Mh. Magufuli tathmini comment za watanzania kwenye hotuba zako

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Habari wanajmvi,,,,,leo nataka tujadili comment za watanzania kwenye hotuba ya magufuli.

"Bora nichukiwe na watu 1000 na nipendwe na watu milioni 50,Kama nitaboresha maisha ya Watanzania hata kwa Mungu nitapokelewa"-Rais Magufuli.

Comment.

1. Ukichukiwa na wengi maana yake wewe ndio tatizo, huwezi kusema unapendwa na watu milioni 1 na unachukiwa na watu milioni 49 halafu wenye matatizo ni hao milioni 49, hapana, ni wewe ndio tatizo na kwa Mungu sahau!

2. Usani mtupu, hakuna ajira, hakuna mikopo kwa wanafunzi, maisha magumu, hakuna dawa mahospitalini, ni vigumu sana kupendwa hata kama unajivuniaje masiki ni masiki tena zaidi kuliko kipindi icho na tajari amebaki vile vile kwahio unampigania yupi? Ni usani tu.......hayo maoni yangu binafsi.

3.Tatizo lako unaanza upya kwa nchi kama yetu unaangamiza hao unaotaka kuwatetea wewe ulichotakiwa kuendeleza kwanza mfumo uliyoukuta wa jk uku unaingiza kidogo kidogo Mfumo Wako Wa Utawala wewe umeingia na miguu miwili ukizani unatutetea Kumbe ndiyo unatumaliza watanzania waliyo wanyonge kila sehemu galama juu afya dawa hakuna walimu mitiani waandike ubaoni kalatasi hakuna eti elimu bule.

4. Mmh yatosha ss,tumechoka iyo tathmin ifanywe vzr idadi ya wanaokuchukua itakuwa kubwa zaidi na hao ndo wenye ukwel.maisha ni mgumu mzee si kwa wafanyakazi na wala si kwa wana Nchi wa kawaida.

5.Kuchukiwa au kupendwa ni kawaida ukiwa kiongoz lkn unatakiwa ujue sababu why unachukiwa, na je wanakuchukia kwa haki au majungu???? Then ukijua sababu tafuta njia ya kutatua tatizo najua hauwez kuwaridhisha wote but jaribu ata kupunguza wanao kuchukia.... Na kuusu kufka mbingun unatakiwa kutenda hak dunian then utafika mbingun na km umetenda haki bac mbingun utafka...

6.Habari ya mjini ni 2020 utuajua watu wanakupenda au la, halafu kwamungu sikwamzungu matendo ndo yatakufanya umwone mungu.

7.Ukweli bado utabakia kuwa ukweli,watanzania walio wengi wako hoi bin taaban,hizo sifa wanazisikia na kuzisoma kwenye vyombo vya habari.Ajira hakuna,kilimo cha uhakika hakuna,kila leo afadhali ya kesho.Tujisifie lakini tuangalie na maisha ya watu wa kipato cha chini yakoje.

8. Muongo sana jamaa mbona miladi ya maendeleo kwa wananchi unaizuia yote iliyo mizuri eti kwa sababu imeletwa na wapinzani? Muongo sana jamaa.

9.Tatizo langu ni hapa jina "Mungu" namna linavyotumika kana kwamba naye ni mwanasiasa! Sielewi!!!!

10.Pumba za kila siku tumezoea.

Nini comment yako kwenye kauli yake hvyo au comment gani ni nzuri.

Hapa kazi tu............
 
Mh. Inabidi ifike hatua apunguze media coverage. Kuna mambo si lazima azungumze au kuwepo yeye. Wasaidizi wake wanatosha na wanaweza kusimamia mambo kwa weledi tu.
 
."Ukiwa mpya lazima watu waone una mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo, Sio mapya ya kubomoa ya kule tulikotoka
 
Sometimes mkulu he is too emotional and personal...unapoongoza watu kila mtu ana maoni yake na mawazo yake sio kila mtu atakupenda kilicho cha muhimu ni concentrate na plan uliyo jiwekea sometimes sio kila masikio yameumbwa kusikiliza kila aina ya maneno..so its good kuchagua yapi ya kuzungumza, ninaamini matendo yanatosha kujibu watu wanao kupinga ila sio maneno. [HASHTAG]#Nohardfeelings[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom