Magufuli,jiuzulu kuonyesha Uadilifu

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Natoa wito kwa waziri magufuli kujiuzulu ili kuonyesha uadilifu,na msimamo..hii ni baada ya waziri mkuu kusitisha zoezi la bomoabomoa,kama kweli magufuli anaamini kwenye maamuzi yake ni wakati wa kuonuesha msimamo...
 
Hana ujasiri huo kw akuwa alikuwa natumia sheria feki kutaka kuwabomolea wananchi nyumba zao.
 
Waziri mkuu amesitisha, hajalifuta moja kwa moja, labda kuna technicality kwenye utekelezaji. Kwa mantiki hiyo hatakiwi kujiuzulu mpaka tupate taharifa Serikali imefuta zoezi moja kwa moja.
 
Natoa wito kwa waziri magufuli kujiuzulu ili kuonyesha uadilifu,na msimamo..hii ni baada ya waziri mkuu kusitisha zoezi la bomoabomoa,kama kweli magufuli anaamini kwenye maamuzi yake ni wakati wa kuonuesha msimamo...

wewe unaelewa maana ya kiranja mkuuu?
 
Hana ujasiri huo kw akuwa alikuwa natumia sheria feki kutaka kuwabomolea wananchi nyumba zao.

usisahau pia kuwa magufuli amshalewa sifa ndiyo maana hakujali au alipuuza kuwa sheria ya barabara ya morogoro iko tofauti na barabara zingine hapa nchini.
 
PPM;1738723[SIZE="3" said:
]Waziri mkuu amesitisha, hajalifuta moja kwa moja, labda kuna technicality kwenye utekelezaji. Kwa mantiki hiyo hatakiwi kujiuzulu mpaka tupate taharifa Serikali imefuta zoezi moja kwa moja.

Ni kweli Waziri Mkuu hajasimamisha bomoa bomoa ya nyumba zilizoko katika eneo linalodaiwa kuwa ni hifadhi ya barabara moja kwa moja. Alichofanya Waziri Mkuu kuondoa utata uliosababishwa na Magufuli kuhusu upana wa hifadhi ya barabara. All along upana wa hifadhi ya barabara umekuwa ni Mita 22 nchi nzima. Lakini kuanzia alipopata uwziri wa wizara hiyo mara ya kwanza mwaka 2000 alianzisha utata kuhus upana wa hifadhi hiyo hususna katika eneo la kati ya Ubungo hadi Kiruvia

Waziri Mkuu analenga kuondoa "TOP DOWN ADMINISTRATION" aliyokuwa akipractice Magufuli. Kama ambavyo ni sera za CCM kuwepo kwa Serikali za MItaa ambazo huhudumia Shule za Msingi, Sekondari, Hospitali, Zahanati, miradi ya maji, barabara n.k na Serikali Kuu kwa maana ya Wizara kusimamia uratibu na sera na viwango va huduma zinzotolewa na Serikali za Mitaa.

Hivyo haiwezekani kwa Wizara moja kujitoa katika utaratibu huo kwa utashi wa waziri mmoja tu. Kama ilivyothibitika usimamazi wa hifadhi za barabara ni mtambuka (cross sectoral) hivyo Magufuli anatakiwa kuacha tabia ya kujenga "Serikali ndani ya Serikali"; na azitambue na kuheshimu ngazi za uongozi za Mikoa, Wilaya, Halmashauri za Miji na Wilaya, Tarafa, Kata na Serikali za mitaa. Kwa hali hiyo vitendo alivyofanya mwaka 2001 Magufuli kuagiza kuwekwa kwa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi kati ya Ubungo na Kiruvia bila ya kushirikisha ngazi hizi ulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za utawala bora. Upana halali wa hifadhi ya barabara kuu zote hapa nchini ni Mita 22 badala ya Mita 120.

Kutokea wakati huo wananchi wanaomiliki ardhi na makazi nje ya Mita 22 hadi 120 kila upande wa barabara wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa na wameshindwa kuendeleza ardhi husika hivyo kuongezeka kwa umaskini katika eno hili. Ushahidi wa hali hiyo ni kukosekana kwa huduma kama vle za kibenki, ATM, maduka makubwa n.k kati ya Ubungo hadi Kiruvia tofauti kabis ana maeno mengine zilipopita barabara kuu k.m Barabara ya Bagamoyo, Kilwa n.k

Kulingana na agizo la Waziri Mkuu kuwa Wakuu wa Mikoa wampatie nyumba orodha ya nyumba zinazodaiwa kujengwa kwenye hifadhi ya barabara. Ili Mkuu wa mkoa apate orodha hiyo ni lazima aipate kutoka kwa Mkuu wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya ni lazima aipate kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmshauri/Manispaa. Mkurugenzi naye ni lazima aipate kutoka kwa Afisa Mtendaji Kata na Diwani wa Kata husika. Afisa Mtendaji Kata na Diwani wa Kata ni lazima wapate orodha hiyo kutoka kwa Wenyeviti wa Mitaa, ambao ni lazima wapate orodha hiyo kutoka kwa wajumbe wa mashina, ambao ni lazima waitishe mikutano ya wananchi ili kuorodhesha nyumba zilizoko katika eneo linalodaiwa ni hifadhi ya barabara. Hivyo hapo ndipo wananchi watapata haki yao ya kumiliki eneo ambalo sio hifadhi ya barabara yaani lilioko nje ya Mita 22 kwa mujibu wa sheria ambalo Magufuli aliwapokonya mwaka 2001 kibabe na kwa mabavu.

Ni katika mikutano hiyo sheria anazozitaja Magufuli zitawekwa mezani na wananchi kuweka mezani mamlaka zipi ziliwaleta katika aameno hayo. walipata vipi hati miliki n.k na hivyo mufaka kutapatikana kama eneo nje ya Mita 22 ni hifadhi ya barabara au la? Bila ya playing field kuwa level Magufuli angeendelea kutumia ubabe baa kuburuza watu, taasisi n.k

[/SIZE]
 
Sioni ni kwa nini Magufuli ajiuzuru, aibu ni ya Mizengo kwa kuropoka kwenye halaiki ili apate umaarufu wa kisiasa, hawa mawaziri na waziri wao naona wanaendesha nchi kama genge la vibaka, hakuna hata maelewano baina yao.Magufuli kaza uzi.
 
Magufuli mwenyewe haamini kama aliyokuwa akiyafanya yalikuwa sahihi. Sitegemei ajiuzulu maana naye ni mchumia tumbo tu kama wengine wa aina yake.
 
Tatizo la Tanzania ni kuwa hakuna serikali kwa maana ya serikali. Kila mmoja akishateuliwa nafasi yoyote ile, tayari anajihisi ana mamlaka ya kufanya atakavyo, maamuzi mengi yakiwa ni ya utashi na maslahi binafsi. Serikali kama serikali haina kauli moja, haina msemaji Mkuu wa serikali. Mnakumbuka yalipoanza malumbano ya katiba, Celina alisema nini na Kikwete baadaye kusema nini? Hivyo hivyo kwa kuwalipa Dowans, Ngeleja na Mwanasheria walisemaje, na baadaye Kikwete alisemaje? Hii ni kusema kila mmoja anatoa kauli zake bila ya serikali kuwa na kauli moja, na kiongozi wao hawakemei au kuwawajibisha.
 
Jamani tupende utawala wa sheria. Magufuli yuko sahihi maana nimesafiri kutoka Tanga mjini kwenda Horohoro na watu wamejenga nyumba zao kwa kufuata sheria. Hata toka Kibaha kwenda Chalinze watu wamejenga kwa kufuata sheria. Hata toka Segera hadi Njia Panda ya Himo kuelekea Holili na Arusha watu wamefuata sheria. Sasa hawa jamaa zetu kando kando ya Morogoro Road ambao wamehamia miaka ya 1980's walitumia uwezo wa pesa na kusogea ndani ya hifadhi. Hawastahili vikao bali sheria ichukue mkondo wake. Mizengo Pinda baada ya kusema uongo Bungeni na kupoteza popularity anataka kurudisha heshima kwa mabavu. Toka ameteuliwa PM hajawahi kuonyesha ujasiri zaidi ya kulia kuhusu mauji ya alibno ili asijiuzulu cheo chake cha uwaziri mkuu. Pinda amepinda kwelil kweli. Bravo Magufuli. Usijiuzulu watoto wako watakufa njaa. If you can't beat them just join them.
 
Kidogo unataka kuzungumza jambo linaloingia akilini. Umesema kuwa "Sasa hawa jamaa zetu kando kando ya Morogoro Road ambao wamehamia miaka ya 1980's walitumia uwezo wa Ndio huo upana unaouona huko Tanga kwenda Horohoro, Kibaha kwenda Chalinze n.k?
 
Point ninayoiona hapa ni kuwa Magufuli hajui sheria ya barabara anayoisimamia. Basi hana sifa za kukalia kiti alichopewa.
 
Hoja yangu,si kwamba magufuli amekosea au hajakosea ninalosema ni kuwa kwa pm kusitisha zoezi halali tena kwenye mkutano wa hadhara,ni wazi hamna mawasiliano ya kiserikali,hivyo basi kama anataka kulinda heshima yake anapaswa ajiuzulu,kama alivyowahi kufanya Mtei Edwin alipotofautiana na mkubwa wake wa kazi.
 
Back
Top Bottom