Magufuri na serikali washitakiwe

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,142
18,769
Watu wanakufa kila siku, magari kuharibika vibaya, kutokana na kuwepo kwa mashimo ya ghafla barabarani ambapo hakuna hata alama inayowekwa kutahadharisha madereva.

Ukifikiria kwamba kwa kila lita ya petroli au dizeli tunayonunua tunalipia road toll, kwa nini basi ndugu zetu, rafiki zetu wafe, na magari yetu kuharibika wakati tunalipia fedha nyingi angalau haya mashimo makubwa ya ghafla barabarani yafukiwe? Mara ngapi maisha yako yameponea chupuchupu kwa kuwa kulikuwa na shimo ghafla barabarani? Mashimo mengine yanakuwapo kwa zaidi ya mwaka. Mameneja wa Tanroad mikoani wanafanya nini?

Kwa nini serikali huwa inaacha yanazidi kuchimbika zaidi na zaidi kila siku, huku yakiua watu na kuharibu magari yao?

Magari kugongana au kupinduka kwa ajili ya uwepo wa shimo barabarani sasa kimekuwa kitu cha kawaida. Kwa nini Watanzania tunakuwa wapole kiasi hiki, ukichukulia kwamba tunalipia fedha nyingi mashimo hayo yaondolewe?

Jamani, huu ni uuaji wa watu wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom