Magufuli: Lipumba amevunja sheria kupanda punda kwenye lami

Magufuli amesema Lipumba amevunja sheria ya farasi au ya punda?

Magufuli pombe hajui asemalo. Wakazi wengi wa Igunga wanatumia usafiri wa punda. Kwa hiyo anatoa taarifa kwamba serikali ya ccm itawafikisha mahakamani.

Hakujua implication ya alichonena. Nadhani usingizi ulimpaa baada ya tafakari, kama alifanya hivyo.

Kejeli nyingine kwa wapinzani zinakibomoa ccm.
 
Ndugu yangu Dkt. Magufuli umebaki wewe tu msafi ndani ya Chama cha Magamba uwe makini tusije tukakuona na wewe "gamba". Tulia
Hana usafi wowote, unjidananya bure. Kama angekuwa ni mtu safi asingeweza kusimamia mpango wa kulitia hasara taifa hili wa uhamishwaji wa mali za umma za thamani ya mabilioni ya shilingi (nyumba za Serikali) kutoka miliki ya pamoja na kuhamishia kwa vigogo wachache huku yeye mwenyewe akinufaika pia na mahawara zake wasio kuwa na sifa zozote.

Nenda pale Kinondoni katazame moja ya nyumba zilizokuwa za serikali alizojimilikisha alivyojenga maghorofa manne, pesa kapata wapi, kama na yeye sio fiisadi. Ndio maana anawateeta magamba kufa na kupona.
 
POMBE hajui kama na yy amevunja sheria za uchaguzi?huyu jamaa anakalili sana,aangalie asiharibu taswira yake mbele ya jamii
 
Saa nyingine nashindwa kuelewa mantiki ya mtendaji wa serikali kujihusisha na siasa
Huyu pombe anatumia wajibu wa serikali Kama ahadi za siasa
ohh Mara nitajenga daraja ohh nitafanya hivi sasa hayo si ni majukumu ta serikali?
 
kama anataka sarakasi za siasa uchwara, aendelee tu!!!
Tutamwambia aturudishie nyumba zetu za serikali na zile alowauzia mahawara zake na ndugu zake!!!

ha kumbe kawahuzia me nilidhani kawapa bure,serikali ina hela ya kuwalipa mkitaka awarudishie?imetoka hiyooooo
 
kwa staili hii basi hawezi kuishi India maana huko kun balaa punda anamadhara gani kwani jmn maana angekuwa heavy weight anaharibu barabara ingekuwa sawa watafute sera mbadala za kuwashawishi watu wawape kula na kuna matatizo mengi yanatakiwa kuongelewa hajayaona hayo kaliona la punda? Poor Magufuli
 
POMBE hajui kama na yy amevunja sheria za uchaguzi?huyu jamaa anakalili sana,aangalie asiharibu taswira yake mbele ya jamii

Hana jipya huyu kasababishia hasara TZ kwa kuuza nyumba za serikali bila utaratibu pamoja na kuwadhurumu wananchi wa biharamulo barabara lao la lami, jana yy na mzee mwenye sura kama..,.? Wamedanganya kujenga daraja la mbutu na kupeleka maji igunga kutokb shinyanga kwa BAJETI IPI HALI BUNGE LIMEMALIZA KIKAO CHAKE? Igunga msidanganyike PEOPLEZ PAWER
 
Ndugu yangu Dkt. Magufuli umebaki wewe tu msafi ndani ya Chama cha Magamba uwe makini tusije tukakuona na wewe "gamba". Tulia

Mkuu kwa hiyo mtu akitulia tu kwako ni sawa hata kama ana matatizo? Magufuli ni mwanachama wa CCM kwa hiyo lazima aitetee CCM.
 
magufuri hajatofautisha aina za wanyama kuna wale ambao kweli hawaruhusiwi kupanda kama alivyofanya lipumba lkn mnyama kama punda
 
Sheria hii ni kwa igunga tu? ama! huko vijijini tunakopanda na kulimia mbonahatujawahi kusikia wakitetewa hawa wanyama? Mbona kama ni haki na sheria zinavunjwa kila siku iweje hii? ninamashaka na siasa hizi?
 
Alitania tu jamani. Kuhutubia watu kwataka kachumbari kama hizi ili usiwachoshe. Kwanza Lipumba hakupanda punda bali alipanda mkokoteni ulookuwa ukivutwa na punda.
 
magufuri hajatofautisha aina za wanyama kuna wale ambao kweli hawaruhusiwi kupanda kama alivyofanya lipumba lkn mnyama kama punda

Magufuli kiboko. Anatumia uzoefu wake: Wakati yupo Wizara ya Kilimo na Mifugo alikuwa akisimamia sheria ya wanyama na ngozi kwa hiyo akakumbuka sheria ya ngozi na kumtuhumu Lipumba kwa kumpiga punda aliyempanda. Kama waziri wa Ujenzi anasimamia sheria ya barabara ya mwaka 2007 akakumbuka kwamba ni kutotii sheria kwa kupanda punda (mkokoteni unaovutwa na punda) kwenye barabara!!
 
hivi alisema kuna punda wangapi TZ? maana kwa takwimu yule bwana ni kiboko sijui huwa ni za kweli au anatulisha sumu!!!!
 
ccm na siasa za maji taka...............mmekwisha.........cuf si ndo haohao ccm jamani?,...kwa nini watz tunadanganywa hivi?.......acheni unafiki tafadhari
 
Magufuli amesema Lipumba amevunja sheria ya farasi au ya punda?
Sasa nime-confirm kuwa ukishabikia ccm au uwe mwanachama wa ccm ni lazima uwe less, kwanza ukiangalia uwezo wako wa kutofautisha kati ya punda na farasi ni mdogo sana, pili sheria anayoiongelea Magufuli ni ya wanyama haijalishi ni mnyama wa aina gani kupita kwenye lami, tatu huyu Magufuli unayemtetea hajui kuwa licha ya watu wanaoishi mijini kutojua sheria za nchi sasa hawa wenzangu wa vijijini wataanzia wapi?, kwa hyo wanapomsikia anahubri sheria wanashangaa sana. Nne usikurupuke kumjibu mtu eti kwa sababu tu kaongelea kitu kinachokugusa ama kukuuma au kimekukela, unahitaji kukaa, kuwaza, kupembua ulichowaza, kufanya tathimini, then wasilisha mawazo yako la sivyo utakuwa less kila wakati, tano unapojipanga ku-quote thread hii usikurupuke tena utaonekana more than less
 
Back
Top Bottom