasa nimeweka picha za bomoa bomoa hii ya kitume na kinabii. Fuatilia stori hii kuhusu AFROplus na Nabii na mtume Josephat Mwingira.
 
Nabii na Mtume Joseph Mwingira amesema, yeye ni Mtume wa mitume wote duniani na hawezi kuogopa na polisi wanao mtafuta.

Amesema serikali ya Tz inaongozwa na watu wanalala makaburi na kuchanjwa chale na waganga wa kienyeji.

Amesema viongoz wakuu akiwemo rais wanavaa pete za wachawi na hirizi hivyo hawana uwezo wa kupambana naye.

Akiongea kwenye ibada alisema kama wananisaka kwa nini wasijekunikamata hapa kanisani? Nitapambana mpaka kieleweke, Nipotayari kufa. Amewataka waumini wake wasitishwe na viogozi wa serikali wanaolala Makaburini.
 
Hata Yesu anayeaminiwa na Mwingira aliwakandia viongozi lakini sio kwa style ya Mwingira ambaye nyuma ya pazia ni mnyang'annyi na mfanya biashara mashuhuri kama kina Barabas. Mtume hajifagilii mwenyewe. Kila ajikwezaye atadhiliwa na kila ajidhiliye atakwezwa.

Historia ya uendeshaji wa kiroho wa Mwingira umejaa shaka tupu, lakini ajuaye kuhukumu vizuri ni Mungu mwenyewe. Mwenzake Kakobe alijifagilia sanaaa lakini somo limeanza kupanda kichwani kidogo siku hizi japo baaaaado kabisa. Watenda kazi wa Mungu wa kweli kwa kawaida ni vigumu kuwaona ila kwa kazi zao, nao wapo wengi tu. Kila debe lililo tupu hutika mno!

Paulo alionya sana, lakini maonyo ya Paulo si rahisi watu kama Mwingira wakafurahia kuyafanyia kazi, achilia mbali kuyatafakari kwa ajili yao wenyewe. Kawaida watu wa style ya Mwingira kila asomapo Maandiko anatafakari kwa namna ya kumhusu anayekwenda kumhubiri, yeye mwenyewe anadhani hayamhusu maana tayari anadhani amekubaliwa na Mungu. Hilo nalo, ni tatizo kubwa.
 
utume wake amepewa na nani...? kitabu gani ameshushiwa...? aache kudanganya watu kwa tamaa ya tumbo. huko anakoenda sasa (kuwatukana viongozi wa serikali) ajiandae kufirisika.
 
Mtume wa Mitume, means YESU na Mohamad wote wanapay respect kwake? kazi ipo kwelikweli
 
Mmh,kwakuwa nimeisoma hii hbr,wala sitashangaa nikickia efatha bank inaendeshwa kinyume na taratibu,
ila wapo weng waichukiayo serikali na kuidharau,miongon mwao ni hawa walosafirisha twiga we2,waliogoma kuvunja ukuta wa Jangwani,
 
Back
Top Bottom