Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Pasco, hiyo dhana ya kulinganisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ndoa ya Kikiristu ya hadi kifo kiwatenganishe - si sahihi hata kidogo. Rejea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - inatoa mchakato unaopaswa kufuatwa katika kuvunja Muungano huu. Mchakato huu unaishia na kura za maoni kwa pande zote mbili na kugawana mali na madeni ya masuala ya Muungano.
Muungano unatawaliwa na mkataba wa muungano au hati za muungano!, hakuna kipengele chochote kinachotoa provision ya huu muungano kuvunjika!.

Katiba imetoa fursa kama kuna upande una malalamiko, uindwe mahakama ya katiba kuyashughulikia malalamiko hayo. Tangu kuundwa kwa muungano, hapajawahi kuwepo malalamiko yoyote rasmi, hivyo hiyo mahakama ya katiba ipo tuu kwenye katiba ya JMT (1977) lakini haijawahi kuundwa!. Kilichopo ni kero tuu za muungano na zinatatulika kwa mazungumzo ya mezani!.

Pasco
 
MIMI NASEMA HIVI: KAMA UDIKITETA WA RAIS JPM NI KWA AJILI YA KUTULETEA MAENDELEO WANANCHI, BAAASI ME NAOMBA AUONGEZE HUO UDIKITETA HADI UFIKIE ASILIMIA MILIONI
 
Dikteta akikuchukulia mkeo utalalamika?

Ukishakubali mtu awe dikteta, huwezi kumpangia awe benevolent dikteta.

Unachosema ni kama mtu anayetaka kumpanda chui mwenda mbio.

Unaweza kufurahi ukiwa mgongoni kwake na kasi anayokwenda, lakini ukifika unapotaka ukitaka kushuka utakiona cha mtema kuni.
Mkuu Kiranga, wala sio dikiteta, kwa sisi watu wa Kanda ya Ziwa, mwanamke sio issue kubwa sana kwa sababu by nature sisi ni watu wa wanawake wengi!, mtu ana wake 20, hata iweje lazima atasaidiwa na huwa hatulalamiki, hata mimi wife yuko US tena kuna kabinti kangu huko ni keupe ajabu!, na silalamiki!.

Tanzania tulipofika tulimhitaji dikiteta, tumempata Magufuli ambaye ni dikiteta mwema, hii paleka peleka ndio ndio kwanza imeanza na mwisho wa siku tutafika tuu!.

Pasco
 
Tunaleta jeuri huku tukiwa tunaishi juu ya mafuta na gesi!!!
Pia Magufuli akumbuke kwamba kauli zake hizo pia ni 'fyoko-fyoko' kwa wakubwa wa dunia, so, ina maana na yeye ajiandae kushikishwa adabu na hao wakubwa!?
Tanzania si kisiwa...kutosafiri kwake hakuifanyi Tanzania kuwa kisiwa.
 
The Greatest Love of All, is learning to love yourself, and kujiappreciate mwenyewe, kuwa satisfied na jinsi ulivyo au chochote ulichonacho, regardless wengine wanakuonaje!. Ulifanikiwa katika hili, utakuwa bold, you can speak out your mind bila kujikomba komba kwa mtu, bila kumuogopa mtu, bila kumuofend mtu bali nguzo yako kuu ni "to speak the truth no matter what". Hiki ndicho ninachokifanya humu jf wakati wote!.

Pasco
Safi sana.
 

Acha kuandika pumba kwani nini Majeshi yetu yakaue watu wasio kuwa na hatia?
Vyombo vyetu vya usalama viko kwa ajili ya kulinda usalama wetu hivyo yoyte yule atakayedhurika ni kwamba hakutii Sheria za nchi yetu ni rahisi kihivyo tu, ikitokea kweli kwamba kuna mtu hatii sheria basi ni lazima vyombo vitamshughulikia lkn ukiwa raia mwema hakuna wa kukugusa!

Nani umemsikia akisema atawashughulikia watu wasio na HATIA? Maghufuli anawashughulikia watakaoleta fyoko fyoko.!! Kuleta FYOKOFYOKO tayari no hatia
 
Wanabodi,

Angalizo. Neno Dikiteta sio neno baya kama lengo la matumizi yake ni lengo jema. Tikisema Magufuli ni Dikiteta, hatumaanishi ni Dikiteta Mbaya kama Hitler!, no way, Magufuli ni Dikiteta mwema anayeitwa Benovelent Dictator!. Tanzania hapa tulipofika, tunamuhitaji mtu kama huyu ili mambo yaende!.

Kwanza watu wengi hawajua kuwa Magufuli anaweza kuja rais wetu wa awamu ya tano, akina sisi, hili tuliliona tangu mwezi August mwaka 2014 na tukalisema humu japo watu hawakulitilia maanani lakini limekuja kutokea, Magufuli sasa ndio rais wetu!. Hata baada ya Magufuli kuwa rais, bado kuna baadhi ya wenzetu wanaamini Magufuli amekuwa rais wetu kwa bahati tuu!, sisi waumini wa everything happens for a reason, tunaamini kunayo sababu kwa nini ni Magufuli, na nimeieleza humu!. Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli!.

Mchakato wa kumtafuta mgombea kupitia CCM ulipoanza, nikawachambua wagombea wote wa CCM, na miongoni mwa vigezo vyangu, hili la udikiteta pia nililisemea!.
Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5, Top 3 na kumtoa Rais wa 5 wa Tanzania!.

Baada ya kuchaguli kwa Magufuli kuhusu udikiteta wake nilisema hivi.
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki
.

Kwenye suala la Zanzibar, mara kibao tumewauliza CUF kwa nini wanapiga tuu kelele bila kuchukua hatua?!.
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchuku hatua!.
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima .
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?.

Kuhusu kususa kwa CUF kushiiki uchaguzi wa marudio Zanzibar, nilisema CUF wasitake kutisha watu kuhusu amani na utulivu wa Zanzibar, kwa sababu Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT, hivyo amani na utulivu wa visiwa hivyo, sio jukumu la Wanzanzibar wenyewe pekee, bali ni jukumu la JMT na mwenye dhamana ya amani na utulivu wa nchi hii ni Amiri Jeshi Mkuu, wa vikosi vya ulinzi na usalama wa nchi hii. Jana ameonya mtu yoyote atakayeleta fyoko fyoko atashikishwa adabu!. Hivyo CUF mshirriki uchaguzi, au msishiriki, uamuzi ni wenu, tunachotaka sisi ni heshima, adabu, amani na utulivu, vinginevyo mtaisoma hii namba!.

Jumapili Njema.

Pasco

Haya mambo ya demokrasia,
Utawala bora,
Haki za binadam
Natural justice
Na vingine vingi ni ubatili tupu
Hasa nchi hii ilipokuwa imefikia.

go
go
Go
Go JPM.

"TILITAKA MABADILIKO NA TUKASAHAU MABADILIKO NI MACHUNGU SANA LAKINI UTAMU WAKE HUJA BAADAE"

NavyboI
Senior citizen
 
Mpendwa Rais wetu JPM. Watanzani wazalendo tuko nyuma yako kila siku tukikuombea kwa mungu uwe na afya njema, maisha marefu, na utekeleze majukumu yako vizuri sana. hatuna uwezo wa kukulinda, ila mungu wa mbinguni atakulinda na atakuwa pamoja nawe daima. tungekuwa na uwezo wa kukulinda hata tusingeruhusu mtu yeyote akuguse hata hata kwa salamu tuu.. na tusinheruhu ukanyage chini. ila kwa sababu huo uwezo hatuna sisi tunakukabidhi mikononi mwa mungu. kamwe usiulegeze upanga wako fyeka wooote wenye nia mbaya na nchi wala usiogope Bwana yuko nawe usiogope hutakufa
 
Kumbe tumefikia hatua ya kumuona mtu anayefuata sheria kuwa ni dikteta. Ina maana kuwa wenzetu bado wanataka mtu anayechekacheka na kuacha sheria zinavunjwa na watu wanaiba mchana kweupe, asiye dikteta
 
Magufuli atapeleka majeshi Zanzibar kwenda kusimamia amani na utulivu, ikitokea majeshi yakaua mtu, itakuwa mtu huyo ameleta fyoko fyoko!. Mtu akileta fyoko fyoko atashughulikiwa kikamilifu!. Ikitokea wengine wasi na hatia wakadhurika katika kututuliza hizo fyoko fyoko, then aliyesababisha madhara hayo ni muanzisha wa fyoko fyoko na sio mtulizaji au mdhibiti wa fyoko fyoko!.

Dawa ni moja tuu kwa Wanzanzibar, baada ya kumsikia Amiri Jeshi Mkuu akiwaonya msilete fyoko fyoko, hili sio ombi ni amri, hivyo msilete fyoko fyoko!.

Pasco
Swali: Ingetokea Seif akawa rais Zanzibar je Magufuli angeendelea kupeleka majeshi kulinda amri za serikali ya CUF?
 
Back
Top Bottom