Magufuli kwa hili umekosea hebu fikiria upya

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
318
Nimeshangazwa na kauli ya magufuli kutaka kuboboa jengo la tanesco najiuliza je tutakua tumepoteza sh ngapi za kodi zetu kukosa plan nzuri ya jiji letu hapo mwanzo'ni kweli jengo liko kwenye road reverse pia ina maana ile mitambo ya umeme nayo itaondolewa itakuwa usumbufu mkubwa na kuleta kiza kwa muda usiojulikana ushauri kwa magufuli watanue huku kwenye wizara maji na kuchukua eneo kubwa upande huo ambao hakuna wingi wa nyumba sana kupunguza hasara kubwa katika taifa
 
Mgema akisifiwa tembo hulitia maji. Hii ndiyo inatokea kwa Magufuli, inaonekana sasa amelewa sifa. Uongozi unatakiwa hekima na siyo nguvu na sifa.
 
Dr bomoa bomoa, atapiga chini ule mjengo, na asipofanya hivyyo wengine wataomba fidia.
 
dah wakuu ilo suala la maguful utata mtupu. kuna thread moja nimeisoma kuhusu maguful humuhumu jf kwamba ni mtu wa visasi au tuseme naye hakupata takrima kwenye zabun ya mjengo huo.

swala la kubomoa inabidi atulie sana asije akapoteza sifa ya uadilifu.
 
Hayo ndo matokeo ya Serikali yetu ya kifisadi!!! Inazarau kinga baadae inaingia hasara kubwa katika tiba!! Mimi najiuliza jengo hilo ni kubwa, na lilichukua muda mrefu kujengwa, hivi kwa muda wote wa ujenzi wake kwa nini hawakuweza kugundua kama ujenzi huo si halali?? Tumezoea kusikia watu binafsi wakivamia maeneo yaliyotengwa, jamani hili la Serikali kuvamia maeneo iliyotenga yenyewe ni kituko!!!!
 
Nimeshangazwa na kauli ya magufuli kutaka kuboboa jengo la tanesco najiuliza je tutakua tumepoteza sh ngapi za kodi zetu kukosa plan nzuri ya jiji letu hapo mwanzo'ni kweli jengo liko kwenye road reverse pia ina maana ile mitambo ya umeme nayo itaondolewa itakuwa usumbufu mkubwa na kuleta kiza kwa muda usiojulikana ushauri kwa magufuli watanue huku kwenye wizara maji na kuchukua eneo kubwa upande huo ambao hakuna wingi wa nyumba sana kupunguza hasara kubwa katika taifa

Kwani TANESCO walipokuwa wanajenga hawakujua kuwa ni eneo la Road reserve? Lazima walijua ila wakatumia ama ujanja au uzembe au jeuri. Na waliohusika wanatakiwa waadhibiwe.

Halafu sikubaliani na tabia hii ambayo watz tunayo. Mtu unavunja sheria kijanja janja, halafu unajaribu kuhalalisha eti kwa sababu umewekeza pesa nyingi, au umetoa ajira kwa watu, au umetoa huduma, n.k. Ndio ujanja kama huu wa akina richmond na dowans. Toka mwanzo wali-plan kutuibia, halafu sasa hivi baada ya kustukiwa wanasema tuwalipe kwasababu tumetumia umeme wao.

Mheshimiwa Magufuli na serikali wanatakiwa kukomalia hili suala la ujenzi wa ujanja ujanja. Sheria ni sheria, umejenga sehemu isiyotakiwa, unatakiwa kubomoa. Hebu fikiria mtu anachukua open space kiujanja, halafu anaweka kashule au kahospitali pale halafu eti asibomolewe kwavile eti anatoa huduma, hapana. Hii haifai.

Kama Tanesco wamekosea halafu wakaachwa, je wamiliki wengine nchi nzima waliofanya faulo kama hizo watachukuliwaje hatua?. Kama wanawaacha Tanesco basi wote waachwe. Hatutaki double standards.
 
dah wakuu ilo suala la maguful utata mtupu. kuna thread moja nimeisoma kuhusu maguful humuhumu jf kwamba ni mtu wa visasi au tuseme naye hakupata takrima kwenye zabun ya mjengo huo.

swala la kubomoa inabidi atulie sana asije akapoteza sifa ya uadilifu.

nashukuru kwa kuliona mkuu
 
Hayo ndo matokeo ya Serikali yetu ya kifisadi!!! Inazarau kinga baadae inaingia hasara kubwa katika tiba!! Mimi najiuliza jengo hilo ni kubwa, na lilichukua muda mrefu kujengwa, hivi kwa muda wote wa ujenzi wake kwa nini hawakuweza kugundua kama ujenzi huo si halali?? Tumezoea kusikia watu binafsi wakivamia maeneo yaliyotengwa, jamani hili la Serikali kuvamia maeneo iliyotenga yenyewe ni kituko!!!!

ni kituko tena kikubwa sana mno
 
Kwani TANESCO walipokuwa wanajenga hawakujua kuwa ni eneo la Road reserve? Lazima walijua ila wakatumia ama ujanja au uzembe au jeuri. Na waliohusika wanatakiwa waadhibiwe.

Halafu sikubaliani na tabia hii ambayo watz tunayo. Mtu unavunja sheria kijanja janja, halafu unajaribu kuhalalisha eti kwa sababu umewekeza pesa nyingi, au umetoa ajira kwa watu, au umetoa huduma, n.k. Ndio ujanja kama huu wa akina richmond na dowans. Toka mwanzo wali-plan kutuibia, halafu sasa hivi baada ya kustukiwa wanasema tuwalipe kwasababu tumetumia umeme wao.

Mheshimiwa Magufuli na serikali wanatakiwa kukomalia hili suala la ujenzi wa ujanja ujanja. Sheria ni sheria, umejenga sehemu isiyotakiwa, unatakiwa kubomoa. Hebu fikiria mtu anachukua open space kiujanja, halafu anaweka kashule au kahospitali pale halafu eti asibomolewe kwavile eti anatoa huduma, hapana. Hii haifai.

Kama Tanesco wamekosea halafu wakaachwa, je wamiliki wengine nchi nzima waliofanya faulo kama hizo watachukuliwaje hatua?. Kama wanawaacha Tanesco basi wote waachwe. Hatutaki double standards.

mkubwa una point kubwa sana hapo hata mimi huna najiuliza tanesco hawakujua ni eneo la barabara sema kama hujatoa jibu angalia na upande wa pili wa sh nafikiri tuwawajibishe viongoz wote wa tanesco kipindi cha mradi unatekelezwa pia waziri wa miundombinu kipindi kwa kututia hasara
 
TANESCO walipojenga ni eneo sahihi wala si eneo la Tanroads! Kinachofanyika ni siasa za kutoona mbali.
Magufuli akilibomoa maana yake amembomoa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndo mwajiri wake jambo ambalo ni kujibomoa!!
 
kama tanesco walikosea au selikari yanyewe ilikosea (Na wakati huo magufuli hakuwepo) acha wabomoe, sio kuonea raia tu, na watuhumiwa wachukuliwe hatua kali, inafika wakati hata kama dawa ni chungu vipi lazima umkabe mtoto ainywe ili apone, uendelee na majukumu mengine. na si vizuri kuhalalisha mambo kwa kigezo cha hasara labda kama nchi itauzwa.
 
sheria ni msumeno lazima ifuate mkondo wake........na ni lazima wahusika waliosababisha wachukuliwe hatua za kisheria
 
hawezi kubomoa... hana ubavu huo!!
ubavu anao kwa kuwa anafuata sheria,ila kwa nchi kama tz ambayo watu wake wanawaza leo tu hawezi,maana walio jenga walijua kabisa jengo lipo kwenye hifadhi ya barabara ila kwakuwa yeye alitaka 10% yake,basi hakutaka kuumiza kichwa
 
Back
Top Bottom