Magufulu,Balozi Mlango vipi hizi bilioni 300?

Sabato masalia

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
228
134
Hivi sasa waziri wa ujenzi bwana Magufulu na katibu mkuu wake anaemaliza muda Balozi Mlango wako katika heka heka kubwa kuiomba hazina iidhinishe bilioni 300 kwa ajili ya kuipa Tanroads ilipie madeni kwa makandarasi wa barabara, cha kujiuliza hizo barabara zenyewe ziko wapi? kama si utapeli kitu gani? ukichunguza kwa makini hayo madeni mengi ya Tanroads ni hewa, pesa nyingi anachukuwa Mtendaji wa Tanroads bwana Mfugale kupitia kampuni ya Chico na kugawana na wakubwa wake, Magufuli,Mlango na Mfugale muogopeni bwana Mungu jueni anawaona na atawahukumu mbele zake kwa dhulma mnayofanya. na wewe mchina wa chico unayetumika kupitisha hizo pesa ukome nakukemea kwa jina la kristo.
 
Back
Top Bottom