Magufuli atuma salamu kwa Kikwete na CCM

Ukitaka kujua barabara inatengenezwa na wa tz ni rahisi sana, kwa mfano wanafanya marekebisho, watachimba sehemu zilizoharibika ili kuweka lami, wakishachimba wataacha mashimo kwa miezi miwili au zaidi, hakuna alama zozote. Baada ya miezi miwili au zaidi, watakuja na mashine zao wataweka mabango mekundu kila mahali na kusababisha foleni kubwaaa kwa wiki nzima au zaidi, ndio kazi ikamilike. Kazi ndogo kero kubwa, kama ni mchina hiyo kazi yote angemaliza kwa siku mbili tu.

Arusha kuna barabara nyingi za magari lakini hizi barabara ni mbovu kupita maelezo, watu wengi wanang'ang'ania kupita barabara kuu ingawa na yenyewe ni nyembamba sana. Hakuna vituo vya daladala, vipanya vinapenya pembezoni mwa barabara na kusimama popote, wewe unayefuata sheria za barabara unakuwa kama mshamba, kulia kwako msururu wa pikipiki za wajasiria mali, kushoto umebanwa na dadalada kama nne hivi.

OMBI KWA MAGUFULI
Kuna barabara ya vumbi inayotoka NMC hadi mjini, mwisho wa hii barabara kuna Daraja linatengenezwa, limeshachukua zaidi ya miezi minne hatuoni kinachoendelea, kuna mabango yamerembwa yanasema kuna ujenzi unaendelea. Muheshimiwa Pombe Magufuli naomba uwaamshe wajenzi wa hili daraja wamalize kazi, pia wachonge hiyo barabara kidogo ili iweze kupitika. Nahakika ni ule usingizi wetu wa kawaida tu, embu waamshe wamalize kazi. Au wape tenda wachina ili mambo yaende. Hii barabara ni muhimu sana kwa wakazi wa Arusha kwa sababu itapunguza msongamano. Magari mengi ya private yatapita kwenye hii barabara na itapunguza msongamano kwa kiasi kikubwa.
 
Aliposema kuwa anataka kubomoa nyumba zote zilizopo kwenye hifadhi ya barabara alipingwa viokali tena na serikali iliyomchagua kuwa Waziri wa Miundombinu. Kwa ujumla alionekana kuwa ni mbabe na asiye na huruma na wananchi.

Aliposema kuwa atataka kuondoa takataka zote za matangazo barabaraniakaonekana pia kuwa atapoteza mapato ya halmashauri.

Nimekuwa nikitafakari hayo mamabo mawili na kugundua kuwa Magufuli uwezo wake ni karne kama tatu zijazo. Na nivigumu sana kuweza kumuelewa kama mtu umezoea kukaa katika mazingira mabovu.

Kwa bahati nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya nikadhani kuwa wapo organized sana kwa kuwa wapo Ulaya. Nimebahatika pia kutembelea nchi kadhaa za Afrika haswa zile zilizopo Kusni mwa Afrika na kugundua kuwa kwa kweli Tanzania nchi yangu inachafuliwa sana na hayo mambo mawili.

Miji yetu imekuwa michafu kwa kuwa taratibu zinashindwa kufuatwa. Ninachoomba wadau wa JF mshauri viongozi wetu katika kutekeleza maagizo ya Magufuli mabadiliko makubwa na uzuri wa miji yetu itaanza kuonekana.

Naomba kuwasilisha
 
Ni bora we umeliona hilo maana mi nilikuwa nafakar wanaompinga sielewi wanawaza nn. Lakin mwishowe nikatambua wanaompinga wengi n type za magamba ambao hawaoni mbele. Wao ni kuwaza ushuru tu wa leo. Magufuri kwa uelewa wake yampasa ahamie tu cdm.
 
ulisema tar 13 july ukabithiwe barabara ya A/mashariki, we mwanaume bana, ndio wamemaliza jana usiku, tungekuwa na mawaziri watatu zaidi kama wewe watanzania tungenona, yaani waziri wa nishati na madini, mali asili na utalii pamoja na elimu, hivi JK huwezi kutamka mara moja huyu mwanaume akazishika hizo wizara miezi 6 halafu awarudishie wahusika? just thinking aloud, pongezi sana bwana Magufuli
 
Anafaa, lakini alitia doa pale alipogawa nyumba za serikali tena kwa mdogo wake kumtoa shule, kumwajili ili awe na vigezo halafu akampa nyumba na akarudi shuleni. Hapo alinitia doa kubwa, otherwise he is good. JK mpe hizo wizara mbili tuone matokeo yake. JK, just try.
 
kweli matatizo ya nchi yetu yanasababiswa na viongozi dhaifu tulionao. Ifike wakati raisi aache kuwapa watu zawadi za vyeo wasivyoviweza la sivyo tutaendelea kuumia sana nchii hii
 
Huyu jamaa alitaka kuondoa foleni Dar wakamzingua mimi naona ****** ajiuzulu
 
Pamoja na madhaifu yake, lakini Magufuli ni mzuri bana. He is the best in our current government, including the presda.
 
Watu kama hawa katika jamii huwa hawakosekani..japo huwa wanakua wachache sana! Shida tuliyonayo ni upendeleo kwa watu wasiofanya kazi na walio ki maslahi zaidi..! Big Magufuli
 
Bungeni leo asubuhi mbunge wa Kinondöni Mh: Idd Azan amemuuliza Waziri mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo Ni kwa nini agizo lililotolewa na Rais kikwete kuhusu kubomolewa kwa uzio pale viwanja vya jangwani halijatekelezwa wakati Mh. MAGUFULI anapotoa agizo kwa mfano kubomoa majengo ya wavamizi wa hifadhi ya barabara hutekelezwa mara moja tofauti na Agizo likitolewa na rais, Ni kweli Jk ni legelege? Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu kwenye wekundu hapo ni kweli maneno yhayo yametamkwa na Ndg. Idd Azzan au unamuwekea maneno kinywani?
 
Back
Top Bottom