Mahakama Arusha yaizuia CDM kuwazomea madiwani

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Mkoa Arusha imetoa uamuzi mdogo wa zuio la muda dhidi ya mikutano ya Chadema kuwasema hadharani madiwani watano wa chama hicho waliotimuliwa.

Mahakama hiyo pia imesema hata kama Chadema itapata kibali cha kuhutubia kihakikishe suala la madiwani hao halizungumzwi wala kuzomewa, kuwatolea lugha chafu na za vitisho wakati huu ambao hapo kesi ya msingi imefunguliwa.

Source: HabariLeo
 
sometimes unajiuliza hawa maakimu wengine ni nani hivi anayewapa uhakimu kwa maana wamefikia mahala mpaka ku control speech.
nani amekupa mamlaka ya kuzuia watu wasitoe maoni yao kwa kuwaambia nini wasizungumze na nini wazungumze ktk kutoa maoni yao ??
hakimu/polisi siku zote inapojiingiza ktk kuwaamulia watu kitu cha kuzungumza au kuwakataza watu kwa kusema maoni haya ni mabaya au haya ni mazuri inajiingiza ktk kazi ambayo hiko juu ya uwezo wao kwani maoni hayo yanaweza kuwa mabaya au mazuri kutegemea mtu na mtu hii ni sawa mahakama kutuchagulia mwanamke mwenye sura ya aina gani ni mzuri au mbaya??
 
Mahakama inataka waendelee kuwa CDM? kama CDM imewakataa wanataka nini? si vyama vya siasa ni vingi si waende huko? au ndio maagizo waliyopewa na magamba? Hata hivyo mahakama haiwezi kushindana na nguvu ya umma wanachofanya ni kuzuia uchaguzi usifanyike haraka. Wasaliti hawawezi kuvumiliwa. Nawatakia kila la kheri mahakamani, hatuwachukii kama binadamu bali matendo yao maovu.
 
Nilifikiri wamefungua kesi ya kupinga kufukuzwa kumbe ni ya kudhalilishwa mazoba kweli watahangaika sana hiyo ndiyo imetoka
CDM sasa inakazi moja tu kulichukua jimbo la fisadi.
 
CCM na vyombo vyao vya habari wako makini sana kufuatilia masuala ya madiwani wa cdm. Laiti wangefuatilia kudhibiti mgao wa umeme, mafisadi, mishahara bora kwa nguvu hii............
 
Ama kweli wewe kichwa cha masaburi, hakimu atoe tamko la umeme? si mpelekee kesi.
za mbayu wayu changanya na za kwako.. nielewe kwanza sio unatafsiri kila kitu kama kilivyo ...angalia kuna nini kwanza ndani ya post utaja ingia chaka
 
Haruna rais, hatuna mawaziri, hatuna serikali. Hii nchi ni f. up kabisa. Nauliza kwa nini kwanza waitwe madiwani? CDM inawaona hao ni watu tu wa kawaida kwani ilishawanyang'anya kadi. Kama wanan'gang'ania wao ni madiwani basi wanapokuwa katika vikao vya Baraza la Madiwani wataje wao wako humo kwa tiketi ya chama gani? Hawa watu ni wajinga kabisa kwenda mahakamani kwa kesi kama hii -- wanataka kitu gani? Ni bora tangu sasa mahakama zitangaze basi kwamba kama chama kinataka kumfukuza mnwanachama wake basi kiende mahakamani kufanikisha hilo -- yaani namna ya kufukuza kihalali ili kusiwepo migogoro. Shit!
 
Mahaka inapelekwa kwa nguvu za magamba wanapoteza muda kujipanga jinsi magamba watakavyonyakua hizo sehem walizoacha wazi. Muwe makini magamba zuluma inaumbua angalia mliyofanya mwaka jana kuzulumu baadhi ya majimbo na waangalie sasa mambo yanavyowashinda kuanza rais baraza la mawaziri mpaka ngazi za chini
 
wtoe tamko kuhusu waliotuletea mgao wa umeme pia.. wasiishie hapa
Hapo mdau umenena, hivi vyombo vyetu vya serikali vinaweza kuona sana mikutano ya chadema ila si matatizo yanayotukabili. intelejinsia ya polisi haina uwezo wa kuona wachakachuaji wa mafuta, kitu kinachopelekea mafuta kupandishwa bei wala hilo hawalioni, mahakama hazioni hawa mafisadi ambao wamelitafuna taifa vibaya na ushahidi upo ila wana uwezo wa kujua ni diwani gani kazungumziwa kwenye mkutano wa chadema. huu ni uzuzu wa hali ya juu!!!!!
 
mahakama imekitaka chama cha democrasia na maendeleo chadema kutowaongelea madiwani 5 walio wafukuza mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa. mahakama ipo kwa ajili ya kutenda haki na kusimamia sheria nchini.
 
Sheria ipi?ya kutetea wahalifu na kukandamiza wasio na hatia?sina imani na mahakama za TZ hata kidogo,KAZI KUWABEBA MAGAMBA TU.
 
Mke anamtaka mume kwa lazima kutumia mahakama..Acha tuone kama talaka itachanwachanwa na mume abebe dem lake.
 
Back
Top Bottom