Magufuli aumbuliwa na Bodi ya Barabara DSM

Hapo nachelewa kuelewa Magufuri kaumbuka vipi? Maana hicho kililikuwa kikao cha mkoa wa DSM na wajumbe wake na hizo ni ajenda zao, sasa kuhumbuka kunatoka wapi?

Mkuu nadhani mwandishi ameshindwa kufikisha ujumbe wake vyema. Ukisoma post huoni Magufuli kaumbuka wapi. Labda ninachokiona ni kwamba issue ya kupandishwa hadhi ya barabara ilishaongelewa lakini hivi karibuni tulisoma kwenye vyombo vya habari waziri magufuli akisema Mnyika hajawahi kuomba barabara zipandishwe hadhi. Labda hapo yaani kwamba hili swala lilishaongelewa kwenye Bodi ya Barabara lakini waziri alisema Mnyika hajawahi kuliongea. Nadhani ndio maana Mnyika akang'ang'ania suala hilo liwe katika yatokanayo kwa sababu ingekuwa ajenda mpya basi ingekuwa kwamba Mnyika ameiongea baada ya sakata la feri. Hayo ni mawazo yangu tu kwa jinsi nilivyosoma hiyo post. Vinginevyo zaidi ya jilo sijaona lingine lenye uhusiano wa heading na content.
 
Waziri wa Ujenzi John Magufuli jana ameumbuka kutokana na tuhuma zake. Hayo yametokea katika mkutano wa bodi ya barabara katika mkoa wa Dar es salaam uliofanyika mnazi mmoja.

Mara baada ya Mkuu wa Mkoa Mecky Sadiq kufungua mkutano huo mbele ya waandishi wa habari, alimkaribisha katibu tawala wa mkoa huo (jina halijapatikana) kusoma kuanza ajenda ya kuthibitisha muktasari wa mkutano uliopita.

Mbunge wa Ubungo, aliingilia kati na kutaka kwanza kikao kithibitishe ajenda na kutoa tuhuma kwamba ajenda moja imeingizwa kinyemela. Mnyika aliitaja ajenda hiyo kuwa ni kupokea mapendekezo ya kupandisha hadhi barabara za Mkoa wa Dar es salaam ambayo alieleza kuwa ikijadiliwa itaeleweka kuwa ndio sasa mkoa umeanza kushughulikia suala hilo.

Mkuu wa Mkoa alitetea uamuzi huo akidai kwamba kuingizwa kwa ajenda hiyo kutaonyesha kwamba wabunge, madiwani na watendaji wa mkoa wa Dar es salaam wamelipa uzito zaidi suala hilo kufuatia kauli ya Waziri Magufuli.

Hata hivyo Mnyika alisisitiza suala hilo lijitokeze kwenye yatokanayo ili badala ya kujadili mapendekezo taarifa itolewe kuhusu utekelezaji wa serikali baada ya mapendekezo kuwasilishwa kwa Wizara ya Ujenzi kwa nyakati mbalimbali.
Msimamo huo uliungwa mkono na Meya wa Kinondoni Yusuph Mwenda na kumlazimu Mkuu wa Mkoa ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano na kukubali kuiondoa ajenda hiyo ili ijadiliwe kama sehemu ya yatokanayo na mkutano uliopita wa bodi hiyo ya barabara.

Katika ajenda hiyo ya yatokanayo suala hilo la kupandishwa kwa hadhi ya barabara za Mkoa wa Dar es salaam lilijadiliwa na wachangiaji wengi zaidi huku wajumbe wakielekea kukubaliana kwenye sehemu kubwa ya maoni na wakizungumza kwa hisia kali.


Wa kwanza kuzungumzia ajenda hiyo kwa mara nyingine tena alikuwa ni mbunge wa Ubungo ambaye alidai kwamba tayari bodi ya barabara ilishapeleka mapendekezo ya kupandishwa hadhi kwa barabara za Dar es salaam katika mikutano ya mwezi Februari na Oktoba 2011 lakini Waziri wa Ujenzi hajatoa majibu yoyote hali ambayo imechelewesha ujenzi wa barabara za kupunguza foleni.


Mnyika alisema kwamba suala hilo limesababisha Dar es salaam kutokutengewa Fedha za kutosha za ujenzi wa barabara, na akataka mwakilishi wa TANROADS na Wizara ya Ujenzi katika kikao hicho kueleza iwapo ni ukweli kwamba serikali inafedha za barabara kwa ajili ya Dar es salaam ambazo zimekaa bila kutumiwa kama alivyodai Waziri Magufuli. Mnyika alimalizia kwa kutaka vigezo vya kupandisha hadhi barabara vya mwaka 2009 vibadilishwe ili kuwe na vigezo maalum kwa ajili ya Dar es salaam ambavyo vitazingatia umuhimu wa jiji kitaifa na hali mbaya ya foleni ilivyo hivi sasa.


Wapili kuzungumzia hoja hiyo alikuwa Mbunge wa Kigamboni Dr Ndugulile ambaye alisema kwamba kama Serikali kupitia kwa Waziri wa Ujenzi imesema kwamba ina Fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Dar es salaam ni kwanini badala ya kuongeza hadhi ya barabara nyingi zaidi imeleta pendekezo jipya la kushusha hadhi za barabara na kuzirejesha kwa Manispaa. Dr Ndugulile alipinga mpango huo na badala yake alitaka Wizara ya Ujenzi ipandishe hadhi barabara zilizoombewa kwa muda mrefu kupandishwa hadhi.


Mwigine aliyezungumzia jambo hilo kwa ukali ni kiongozi wa chama cha wasafirishaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Mabruk alinukuu gazeti la habari leo ambalo lilomnukuu Waziri Magufuli akieleza kuwa Wizara ya Ujenzi iko tayari kuondoa tatizo la foleni Dar es salaam isipokuwa Manispaa za Jiji la Dar es salaam zinangangania barabara hizo na kutaka maelezo ya TANROADS na Mhandisi wa Mkoa. Katika maelezo yao waataalamu walioshiriki kikao hicho walieleza kuwa kikwazo cha kupandisha hadhi barabara nyingi zilizoko chini ya Manispaa kwa sasa ni vigezo. Mabruk aliingilia kati na kudai kuwa kama kikwazo ni vigezo ambavyo vimetengenezwa na Waziri, kwanini Waziri huyo huyo anazisingizia Manispaa badala ya kufanya kazi inavyostahili.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni alisisitiza kwa Manispaa hazijawahi kuwa kikwazo na kuitaka Wizara ya Ujenzi iongeze fungu kwa ajili ya ujenzi wa barabara, sisi ndio tunaochangia kwa zaidi ya asilimia 70 kwenye Fedha zinazotokana na kodi ya mafuta lakini barabara zetu zinatengewa Fedha kidogo. Serikali inafanya kama vile Dar es salaam tunapaswa kupiga magoti na kuomba, wakati Wizara ya Ujenzi inapaswa kufanya kazi ya kuleta maendeleo na kutoa mgawo mkubwa kwa barabara zetu kwa kuwa ni haki yetu., alisema Mwenda.


Msimamo huo wa wajumbe ulifanya Mwenyekiti wa Mkutano aombe kwamba ajenda hiyo isiendelee na badala yake kuundwe kamati maalum ya kuonana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Waziri Magufuli kuhusu barabara za Dar es salaam kupandishwa hadhi na kuongezewa Fedha za ujenzi. Pia, mkuu wa mkoa alisema kwamba hoja isiwe kiwango cha mapato kinachokusanywa toka Dar es salaam bali iwe ni umuhimu wa barabara za Dar es salaam na jiji lenyewe kwa kuwa zinatumiwa na wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali nchini.


Kufuatia kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa, Mnyika alitaka kwamba hoja kuu iwe ni hasara ya kifedha na athari za kiuchumi kutokana na matatizo ya msongamano wa magari, na kutaka wataalamu waandae hoja yenye kuonyesha tija ambayo nchi itapata iwapo barabara zote muhimu za kupunguza foleni zinapandishwa hadhi na kujengwa kwa pamoja kwa kipindi kifupi inavyowezekana.


Ajenda nyingine iliyovuta hisia za wachangiaji ni taarifa ya utekelezaji ya miradi ya barabara katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ambapo wajumbe walihoji ufanisi wa kazi zinazofanywa na wakandarasi mbalimbali, kupungua kwa utawala wa sheria katika masuala ya barabara hali ambayo inachangia katika ongezeko la foleni na ajali na mpango mpya wa njia moja katika barabara za katikati ya mji ambao utazinduliwa karibuni baada ya kufanyika kwa mkutano na wadau.
,,,,,;,,,, kilicho muumbuwa mh pombe ni kipi nadhani wewe ndo unau umbuka sasa ,,,,,;,,,,
 
Mkuu nadhani mwandishi ameshindwa kufikisha ujumbe wake vyema. Ukisoma post huoni Magufuli kaumbuka wapi. Labda ninachokiona ni kwamba issue ya kupandishwa hadhi ya barabara ilishaongelewa lakini hivi karibuni tulisoma kwenye vyombo vya habari waziri magufuli akisema Mnyika hajawahi kuomba barabara zipandishwe hadhi. Labda hapo yaani kwamba hili swala lilishaongelewa kwenye Bodi ya Barabara lakini waziri alisema Mnyika hajawahi kuliongea. Nadhani ndio maana Mnyika akang'ang'ania suala hilo liwe katika yatokanayo kwa sababu ingekuwa ajenda mpya basi ingekuwa kwamba Mnyika ameiongea baada ya sakata la feri. Hayo ni mawazo yangu tu kwa jinsi nilivyosoma hiyo post. Vinginevyo zaidi ya jilo sijaona lingine lenye uhusiano wa heading na content.


It sounds more politicised.......
 
Mwandishi wa mada hii ulikuwapo katika kikao hicho au ulikuwa katibu wa kikao hicho.

Kweli Tz hakuna maadili ya utawala na sheria za kazi. Mmambo ya vikaoni mpaka kwenye mitandao.

kazi ipo.
​acha unafiki wewe mwarabu wa Libya nyie ndo huwa mnakua wa1 kutaka kujua yaliyojiri ndani ya serikali.
 
Kwa mwenye hekima na busara kukaa kimya ni busara ili ujipange kumbuka hawa watu wana jazba na issue ya kigamboni ambayo ni latest.Big up Magufuri kwa kuwachunia ili wakileta hoja zao formally kwako ujue namna ya kuzipangua.
Fidia baada ya kuzipandisha hadhi izo barabara ela jamani ipo?wakati mishahara tuu issue.
Imagine uhuru road inapanda hadhi iyo bomoa bomoa itawatokea puani hao hao wanaotakka ipandishwe hadhi
 
Pia tusisahau kuwa Magufuli alipinga sana mradi wa daraja la kigamboni

ushahidi ninao nipeni 1 hr hivi nitamwaga mboga zote

NUiQb.gif

mwaga mambo mkuu still loading...
 
Kwa mwenye hekima na busara kukaa kimya ni busara ili ujipange kumbuka hawa watu wana jazba na issue ya kigamboni ambayo ni latest.Big up Magufuri kwa kuwachunia ili wakileta hoja zao formally kwako ujue namna ya kuzipangua.
Fidia baada ya kuzipandisha hadhi izo barabara ela jamani ipo?wakati mishahara tuu issue.
Imagine uhuru road inapanda hadhi iyo bomoa bomoa itawatokea puani hao hao wanaotakka ipandishwe hadhi



Waziri Magufuli aliongeza kuwa, Jiji la Dar es Salaam lina jumla ya barabara zenye urefu wa km 560, lakini baadhi hazijapandishwa hadhi na kwamba alifikiri wabunge wake wangeungana wakaandaa mapendekezo ya kupandishwa hadhi za barabara hizo ili ziweze kusimamiwa na serikali kuu.
Waziri huyo alisema serikali kwa mwaka huu imetenga sh bilioni 400 kwa ajili ya barabara zake za Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo alitegemea zingetumika vema katika barabara ambazo wabunge wangependekeza zifanyiwe kazi.

Chanzo: Nasema Simuombi mtu radhi Ng'oo! | darhotwire
 
Mimi Nafurahi sana nikiona Haya yanajadiliwa!! Ila ikumbukwe kuwa barabara Nyingi zipo under capacity!! Angalia pale Manzese Kuna foleni Kubwa inaanzia Mitaa ya Kagera!!, Similarly Tegeta, and Many more Places!! Ubungo Usiku Kuanzia saa Tatu daladala zinaziba njia kwa kutoingia Stand!! Je haya nayo yanahitaji fedha za kigeni au Just Law Enforcers!!
Jamani tuwe Tunafikiria Kuboresha Barabara na huku Yale ambayo Yapo ndani ya uwezo wetu nayo Tuyafanyie kazi!! Hayahitaji Wafadhili Haya!!
 
Kama ambavyo mnaomchukia mnapaswa kuona mazuri anayoyafanya kwa NCHI hii. Binadamu aliyekamilika siku zote ni pande mbili. Baadhi yetu tunashabikia utendaji wake, uthubutu wake na ujasiri wake. Nimeisoma hiyo Post ya kwanza hapo juu. Mnyika kashikwa pabaya.

Kwa swala hili mpaka sasa sina imani na Mbunge wa UBUNGO, Mbunge wa KIGAMBONI na mbunge wa TEMEKE
 
Ni bora barabara zipandishwe Hadhi na kupunguza fungu la hela Huko Tamisemi, kwani hawa ndio Kikwazo Kikubwa kwani wamejenga Barabara Nyingi ambazo asilimia Kubwa Hazina Viwango na huwa hazina Usimamizi Wowote na Huwa Zinabomoka wakati Mkandarasi akiwa bado site!! Nina Mfano wa barabara Chache
1. Barabara ya shekilango Under Hari Sigh!! Barabara imebomoka kabla ya Ujenzi Kukamilika, hasa kwenye Vituo vya kupaki Mabasi
2. Barabara ya Kigogo First Inn via Mburahati to Kagera!! Hii barabara ni Kichefu Chefu!! Kwani ujenzi wake ulikuwa wa kienyeji sana!! Mkandarasi alikuwa huyu huyu Hari Sigh na alikuwa anaweka udongo Mzuri juu ya karatasi za Nailon!! in principle Hakufanya any site Clarence Hivyo barabara inafumuka sasa!! in priciple ujenzi wa hii barabara Gharama yake ilikuwa more than 9 bilions.
3. Barabara ya Sinza Mwika Makaburini!! Same contractor Rubbish work
4 And Many More!!
 
Mwandishi wa mada hii ulikuwapo katika kikao hicho au ulikuwa katibu wa kikao hicho.

Kweli Tz hakuna maadili ya utawala na sheria za kazi. Mmambo ya vikaoni mpaka kwenye mitandao.

kazi ipo.

Hivi wewe ni mshabiki wa magufuri?
 
Sina la kuchangia hapa, kwanza maandishi yanajikanganya na pili naona ni yale yale ya "kuelekea 2015".

Ngoja nirudie kusoma michango ya wanabodi.
 
Mimi naona hili suala la upandishaji hadhi na upunguzaji ni kama porojo tu, kama kweli hawa viongozi wanatafuta njia ya kupunguza foleni za ajabu, basi ni kufikiria vipi wataweka fly-over kwenye barabara kuu na kusahau masuala ya mataa ya kuongozea magari, hiyo itaweza kusaidia kupunguza foleni kuliko huo mradi au porojo za kupandisha na kushusha hadhi barabara, ukijumlisha na ile story ya mabasi yaendayo kasi. Wenzangu tufikirie foleni ya ubungo ilivyo, naamini kama kungekuwa na barabara au daraja la juu au chini linaloweza kupitisha magari bila ya kusubiri mataa, mnadhani kungekuwa na biashara ya foleni pale, na kuendelea na mradi kwenye mataa kwengineko. Ni maoni tu,

Very simple! Mimi sielewi hawa wasomi wetu wanaishi wapi? Wameishia kuijenga mandels kwa mabilioni wakati hakuna lolote waliloongeza zaidi ya foleni zaidi na kupunguza upana wa barabara na kujenga mahandaki wayaitayo mitaro. Nimetembea nchi nyingi duniani lakini sijawahi kuona mitaro kama hiyo. Wazungu wanavunjika mbavu kwa kutucheka! Eti magufuli!
 
huyu ndiye rais wenu wa ccm ajaye!! mkurupukaji hivi? ajibu kwanza hoja za Mnyika si kutuletea ubabaishaji.
 
Back
Top Bottom