Magufuli awaonya madiwani

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli amewahadharisha madiwani kujiepusha na ufukuzaji holela wa makandarasi. Ametoa kauli hiyo jana bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la Mbunge wa Buchosa, Dk. Charles Tizeba (CCM) aliyetaka kufahamu hatima ya mkandarasi jimboni mwake ambaye Baraza la Madiwani liliazimia kumfukuza. Katika swali la nyongeza, alisema Baraza la Madiwani lilimpa mwezi mmoja ambao umeshapita. Akijibu, Dk. Magufuli alisema, mkandarasi huyo anafanya kazi yake vizuri na kufafanua “Mkandarasi hafukuzwi na madiwani kwani siyo waliomweka. Tujiepushe kufukuza tu makandarasi kama anatimiza mkataba wake”.

HabariLeo
 
Madiwani si ndio waajiri katika Halmashauri? au mkandarasi ndugu yake Magufuri
 
Back
Top Bottom