Aisatu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 775
- 321
Japo bado sijapata kazi rasmi, nina ushuhuda wa kuwapa enyi watafutaji wa kazi kama mimi mja wa MUNGU. Kuna waajili wengine hapa nchini wanachangia kutufanya tuonekane kuwa tuna maisha magumu na ionekane kuwa tuna shida sana ya kupata kazi japo sio kwa wote, nakumbuka tar 1/8/2014 +255652198676 company X ilinihitaji kufika dar kwa ajili ya usaili wa Fertilizer Sales Person kwa bahati nzuri nikawaambia nipo nje ya dar kwa maana kwamba npo mkoani, nikasisitizwa kuwa nijitahidi nifike siku hiyo nikajipanga nikaamua kufunga kabiashara kangu hapa mjini ili nielekee huko dar kwa interview. Kitu Cha ajabu ni kwamba nilipoanza safari njiani walikuwa wakinipigia simu kuwa nmefika wapi, ile npo kimara tu, nikatumiwa sms kuwa wamearisha usaili wangu mpaka wiki inayofuata (nitapigiwa simu). Sikuwajibu nikasubiri mpaka niliposhuka kwenye basi ubungo, nikajaribu kuwasiliana nao lakini hawakunielewa kabisa na nikadiriki kuwaomba wanichangie japo nauli ya kurudia POLE SANA MKUU