Ng'ombe akikatika mkia hazuiwi kuingia zizini, ila...; Wale waliorudi wanajisikiaje?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Inatia ukakasi kama si kinyaa,pale unapoona mtu mzima mwenye hekima anatoka mbele ya adhara nakusema CCM haiwezi kuongoza tena na sasa nimeamua kuwa mpinzani kwa vigezo hivi na vile, baadae njaa inamshika maana upinzani hakuna mkato. Hali inapokuwa ngumu unasikia narudi nyumbani!

Hapo unajiuliza nini kimebadilika? Nimeshukuru jana Mwenyekiti wa CCM Rais JPM kasema "Ng'ombe akikatika mkia hazuiwi kuingia zizini ila akiingia Ng'ombe wenzake umjua kuwa amekatika mkia"

Hivyo niwakumbushe nyie tanga tanga hata mkirudi CCM nyinyi mlishapoteza imani kwa hali ilivyo CCM nyie ni wapinzani.

Pia Abdallah Bulembo kasema kinachowarudisha nini wakati mliondoka kwa matusi mbwembwe? Hata mkirudi bado hatuna imani na ninyi.

Mytake: Nyie mnaotangatanga CCM haitakuja kuwapa uongozi kamwe mnajisumbua na kujidhalilisha.
 
Mwenyekiti alisema wale walo imba imba kuwa na imani na lowassa angewapoteza....lakini ndio hao wanao rudi....na kuwapokea....kwa shangwe...
 
Hahaaa, kwa hiyo kwa maneno hayo ya 'chameni' wanachama wa chama hicho ni mang'ombe au?!
=Chama Cha Mang'ombe.
 
Namuunga sana mkono Mh Magufuli sana sana.nimefuatilia sana sana kuhusu democratic party na republican party. Pia labaur party vs conservative party mbona watu wao uwa kamwe hawaami vyama vyao kbsaa kbsaa jamani
 
Wewe unadhani wamerudi bure ccm wamenunuliwa hao kwa ela ya kunogesha kikao Chao ndio maana walisema upinzani utatikisika kumbe wolper Na msindai Na mpendazoe wote hakuna aliyokuwa kwenye safu ya uongozi
 
Hahaaa, kwa hiyo kwa maneno hayo ya 'chameni' wanachama wa chama hicho ni mang'ombe au?!
=Chama Cha Mang'ombe.

Kuna wanachama na pia mang'ombe yanayotangatanga na kurudi.
Mwanachama mwenye akili na wa kutumainiwa, haondoki na kurudi.
 
Kuna wanachama na pia mang'ombe yanayotangatanga na kurudi.
Mwanachama mwenye akili na wa kutumainiwa, haondoki na kurudi.
Mkuu, unaweza usiwe sahihi kwa mujibu wa nukuu iliyoletwa hapa kama ni ya kweli.
Wewe unadhani 'mang'ombe yenye mikia' ni yapi?! Maana kwa nukuu hiyo, hayo yanayotangatanga ndiyo yale yaliyokatika mikia!
 
Mkuu, unaweza usiwe sahihi kwa mujibu wa nukuu iliyoletwa hapa kama ni ya kweli.
Wewe unadhani 'mang'ombe yenye mikia' ni yapi?! Maana kwa nukuu hiyo, hayo yanayotangatanga ndiyo yale yaliyokatika mikia!

Kweli mkuu,
Kuna mang'ombe yaliyo ndani na yale yanayotangatanga hadi yakakatwa mikia na kurudi ndani.
 
Njaa ya kutoka wapi ,wakati hata chadema tuna hela nyingi tu, hadi bavicha wanajipiga ngwala na kujiibia wenyewe million 10 za posho???
 
"Sisi wafugaji, ng'ombe akikatika mkia huwa hatumzuii kuingia zizini ila akiingia zizini ng'ombe wenzake humjua kuwa amekatika mkia". Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli. Dodoma mkutano mkuu wa ccm 23/7/2016.
 
Back
Top Bottom