Magufuli kiboko: Meneja wa TANROADS akemewa kama mhudumu!

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
246
Magufuri ni Kiboko kweli. Jinsi anavyokaripia watendaji wa wizara yake inatisha. Muda si mrefu uliopita ameonekana kwenye taarifa ya habari TBC1 akimkaripia Meneja wa Tanroad mkoa wa Dsm kama anamgombeza mhudumu vile. So serious and irritated.

Mawaziri wa JK japo nusu yao tu, wangekuwa wanajiamini kama huyu jamaa tungepiga hatua japo kidogo kimaendeleo.
 
Huyu naye ni MLIPUKAJI tu kama Lowassa. Juzi kajisifu kuwa ujenzi wa barabara ni wa CCM na Serikali yake.Sasa hivi mbona kwenye Mafuriko, kajikalia kimya kama Boga la Halowini?
 
Magufuri ni Kiboko kweli. Jinsi anavyokaripia watendaji wa wizara yake inatisha. Muda si mrefu uliopita ameonekana kwenye taarifa ya habari TBC1 akimkaripia Meneja wa Tanroad mkoa wa Dsm kama anamgombeza mhudumu vile. So serious and irritated.

Mawaziri wa JK japo nusu yao tu, wangekuwa wanajiamini kama huyu jamaa tungepiga hatua japo kidogo kimaendeleo.
Hii actually ni weakness na sloppy management style. Anatengeneza tension bure, anawa demoralize wafanyakazi wake, anawaumbua hadharani watu wazima, anatengeneza uadui etc.

Angeweza kufanya yote hayo kwa maandishi, akawa na ushahidi wa kimaandishi kwamba alikwishaonya etc.

Hata mtoto wako akifikisha umri wa miaka 18 si uungwana kumshambulia mbele ya wenzake, unamuita pembeni na kumpa kisago.

Magufuli kwa kuwaka hivi anatuonyesha kwamba hapati taarifa mapema inavyotakiwa au anataka kuuza sura aonekane mnoko/mfuatiliaji.

Siku moja atakutana na mchizi asiyetegemea kazi yake atamkaripia atapewa majibu ya ajabu ya hapo kwa papo kama aliyopewa Lowassa na yule mjeshi mkuu wa wilaya kule Mwanza.
 
Jamaa anajua dhamira yake, mnafikiri mzee Benny anamsaport nani? Mtaona malengo ya huyu jamaa muda ukifika
 
Ndo utamaduni wa serikali yetu! Raisi aligombeza foleni iishe, bado twaiona. Wa mabondeni nao waligombezwa wahame, haya hao wanaogelea na kuelea. Sasa nae aligombezwa na mukulu aache kubomoa bomoa, nae anagomba mbele za watu. Tuone kama kugomba kunaondosha matatizo basi!
 
Hiyo ni hulka ya viongozi kutaka sifa kwa wananchi kwa kupitia migongo ya watendaji. Hata Lowassa anayo na huenda maombi ya wahanga wa tabia hiyo yamechangia anguko lake.
 
Hii actually ni weakness na sloppy management style. Anatengeneza tension bure, anawa demoralize wafanyakazi wake, anawaumbua hadharani watu wazima, anatengeneza uadui etc.

Magufuli kwa kuwaka hivi anatuonyesha kwamba hapati taarifa mapema inavyotakiwa au anataka kuuza sura

Anapenda kucheza na jukwaa huyu. Hana maana yoyote. Hivi angekua ndo yeye anadhalilishwa hivyo ni kiranja mkuu tena mbele ya watendaji walio chini yake angejisikiaje?

Hakika mkuu Kiranga umenena vyema. Aina ya utendaji huo wa John Pombe haufai kwani unawafanya watendaji kua waoga na wanafiki ili kumridhisha bwana mkubwa!
 
uongozi na utawala ni viipaji viwili tofauti kuwa navyo vyote ni majaliwa
 
Huko sasa ni kuzidisha na kupitiliza. Meneja/kiongozi unaweza kabisa ukawa firm bila kufokea watu na kuwaadhirisha hadharani. Kufanya hivyo ni kama kutafuta sifa vile. Unataka watu wakusifie...flani mkali bana..flani hana mchezo.

Sijavutiwa kabisa na management na leadership style ya Magufuli.
 
Hao wanajuana tu. Magufuli huwa anapanga na mameneja wake kabla kuwa atawagombeza ili aonekane anachapa kazi. Baadaye wanagawana posho za Meremeta na ubwabwa wa njano wa msaada kwa watu wa mafuriko.

Duh! Ina maana hao mameneja hawana hata familia!? Mbona wanakua wanaziabisha sana familia zao!
 
Huyu naye ni MLIPUKAJI tu kama Lowassa. Juzi kajisifu kuwa ujenzi wa barabara ni wa CCM na Serikali yake.Sasa hivi mbona kwenye Mafuriko, kajikalia kimya kama Boga la Halowini?

Usikurupuke.

Jana kwenye taarifa ya habari nimemsikia magufuli akiwaagiza wakandarasi kuhakikisha barabara zilizobomka kwa mvua zirekebishwe haraka sana na aliwashutumu ma engineer wa Iringa kwa kuwa mpaka sasa hawajachukuwa hatua za kukarabati Kitonga wakati fedha zipo.

Wewe ambae hujui kinachoendelea ndio unaona kakaa kimya. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Tanzania has a very very very long way to go as a country!!

Inasikitisha kuona watu na akili zao(I suppose kuwa wana akili!!) kushangilia upuuzi wa waziri kukaripia watendaji hadharani - inasikitisha!!

Mimi nilitegemea hii mentality ya mabwana na watwana itakuwa imefifia au kufa lakini naona hata hao ambao wanajiita magreat thinkers wanachekelea. Hii ni tabia waliyokuwa nayo wakoloni dhidi ya watanganyika - na sikumoja Mr. Nyerere(RIP) amewahi kutamka kuwa tuliwakataa wakoloni si kwasababu ya rangi zao bali kwasababu ya tabia zao za ukandamizaji...

Mr/Dr whatever, acha upumbavu wa kukaripia watu wazima hadharani,acha upubavu wa kudharirisha watendaji wa serikali hata kama wana mapungufu - waite ofisi au waonye kwa barua ecc shame on you Magufuri!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom