Magufuli ameukinai uwaziri..sasa apumzike

Status
Not open for further replies.
Watanzania mnataka waziri wa aina gani?Pana ubaya wowote waziri akisoa uwajibikaji mmbovu waziri mwenzie?Kukosoa ni kukumbusha sioni ubaya katika hili labda lile la wananchi kitakiwa kupiga mbizi kama hawana pesa ya kulipia kivuko.

Msingi mmojawapo wa uongozi bora ni kuepuka kusemana viongozi kwa viongozi hadharani wakati mna nafasi ya kukutana kwenye vikao vyenu. This is one of 101 rules of a good leader!
 
kuchapa kazi ni quantity ama na quality.tembea mandela express highway siku ya mvua utaona kichekesho kuwa maji yanajaa barabarani badala ya kujaa kwenye mitaro mikubwa miwili,hii aliifungua waziri mchapakazi?msisahau alivyobariki mauzo ya nyumba za serikali hadi za ma rpc!na yeye akajipatia ka nyumba kadogo tu hapo ubungo kuhifadhi kanyumba kadogo bila shaka na waliohoji waliambiwa wana wivu wa kike ama kitu kama hiyo
kwa hiyo uchapa kazi ukitazamwa kwa jicho la tofauti waweza kuwa ubabaishaji na kutafuta umaarufu wa reja reja

Dr. Magufuli ana miaka 18 serikalini kama waziri ana nyumba ndogo ubungo kwa mujibu wa maelezo yako mwenyewe, huyo bwana Maige ana miaka 4 kazini nyumba ya milioni 700 na malizingine ambazo hazijandikwa humu sasa hapo na mtendaji mzuri ni nani? Magufuli hata akisema arudi jimboni mwake tutamfuata tu kwa kazi zake zinaonekana kwa wenye macho wote lakini vipofu kama wewe hamuwezi na kamwe hamtaziona kazi zake. lililobaki kuchimba wenzenu tu. Kwa taarifa yako mwajiri wake anamkubali na jioni ya leo atakuwamo kwenye baraza jipya kajinyonge na roho yako mbaya kama nyoka
 
Na kwa taarifa zilizotoka chini ya carpet, Magufuli anakula wizara ya Ngeleja!! Professor anapewa unaibu.
 
Pamoja na John Obhwarwa Magufuli kuonekana kama waziri pekee wa ccm mchapakazi,lakini kuna kitu kinachomfanya uchapakazi wake uonekane sio lolote.kitu hicho ni dharau.huyu bwana ana dharau ya hali ya juu.sijui kwa kuwa amekuwa waziri kwa muda mrefu sana takribani miaka 17 au sijui kwa kuwa tunamsifu sana ndo maana anakuwa hivi sipati jibu.juzi wakati naangalia TB-CCM1 wakati huyu bwana akitembelea barabara zinazojengwa dar alikaripia vikali mamlaka zingine za serikali zinazokwamisha ujenzi huo zikiwemo tanesco na dawasco.akamwagiza mfugale afuatilie mamlaka hizo na kama wakisuasua ataonana na mawaziri wa mashirika hayo..na kama hiyo haitoshi akasema kama mawaziri hao pia watasuasua ataenda kwa JK moja kwa moja kuwashtakia...lol!!niliduwaa!!

haya ni mambo ya kuongelea hukoo kwenye vikao vyao vya ndani (inter-ministrial meetings) sio kwenye vyombo vya habari bwana magufuli.sasa kama kuna waziri mhusika alikuwa anaangalia taarifa ile ya habari unadhani atakupa ushirikiano?atakukwepa tu.mimi nadhani this is too much for magufuli.anaropoka tu hadharani.hana busara hata kidogo.pamoja na uchapa kazi wake lakini bila busara ktk kutekeleza majukumu yake ni kazi bure. ndio kuna mambo ya sheria zaidi,lakini kuna mengine hayahusu sheria.atulize jazba.achape kazi.lakini pia kuna kitu najiuliza,kuugua kwa huyu bwana malaria ya mara kwa mara ndo yamemfanya hivi?yamechukua sehemu ya ufahamu wake?mi nadhani akili zake zimezidi sana kiasi kwamba anaonekana kuchanganyikiwa...

Apumzike sasa.aachie wengine waongoze.pamoja na uchapa kazi wake lakini hafai kuwa kiongozi.

hv unapenda sana suala la dakika 2 had waunde kamati na kukaa vkoa kulijadil? Kwa nini tanesco wasitoe nguzo zao ili barabara ijingwe? Kwa nin dawasco wasitoe mabomba yao kwenye njia? Acha hzo mwana
 
sasaivi magufuli fanya kimyakimya kama maige,Ngereja,Mkullo, Nundu. Hii nchi inawananchi wa ajabu sana ya mtu badala ya kuwachoka mafisadi anawachoka wachapa kazi..hii itakua laana sio hivihivi.

IDAWA NDUGU YANGU HATA MIMI NIMEKUBALI MAANA KWA YOOOOOOOTE ANAYOFANYA Dr.MAGUFULI KWA WAJINGA HAWA INAONEKANA WORK DONE IS EQUAL TO 0 HIVI WANATAKA MALAIKA ATOKE MBINGUNI AWAFANYE KAZI? HATA YEYE CHA MOTO ATAKIONA TU, MIMI NAONA MAGUFULI ANGEFANYA KAZI KWA VIBOKO KAMA MJERUMANI WAKATI WA UJENZI WA RELI YA KATI MAANA MPAKA LEO WAZEE WA ENZI ZILE WANAKUMBUKA KAZI ZA MDACHI. NI WAZIRI GANI KATIKA HISTORIA YA NCHI HII ALISHAKATAA KUPOKEA BARABARA TENA ILIYOJENGWA KWA MSAADA WA JAPANI? MPKA JAPANI WENYEWE WALIOMBA RADHI!!!!!! LEO MBURUKENGE HAWA WANAMPONDA ETI HAJUI KAZI MIMI NASHINDWA KUJIZUIA KUKASIRIKA KWANI MAMBO YA MAGUFULI YAKO WAZI SANA KILA MTU ANAONA NI MPUMBAVU TU NA KIPOFU NDIYE HAONI KAZI ZA MAGUFULI
 
Pamoja na John Obhwarwa Magufuli kuonekana kama waziri pekee wa ccm mchapakazi,lakini kuna kitu kinachomfanya uchapakazi wake uonekane sio lolote.kitu hicho ni dharau.huyu bwana ana dharau ya hali ya juu.sijui kwa kuwa amekuwa waziri kwa muda mrefu sana takribani miaka 17 au sijui kwa kuwa tunamsifu sana ndo maana anakuwa hivi sipati jibu.juzi wakati naangalia TB-CCM1 wakati huyu bwana akitembelea barabara zinazojengwa dar alikaripia vikali mamlaka zingine za serikali zinazokwamisha ujenzi huo zikiwemo tanesco na dawasco.akamwagiza mfugale afuatilie mamlaka hizo na kama wakisuasua ataonana na mawaziri wa mashirika hayo..na kama hiyo haitoshi akasema kama mawaziri hao pia watasuasua ataenda kwa JK moja kwa moja kuwashtakia...lol!!niliduwaa!!

Apumzike sasa.aachie wengine waongoze.pamoja na uchapa kazi wake lakini hafai kuwa kiongozi.

ukiachilia mbali mapungu yake madogo asilimia kubwa magufuli ni mchapakazi....yeye siyo malaika na kila binadamu anapungufu yake....let take advantage of his strength....bila watu kama aina ya magufuli hii inchi itaoza na urasimu usiowalazima
 
TANESCO na DAWASCO hawajajibu? Najua tu wana majibu tena mabaya!

twende mbele kisha turudi nyuma......hivi kweli bomba la maji safi, lenye diamemter ya inchi 18 na zaidi linaweza kuhamishwa kwa siku saba?

Japo naichukia TANESCO lakini nimefurahia majibu ya mkuu wa uhusiano wa TANESCO. pamoja na mambo mengine amesema wanashindwa kuhamisha nguzo kwa sababu karibu na barabara kuna nyumba na vibanda vya watu wanaopaswa kuhama/kuhamishwa si kazi ya TANESCO kuwahamisha au kubomoa hizo nyumba........Ngoma inarudi kwa TANROAD na wizara yake.....kwa hili nadhani Magufuli amekosea.
 
Sidhani kama watanzania wanamtafuta baba mtakatifu, au kuhani au sheikh. Bali wanataka kiongozi licha ya udhaifu wake wa kibinadamu bado anafanya kazi na inaonekana.

Magufuli anaweza asiwe kwenye safu ya watakatifu, lakini huyu bwana akisema kitu kinafanyika, na hii ni kwa sababu anafuatilia na kusimamia anachosema. Hatutaki watu wanaosema moja kumbe waliamaanisha mbili.

SASA NAPUMUA KUMBE WENYE MACHO TUKO WENGI SAFI SANA FJM WAAMBIE HAO VILAZA WANAOKUMBATIA MAFISADI WANAACHA WATENDAJI DR. Kawambwa alishindwa kumuondoa Mkurugenzi wa Tanroad pale makau makuu ya Wizara ya Ujenzi lakini jamaa ile kuingia tu ndipo alipoanzia Mkurugenzi kule lakini vipofu hawaoni hili haya Japani walitujengea barabara ya mbagala kwa msaada wa fedha kutoka Japani kulekule Jamaa aliikataa kuipokea na Japani pamoja na kuwa waliijenga kwa msaada lakini waliimba radhi Tanzania na kuahidi kujenga upya barabara hiyo lakini kwa vipofu bado hawaoni tu ni nani katika historia ya nchi hii alishafanya hivyo kama siyo Dr. John pekee?
 
Msingi mmojawapo wa uongozi bora ni kuepuka kusemana viongozi kwa viongozi hadharani wakati mna nafasi ya kukutana kwenye vikao vyenu. This is one of 101 rules of a good leader!

Kosa lile lile nililolisema katika kuchangia kwangu ndilo ulilolirudia hapa.Hizi nafasi unazosema kuwa mkutane ktk vikao vyenu ndio huko huko mtafichiana siri.Yapo mambo yakisemwa hadharani(ktk jamii)yanasaidia sana.Kumbuka ufisadi wote uliokwisha kufanyika nchi hii na ukagundulika lazima ulisemwa hadharani.Haya mambo ya kishikaji tuyaache kabisa hasa katika utendaji wa jambo fulani ktk nchi yetu
 
Pamoja na John Obhwarwa Magufuli kuonekana kama waziri pekee wa ccm mchapakazi,lakini kuna kitu kinachomfanya uchapakazi wake uonekane sio lolote.kitu hicho ni dharau.huyu bwana ana dharau ya hali ya juu.sijui kwa kuwa amekuwa waziri kwa muda mrefu sana takribani miaka 17 au sijui kwa kuwa tunamsifu sana ndo maana anakuwa hivi sipati jibu.juzi wakati naangalia TB-CCM1 wakati huyu bwana akitembelea barabara zinazojengwa dar alikaripia vikali mamlaka zingine za serikali zinazokwamisha ujenzi huo zikiwemo tanesco na dawasco.akamwagiza mfugale afuatilie mamlaka hizo na kama wakisuasua ataonana na mawaziri wa mashirika hayo..na kama hiyo haitoshi akasema kama mawaziri hao pia watasuasua ataenda kwa JK moja kwa moja kuwashtakia...lol!!niliduwaa!!

haya ni mambo ya kuongelea hukoo kwenye vikao vyao vya ndani (inter-ministrial meetings) sio kwenye vyombo vya habari bwana magufuli.sasa kama kuna waziri mhusika alikuwa anaangalia taarifa ile ya habari unadhani atakupa ushirikiano?atakukwepa tu.mimi nadhani this is too much for magufuli.anaropoka tu hadharani.hana busara hata kidogo.pamoja na uchapa kazi wake lakini bila busara ktk kutekeleza majukumu yake ni kazi bure. ndio kuna mambo ya sheria zaidi,lakini kuna mengine hayahusu sheria.atulize jazba.achape kazi.lakini pia kuna kitu najiuliza,kuugua kwa huyu bwana malaria ya mara kwa mara ndo yamemfanya hivi?yamechukua sehemu ya ufahamu wake?mi nadhani akili zake zimezidi sana kiasi kwamba anaonekana kuchanganyikiwa...

Apumzike sasa.aachie wengine waongoze.pamoja na uchapa kazi wake lakini hafai kuwa kiongozi.

Unamlaumu bure Tanzania ya sasa inahitaji mawaziri wa akina Magufuli au zaidi yake. Wewe unategemea km lijitu lingine limepewa mamlaka kusimamia sehemu halafu linamkwamisha afanyeje? Vinogozi wengi hawafanyi kazi na kwa vile issues nyingi ni crosscutting hata km wewe ni mchapakazi unafika mahala unakwama. Magufuli alikuwa ni waziri mzuri lakini ubora wake umepunguzwa na serikali ya Kikwete. Mifano ni mingi na iko wazi km ni mfuatiliaji utanielewa. Ningekuwa na mamlaka ya uteuzi ningemuweka kwenye wizara ya kusimamia na kutefuta fedha huenda angeongeza ukali na ubunifu na kuongeza wigo wa mapato badala ya kuendelea kutegemea kodi za wafanyakazi kwa asilimia kubwa.
 
Naona upo sahihi, lakini nahisi unaprejudice na Magufuli ambazo zinakusukuma kuichukia kazi yake ya haki. Magufuli si malaika, lakini wote ni mashahidi kwamba Magufuli anafanya kazi nzuri na isio acha maswali.

Unapomtukana huyu mzee kwa kusimamia kwa nguvu utekelezaji wa malengo yake kwa manufaa ya umma unanifnya masikio kope ziwashe ninapokusoma.

Kuchukia watu wanaosimamia kazi na kutekeleza majukumu yao kwa bidii ni kitu cha kawaida Tanzania. Hata huku maofisini, ukifanya kazi zako kwa bidii, utaambiwa unajipendekeza, na utachukiwa. Ukitaka watu wakupendeze we fanya uzembe, masyala na ufisadi kazini ndo utaonekana mtu wa maana wakati hovyo.

Magesa, jipime na ikiwezekana u-edit thread yako. Usipo fanya hivyo utaaibika kwani Maguli si muda mrefu atakuthibitishia kwamba he is the of the leader needed by Tanzanians.

Pamoja na John Obhwarwa Magufuli kuonekana kama waziri pekee wa ccm mchapakazi,lakini kuna kitu kinachomfanya uchapakazi wake uonekane sio lolote.kitu hicho ni dharau.huyu bwana ana dharau ya hali ya juu.sijui kwa kuwa amekuwa waziri kwa muda mrefu sana takribani miaka 17 au sijui kwa kuwa tunamsifu sana ndo maana anakuwa hivi sipati jibu.juzi wakati naangalia TB-CCM1 wakati huyu bwana akitembelea barabara zinazojengwa dar alikaripia vikali mamlaka zingine za serikali zinazokwamisha ujenzi huo zikiwemo tanesco na dawasco.akamwagiza mfugale afuatilie mamlaka hizo na kama wakisuasua ataonana na mawaziri wa mashirika hayo..na kama hiyo haitoshi akasema kama mawaziri hao pia watasuasua ataenda kwa JK moja kwa moja kuwashtakia...lol!!niliduwaa!!

haya ni mambo ya kuongelea hukoo kwenye vikao vyao vya ndani (inter-ministrial meetings) sio kwenye vyombo vya habari bwana magufuli.sasa kama kuna waziri mhusika alikuwa anaangalia taarifa ile ya habari unadhani atakupa ushirikiano?atakukwepa tu.mimi nadhani this is too much for magufuli.anaropoka tu hadharani.hana busara hata kidogo.pamoja na uchapa kazi wake lakini bila busara ktk kutekeleza majukumu yake ni kazi bure. ndio kuna mambo ya sheria zaidi,lakini kuna mengine hayahusu sheria.atulize jazba.achape kazi.lakini pia kuna kitu najiuliza,kuugua kwa huyu bwana malaria ya mara kwa mara ndo yamemfanya hivi?yamechukua sehemu ya ufahamu wake?mi nadhani akili zake zimezidi sana kiasi kwamba anaonekana kuchanganyikiwa...

Apumzike sasa.aachie wengine waongoze.pamoja na uchapa kazi wake lakini hafai kuwa kiongozi.
 
Pengine alishaongea na akina Mkullo in private kuhusu alicho ongea hadharani na akina mkullo hawakutekeleza, mtajuaje? Mbona Pinda lishaendaga jimboni kwake Chato na kumnanga, na ikaonekana sawa? Mbona muungano wa wabunge wa Dar pamoja na Mameya nao walienda kumlaani kwenye vyombo vya habari juu ya nauli ya daladala, badala ya kutumia vikao husika?

Akiwa waziri wa ujenzi mbona alirudisha mali nyingi za umma serikalini, akatishiwa kuuwawa na wenzie. Akiwa wizara ya ardhi, aliondoa urasimu uliotawala pale wizarani wa kupata hati, kuja utaratibu, jinsi ya malipo na taarifa. Kitoweo je?

Magufuli hajachaguliwa aendeshe ibada, aongee anacho ongea sisi wananchi tunachotaka kuona ni kazi, woote walioona wanadhalilishwa naye wanayo idara na mahakama ya kupeleka malalamiko yao.

Kibanga Msese
 
Kila mtu ana hulka zake, lakini pamoja na utendaji mzuri Magufuli ana udhaifu wa superior complexity. So kwa vile sio mkamilifu 100%, tumsamehe maana ki-ukweli na kwa lugha yoyote alikosea ktk hilo.

Kiongozi mzuri pamoja na mengine ni vizuri awe inclusive and flexible. Binafsi sipendi style ya uongozi ya Magufuli, ingawa mara nyingi anapata results!
 
acha wifu na chuki,muache magufuri achape kazi bana.mimi sioni kosa lake.usiwe mvivu wa kufikiria
 
Kila mtu ana hulka zake, lakini pamoja na utendaji mzuri Magufuli ana udhaifu wa superior complexity. So kwa vile sio mkamilifu 100%, tumsamehe maana ki-ukweli na kwa lugha yoyote alikosea ktk hilo.

Kiongozi mzuri pamoja na mengine ni vizuri awe inclusive and flexible. Binafsi sipendi style ya uongozi ya Magufuli, ingawa mara nyingi anapata results!

RR,
Nakubaliana na wewe, binafsi naamini Magufuli anahukumiwa zaidi na historia, jinsi alivyosimamia zoezi la uuzaji wa nyumba za serikali linaweka doa ambalo linafanya chochote anachokifanya hata kama kiwe kizuri kikiwekwa kwenye mzani na hilo la nyumba linawafanya wale wanaotilia shaka uadilifu wake wayatazame mafanikio yake kwa macho tofauti.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom