Magufuli achangia Sh10 milioni matibabu ya mwanafunzi

Qualcomm

Senior Member
Nov 27, 2013
177
138
Magufuli achangia Sh10 milioni matibabu ya mwanafunzi

Dar es Salaam.
Rais John Magufuli ametoa mchango wa Sh10 milioni kwa ajili kusaidia matibabu ya mwanafunzi Bernadetha Msigwa aliyepata upofu hivi karibuni.

Msichana huyo anayesoma mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, ni miongoni wa wasichana ambao tatizo lake limeibuliwa kupitia kampeni ya Kipepeo, iliyoanzishwa na kampuni ya Clouds Media, Mei Mosi mwaka huu.

Kupitia matangazo yanayorushwa na kampuni hiyo, Rais Magufuli baada ya kusikia tatizo la Msigwa, ambaye pia picha yake imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, akiwaomba Watanzania wamsaidie mchango wa fedha ili aweze kutibiwa. aliguswa na kuamua kutoa mchango huo.

Meneja wa kipindi cha 360 kinachorushwa kila siku za wiki asubuhi na televisheni ya Clouds, Hudson Kamoga alisema baada ya Rais kuona tangazo hilo, lililorushwa muda mfupi kabla ya kuanza uchambuzi wa magazeti, alimpigia simu.

“… Alisema ameguswa na stori ya Bernadetha, hivyo yeye na familia yake watachangia Sh10 milioni ili kumsadia,” alisema Kamoga.

Kamoga ambaye aliwahi kupigiwa simu na Rais Magufuli akiwa katika ya kipindi hicho na kuwasifu yeye na wenzake wanaokiendesha, alisema baada ya muda mfupi, Rais alimwagiza msaidizi wake apaleke mchango huo.

“Zilipita kama dakika 30 hivi au 45, akawa amemtuma mtu alete zile hela,” alisema Kamoga.

Mbali na Rais Magufuli, Kamoga alisema viongozi wengine walioguswa na tatizo la Msigwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ambaye alikuwa mgeni kwenye kipindi cha 360 jana asubuhi, alichangia Sh2 milioni.

Pia, Manaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu), Anthony Mavunde Dk Abdallah Posi kila mmoja alichangia Sh1 milioni na Mkurugenzi wa Kampuni ya TSN, Farough Baghozah alichangia Sh3 milioni.

Kamoga alisema mwitikio wa Watanzania umekuwa mkubwa na hadi jana, michango iliyokuwa imetolewa ilikuwa zaidi ya Sh30 milioni anazohitaji Msigwa kwa ajili ya matibabu.

Kamoga alieleza kuwa msichana huyo alianza kupata maumivu makali ya kichwa mwaka huu na baada ya muda, alipoteza uwezo wa kuona.

“Hakuzaliwa kipofu. Amepata tatizo mwaka huu, wakiwa chuo mwaka wa tatu,” alisema Kamoga.

Alisema aliomba msaada kwao hivyo kupitia kampeni ya kipepeo, tatizo lake limefahamika na wengi na Watanzania wamemchangia ili aweze kutibiwa na kuona tena.

Source: Magufuli achangia Sh10 milioni matibabu ya mwanafunzi
 
Nampongeza sana! Ila ajue nchi hii ina changamoto nyingi sana! Wenye shida na wamekosa kabisa kuwasaidia wako wengi mahospitalini.....wengine wamekaa zaidi hata mwaka wanateseka wanashindwa hela ya operation kuanzia 1m to 30m wako wengi! Nadhani. Ifikie sasa mfuko w wizara afya kusaidia wale wasiojiweza kabisa! Vipi ambao wanateseka hawana access kufikiwa na media?
 
Sijui unampongeza kwa mantiki ipi?
Km kiongozi alitakiwa ahakikishe huyo msichana anapata tiba haraka iwezekanavyo, hiyo ndio maana ya kuongoza.

Rais anatakiwa ajue wajibu wake ku make sure wananchi wake wanapata tiba bure na huduma za operation kubwa ambazo hazipatikani nchini kuwe na mfuko wa kuwasaidia wananchi. Na sio kutaka sifa za kijinga eti anachangia wakati mchi ina wagonjwa wengi na wote wanahitaji msaada. Viongozi sio creative na on top ni lazy. Wanataka sifa za kijinga tuu through social media.

Alitakiwa akae chini na cabinet yake na wa come up with the strategy to help people in health sector.
Mashuleni hakuna laboratories na shule ambazo wanazo hizo laboratories hakuna equipments. Sasa hili taifa litazalisha ma doctors na scientists au litazalisha wakalili madesa.
Walimu nao ni tatizo, mwalimu wa Tanzania ni mtu aliyefeli mtihani halafu tuna expect wawafundishe wanafunzi ili waje kuwa na better careers, seriously? Matokeo yake ndio tuna viongozi waopenda sifa na hawajui thamani wala wajibu wao kwa wananchi waliowaweka madarakani.

Narudia tena , Magufuli acha sifa na kaa chini na cabinet yako mje na strategies zakueleweka
 
Hakika! Ni vizuri huyu ameweza kuonekana hata kwenye TV. Wapo ambao hawajaweza hata kugusa hospitali kwa matibabu.
Kwa ujumla, huduma za jamii kuu mbili, elimu na tiba, zilistahili kuwa ni nambari wani ktk bajeti badala ya barabara za rami.
 
Ila hii nchi bwana ,sasa mboreshe huduma na kuajiri wataalam,sasa hivi kuna wagonjwa wangapi wanahitaji misaada,mimi naona mnafanya ubaguzi,wagonjwa wote wajitokeze wanaohitaji matibabu nje ya nchi tuone kama mtawachangia,mimi naona ni ubaguzi tu
 
Sijui unampongeza kwa mantiki ipi?
Km kiongozi alitakiwa ahakikishe huyo msichana anapata tiba haraka iwezekanavyo, hiyo ndio maana ya kuongoza.

Rais anatakiwa ajue wajibu wake ku make sure wananchi wake wanapata tiba bure na huduma za operation kubwa ambazo hazipatikani nchini kuwe na mfuko wa kuwasaidia wananchi. Na sio kutaka sifa za kijinga eti anachangia wakati mchi ina wagonjwa wengi na wote wanahitaji msaada. Viongozi sio creative na on top ni lazy. Wanataka sifa za kijinga tuu through social media.

Alitakiwa akae chini na cabinet yake na wa come up with the strategy to help people in health sector.
Mashuleni hakuna laboratories na shule ambazo wanazo hizo laboratories hakuna equipments. Sasa hili taifa litazalisha ma doctors na scientists au litazalisha wakalili madesa.
Walimu nao ni tatizo, mwalimu wa Tanzania ni mtu aliyefeli mtihani halafu tuna expect wawafundishe wanafunzi ili waje kuwa na better careers, seriously? Matokeo yake ndio tuna viongozi waopenda sifa na hawajui thamani wala wajibu wao kwa wananchi waliowaweka madarakani.

Narudia tena , Magufuli acha sifa na kaa chini na cabinet yako mje na strategies zakueleweka
Hapana! Magufuli kama binadamu, ana emotion na tangazo kama hilo lazima likuingie akilini. Tusimlaumu ila tuseme aone umuhimu wa mambo yanayogusa jamii kila siku na siyo wale tu walioonekana kwenye TV.
 
Ndio aangalie wizara ya Afya inatatizo gani, hii ni aibu
 
kuna haja gani ya kujitangaza kama farisayo?
Mbona alipokwenda kumuona sumaye hamkusema anajitangaza.

Kweli binadamu hatuna shukrani amemsaidia mnalaumu na asingemsaidia mngelaumu ifikie hatuna linapofanywa jema tupongeze hata kama tuwapinzani.

Upinzani si kupinga kila jambo
 
Kwa hiyo kila ataejitangaza kwenye radio ataenda kumchangia? Ajue Urais ni taasisi sio mtu mmoja! Jukumu la Serikali kuona jinsi kusaidia watanzania hasa wale masikini kabisa na wako wengi sana! Angemtuma hata mke wake kupitia NGO yake au kikundi cha kina mama watoe sio Rais moja kwa moja....wakija wengine na wengine asipotoa inakuwa double standard na upendeleo!!
Mbona alipokwenda kumuona sumaye hamkusema anajitangaza.

Kweli binadamu hatuna shukrani amemsaidia mnalaumu na asingemsaidia mngelaumu ifikie hatuna linapofanywa jema tupongeze hata kama tuwapinzani.

Upinzani si kupinga kila jambo
 
Mnaosema kakosea nazan hamjapata stori kamili ya huyu binti, na haijawagusa.
Embu fikiria n wewe hapo upo degree mwaka wa misho semester ya mwisho ukitarajia kukamilisha ndoto yako alafu inatokea hali hiyo na hunamsaada zaid ya kuupata katika jamii.
 
Sasa watu wanalalamika nini hapa mbona sielewi huyo Maguful hata mwaka hajafikisha madarakani eti wanasema tuandae taratibu watu watibiwe hapa kwa taratibu gani hebu zieke hapa na onyesha itachukua mda gani kila kitu kinahitaji mda kufanikisha hakuna shortcut.

Mm nampongeza kwa kweli katoa yy na familia Yake kutoka mfukoni mwake km yy kutokana na historia ya huyo mtu Ila naamini tutafika huko tunako taka kufika
 
Kwani huyu binti anahitaji matibabu gani? Ameenda ccbrt? Sijaelewa stories naona kila mahali wanaongelea kaamka haoni
 
Back
Top Bottom