Magufuli aanza kazi J2 kwa vitisho......Kweli aanza vibaya......

Hakuna WIZARA, IDARA, SHIRIKA LA UMMA, TAASISI YA UMMA itasafishika peke yake kwa staili hii ya Maghufuli ya TV na vyombo vingine vya habari. Tatizo tulilo nalo ni la NCHI kama sio TAIFA. Ni MFUMO. Unahitaji kubadilishwa. Ni kuiondoa CCM na akina Maghufuli madarakani. Alikuwepo wizara hiyo miaka michache iliyopita. Hakuna mkakati wa kudumu na endelevu aloouacha kuzuia haya. Serikali ya CCM haiwezi kujikaanga yenyewe kwa mafuta yake. TUSIDANGANYANE.
 
tumpe mda Dr Magufuri,mimi namkubari yule Dr hana makuu na anachokisema humaanisha huwa hakurupuki,kwa kweli Tanroad inamatatizo makubwa sana kama unakumbuka yule mkuu wao alitakiwa kujiuzuri kipindi furani kwa kutoa ajira ki kabara na pia wabunge wengi walikuwa na wasiwasi na elimu ya kingunge huyo,sasa tumpe mda Dr afanye kazi titamkubari wenyewe ni mapema mno kublem

mapinduziiiiii daimaaaaa
 
mhh hapa tz ukifanya vizuri unaonekana mbaya kweli ukila kimya kimya kifisadi basi watu unafanya kazi kweli aisee tabu kweli niliposikis magufuri kaenda huko niikajua kule tanlods Mrema kwisha kazi na kumuondoa mrema kwangu ni big up magufuri manake kulikuwa kunanuka uvundo na chapili kama ntaona ktk miaka mitano yako vitu vingi utakavyovifanya kama utajenga lile daraja kigamboni basi kwangu nitakuendelea kukuamini sitaaki kujua ukochama gani mi na thithiem tofauti ila utendaji wako kwangu naukubali saan a si lazima utangaze vita na mafisadi vitendo vyako wenyewe watajua kwani unapotaka kula na kipofu lazima umguse mkono big up mwanzo mzuri hasa kuona unafanya kazi na mwakyembe wizara zipo nyingi zingine hata hatuju miaka mitano inafanya nini umepelekwa kule uvuvi hata vitoto vikajua kumbe nako kunalidwa aisee watnzania tuspende majungu ndo maana nchi inavitu vingi ila bado maskini sie tumekalia majungu na kubebana huku taifa linateketea yan wamembeba mrema huku wanajua anaharibu bado wamemuachaa haya wapeni nchi hao wakina lowasa chenge muone
 
Magufli is a right man in this ministry..Rutashubanyuma please uwe mwangalifu na kukurupuka kutoa comments na conclusion bila kujua.

Magufuli siyo mnafiki ameeleza waziwazi kuhusu Mrema, sijajua unaifahamu kiasi gani hii wizara, mimi kazi zangu zinaangukia wizara hii, inatisha imeoza
 
mhh hapa tz ukifanya vizuri unaonekana mbaya kweli ukila kimya kimya kifisadi basi watu unafanya kazi kweli aisee tabu kweli niliposikis magufuri kaenda huko niikajua kule tanlods Mrema kwisha kazi na kumuondoa mrema kwangu ni big up magufuri manake kulikuwa kunanuka uvundo na chapili kama ntaona ktk miaka mitano yako vitu vingi utakavyovifanya kama utajenga lile daraja kigamboni basi kwangu nitakuendelea kukuamini sitaaki kujua ukochama gani mi na thithiem tofauti ila utendaji wako kwangu naukubali saan a si lazima utangaze vita na mafisadi vitendo vyako wenyewe watajua kwani unapotaka kula na kipofu lazima umguse mkono big up mwanzo mzuri hasa kuona unafanya kazi na mwakyembe wizara zipo nyingi zingine hata hatuju miaka mitano inafanya nini umepelekwa kule uvuvi hata vitoto vikajua kumbe nako kunalidwa aisee watnzania tuspende majungu ndo maana nchi inavitu vingi ila bado maskini sie tumekalia majungu na kubebana huku taifa linateketea yan wamembeba mrema huku wanajua anaharibu bado wamemuachaa haya wapeni nchi hao wakina lowasa chenge muone
 
Unajua wanaomchukia Magufuli ni Kati ya hao watakaoathirika na kurudi kwake. Maana Tanroad wameongeza gharama ya Km 1 ya lami kutoka mil. 300 hadi 1 Bilioni kwa ajili ya kugawana. Sasa wasubiri kiama chao

Mkuu hapo juu kwenye red kuna ushahidi wa wazi? kama upo mkabidhi wakili Marando/Tindu Lissu wafanyie kazi
 
mbona lalipouza nyumba za serikali hamkusema "end justifies the means"??? sasa hata atakapouza mgreda yote ya serikali kama aliyouza zile nyumba mtasema "end justify the means"!! jamani waTZ mna tatizo gani kwenye mbongo zenu????

hauyu ni kati ya makosa makubwa aliyorudisha kikwete!


Hilo swala la nyumba kuuzwa lazima liwe cabinet decision siyo waziri peke yake na wala halihusiani na utendaji wa waziri kwa ujumla. Ukubali au ukatae huyu ni mchapa kazi kuliko mawaziri wote kwenye hilo baraza la JK unless kama una bifu naye tu!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lazima tuwe objective na sio kuleta ushabiki wa vijiweni.
1.Kuhusu ilani ya CCM wewe ulitaka agawe ilani ya CDM?of course vipa umbele vinaweza badilika from time to time na ilani inacover nch nzima
2.Ajira mpya-Magufuli anataka afanye nao kazi hao hao ili mwishowe kama wanaboronga waboronge nae akiwa yupo na itakuwa mda mwafaka wa kuwatimua.The msg apa ni kuwa kama umekoswa koswa kutimuliwa ukiachwa unabadilika.
3.Sasa kama ata kazi hajaanza rasmi ushaanza kumkosoa then sidhani kama ata akifanya mzauri utaapriciate?
Uzuri wa Magufuli huwa hasikilizi majungu ya apa na pale,as he is after delivering what is in the ILAN plus items to be added in future.
NB:Kasema in 3 years atakuwa ameaccomplish yaliyomo kwenye ILANI then remaining 2 years itakuwa AOB
 
Wizara hii ndiyo itamaliza Magufuli kisiasa. Kila mahali (wizara), alipopita Magufuli ameacha matatizo. Nyumba za serikali ziliuzwa wakati wake, makandarasi fake wa China ilikuwa wakati wake na kuna wavuvi wa kigeni bado wapo rumande mpaka leo kwa sababu yake na dalili zinaonyesha kuwa itakuwa vigumu kushinda hiyo kesi. Serikali ilitakiwa kulipa fidia Mwanza kwa mfanyabiashara aliye vunjiwa kituo cha mafuta. AMEFANYA NINI zaidi ya tumia magazeti kufanya kazi.
 
:yo::yo::plane::A S 41::A S 41::welcome:"MATOKEO YA KAZI YOYOTE NI VITENDO TUSUBIRI TUONE; MAANA MAGUFULI HANA MASIHARA KABISA"
 
hakuna wizara, idara, shirika la umma, taasisi ya umma itasafishika peke yake kwa staili hii ya maghufuli ya tv na vyombo vingine vya habari. Tatizo tulilo nalo ni la nchi kama sio taifa. Ni mfumo. Unahitaji kubadilishwa. Ni kuiondoa ccm na akina maghufuli madarakani. Alikuwepo wizara hiyo miaka michache iliyopita. Hakuna mkakati wa kudumu na endelevu aloouacha kuzuia haya. Serikali ya ccm haiwezi kujikaanga yenyewe kwa mafuta yake. Tusidanganyane.

we unasambaziwa ilan ya ccm wht nexty?
 
Najua wengi watamsema magufuli vibaya hapa, sababu wanajua kitumbua kimeingia mchanga
 
umewahi mnuo ndio kwanza watu wanaamuka subiri wanywe chai halafu usalimie
 
Hilo swala la nyumba kuuzwa lazima liwe cabinet decision siyo waziri peke yake na wala halihusiani na utendaji wa waziri kwa ujumla. Ukubali au ukatae huyu ni mchapa kazi kuliko mawaziri wote kwenye hilo baraza la JK unless kama una bifu naye tu!!!!!!!!!!!!!!!!


Yaani hapo Mr Zero mi ndipo ninaposhindwa kuwaelewa watu. Tatizo la watanzania walio wengi ni kushindwa kujieleimisha kuhusu mazingira yao yanayowazunguka na mwisho kuishia kutumia maneno ya vijiweni na magazeti ya udaku kujenga hoja zao. Magufuli hakuuza Nyumba kama wazo lake binafsi alilotoka nalo nyumbani. Nyumba zile zimeuzwa kwa kile kinachoitwa uwajibikaji wa Pamoja wa Baraza la Mawaziri ingawaje inawezekana pia aliyelianzisha wazo hilo ni aliyekuwa mkulu mwenyewe ama mkewe.
Tusimhukumu Magufuli kwa hilo.
At least katika huu uozo wote wa uongozi uliotuzunguka there is somebody who dares to put something right, no matter how little.
Ndugu yangu Ruta hii nchi sasa imefika mahali ambapo hatuswi kupaka rangi ama sukari maneno yetu ili kufurahisha watu. We are too far gone for that.
Tunataka mtu mwenye ujasiri wa kuita beleshi ni beleshi na sio kijiko kikubwa.
Let Magufuli try his two cent.
At least he is trying.............Give him a Chance,and a hand in that, Please.
 
Give me a break!!!! Asilimia 99 ya wananchi waliohojiwa wakati tunasubiri Raisi atangaze baraza la mawaziri walisema wangependa kumuona Magufuli na Prof Tibaijuka wakipewa uwaziri! Leo hii wewe tu ndio unaona hafai....una lako binafsi
 
Taarifa ya habari ya saa moja jioni ya leo ya TBC1, Waziri wa Miundo mbinu Dr. Magufuli amesambaza Ilani ya uchaguzi za CCM kwa watendaji Wizarani kwake katika hali inayoonyesha anachapa siasa zaidi na kuwataka watendaji wote kwenye Wizara yake kuisoma, kuielewa na kuifuata..................au vinginevyo waache kazi au wataondolewa.....................

Vile vile amesimamisha zoezi la ajira mpya TANROADS katika hali inayoonyesha mwingiliano kati ya Bodi ya Wakurugenzi na Wizara Mama.............Kiutaratibu Wizara Mama haipaswi kujiingiza katika shughuli za kiutendaji za TANROADS..........Hayo ni majukumu ya Bodi na Menejimenti.......

La kusikitisha zaidi ni sababu alizozitumia katika kuhalalisha Uongozi wa Wizara kuingilia zoezi la ajira mpya za Wahandisi wa Mikoa wa TANROADS............alidai wao wanataka barabara zijengwe tu..........kama vile waliopo kazi hiyo huifanya kwa ufanisi wakati sivyo hata kidogo..................

Magufuli anashindwa kuelewa ya kuwa ni sera ya TANROADS ili kuimarisha ufanisi ajira ni za mikataba na kama watendaji wataelewa ajira ni za kudumu hawatakuwa na motisha wa kuongeza ufanisi...............................Pia TANROADS ina kashfa nyingi za matengenezo bomu ya barabara ikilinganishwa na fedha ambazo serikali hutumiwa kwenye shughuli hizo zikiongeza kasi ya umuhimu wa kuubadilisha uongozi mzima wa TANROADS....................

Mbaya zaidi, zoezi la mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS yamekuwa yakipingwa na wabunge hususani Bunge la 9 kwa sababu hizohizo za kujenga barabara wakati barabara nyingi ni bomu................hii yaashiria Regional Engineers na watendaji ndani ya TANROADS wana sauti kubwa kuliko hata Bodi yao ya wakurugenzi katika kuchelewesha mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS kwa masilahi yao binafsi tu......Kwa mwelekeo huu usitegemee jipya kutoka kwa Magufuli........aonekana ni mchovu sana kifikra na sasa ategemea jina kuisukuma Wizara hii atakako..........

ni mapema mno ku conclude kama ulivyofanya , wape muda ili upate facts za kukuwezesha kutoa conclusion inayokubalika
 
Taarifa ya habari ya saa moja jioni ya leo ya TBC1, Waziri wa Miundo mbinu Dr. Magufuli amesambaza Ilani ya uchaguzi za CCM kwa watendaji Wizarani kwake katika hali inayoonyesha anachapa siasa zaidi na kuwataka watendaji wote kwenye Wizara yake kuisoma, kuielewa na kuifuata..................au vinginevyo waache kazi au wataondolewa.....................

Vile vile amesimamisha zoezi la ajira mpya TANROADS katika hali inayoonyesha mwingiliano kati ya Bodi ya Wakurugenzi na Wizara Mama.............Kiutaratibu Wizara Mama haipaswi kujiingiza katika shughuli za kiutendaji za TANROADS..........Hayo ni majukumu ya Bodi na Menejimenti.......

La kusikitisha zaidi ni sababu alizozitumia katika kuhalalisha Uongozi wa Wizara kuingilia zoezi la ajira mpya za Wahandisi wa Mikoa wa TANROADS............alidai wao wanataka barabara zijengwe tu..........kama vile waliopo kazi hiyo huifanya kwa ufanisi wakati sivyo hata kidogo..................

Magufuli anashindwa kuelewa ya kuwa ni sera ya TANROADS ili kuimarisha ufanisi ajira ni za mikataba na kama watendaji wataelewa ajira ni za kudumu hawatakuwa na motisha wa kuongeza ufanisi...............................Pia TANROADS ina kashfa nyingi za matengenezo bomu ya barabara ikilinganishwa na fedha ambazo serikali hutumiwa kwenye shughuli hizo zikiongeza kasi ya umuhimu wa kuubadilisha uongozi mzima wa TANROADS....................

Mbaya zaidi, zoezi la mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS yamekuwa yakipingwa na wabunge hususani Bunge la 9 kwa sababu hizohizo za kujenga barabara wakati barabara nyingi ni bomu................hii yaashiria Regional Engineers na watendaji ndani ya TANROADS wana sauti kubwa kuliko hata Bodi yao ya wakurugenzi katika kuchelewesha mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS kwa masilahi yao binafsi tu......Kwa mwelekeo huu usitegemee jipya kutoka kwa Magufuli........aonekana ni mchovu sana kifikra na sasa ategemea jina kuisukuma Wizara hii atakako..........

Mkuu ulijianda kuchukua Post nini. Naona umesikitika kweli kusitishwa kwa ajira hizo. Pole sana. Hata hivyo unaonekana ni wale wanataka kuingia TANROADS kujinufaisha.

Fanya utafiti ujue Matatizo yaliyopo TANROADS, Nani kasababisha, Na nini kinahitajika kufanyika ndo uandaa maada yako.
 
Kama ni mori, basi huu umeanzia kileleni. Natumai nguvu hii iliyooneshwa asubuhi hii itaendelea mchana hadi jioni. Hadi atakapochoka, atakuwa ametiisha adabu kidogo na heshima kurudi mahala pake.

Magufuli baba, lianzishe tu, barabara michosho zishatukifu, majengo yanayoanguka hovyo, sasa basi!

Bofya kifute hapo umsikilize kiduuuchu kilichorekodiwa kupitia TBC one. Taarifa ya maandishi inafuatia...



Siku moja tu baada ya kuapishwa, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na naibu wake Dk. Harrison Mwakyembe wamefanya kikao na Watumishi wa Wizara na kutoa maagizo kadha wa kadha.

Magufuli vs TanRoads vs Mrema

Mojawapo ya maagizo makuu, Waziri Magufuli alitengua maamuzi ya Mkurugenzi Wakala wa Barabara nchini (TanRoads), Ephraim Mrema na kuagiza mameneja wa mikoa waelezwe mara moja kuwa wamerudishwa kazini isipokuwa kwa nafasi ya Dodoma tu ambayo meneja wake hayupo. "Futeni hiyo mara moja, mameneja wa sasa waliopo nasema waendelee na kazi, maamuzi mliyochukua hayafai," akamwagiza Mrema kutoa tangazo haraka kuanzia leo katika vyombo vya habari, kusitisha tangazo lake la awali la kuwasimamisha kazi mameneja wa TanRoads mikoani kwa kuwa hatua aliyoichukua inaonekana ni ya kulipizana visasi. "Nimesoma katika gazeti moja wiki hii, umetangaza nafasi za kazi…kuna utaratibu kwa kazi zozote zinapotangazwa, hivyo waandikie vyombo vyahabari kuwa umefuta nafasi hizo..." "Nakuagiza Mrema, uandike katika vyombo vya habari kuwa umefuta tangazo hilo na mengine yatafuatia.” alisema na kukamtaka Mrema asifanye kazi kama mtu anayeondoka kesho, bali atekeleze majukumu yake kama atafanya kazi hiyo kwa miaka 100 ijayo.

“TanRoads jipangeni sawasawa, blaablaa ziishe, wewe Mkurugenzi uliona nafasi yako inatangazwa na wewe ukaamua kutangaza za mameneja wa mikoa ili kuchomeana na kila kitu kisimamishwe, kwanini ulitangaza kwamba waliopo hawachapi kazi?” alihoji Dk. Magufuli.

Kutokana na umuhimu wa usimamizi wa ujenzi wa barabara, Akamtaka Mkurugenzi huyo wa TanRoads, kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba kama Waziri na Naibu wake Dk. Harrison Mwakyembe watauliza jambo lolote, wajibiwe haraka, la sivyo itakuwa ni dharau. Mkurugenzi huyo wa TanRoads inadaiwa kuwa kipindi chake cha kuongoza wakala huo kimemalizika kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi, lakini ameendelea kukalia ofisi hiyo.

Kunyang'anywa nyumba na kufikishwa mahakamani

Waziri Magufuli ameagiza wote waliouziwa nyumba za serikali ambao hawajamaliza madeni yao kufikishwa mahakamani pamoja na kunyangíanywa nyumba hizo. "Muwaandikie barua wote walipe au muwapeleke mahakamani na wasipolipa wanyangíanywe," alisema Magufuli na kushangaa kwa nini Wizara inahangaika suala la uhaba wa nyumba za watumishi wakati kuna pesa nyingine nje. Akasema kwa kawaida, hana lugha ya kidiplomasia na amewataka wenye madeni kuyalipa mara moja.

Magufuli vs Rushwa na Mizani

Dk. Magufuli alisema kasi ya ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege imepungua kwa kiasi kikubwa, huku wafanyakazi wengi wakijihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwapa kazi makandarasi wababaishaji ambao lengo lao ni kuchuma. Waziri Magufuli aliahidi kupanda lori lililozidisha uzito na kutoa rushwa na akasema akikamilisha kazi hiyo watakaohusika watamtambua. Aliwataka watendaji wa mizani kusimamia sheria, kukamata magari na kupiga faini na kuteremsha mizigo bila kujali mmiliki wa gari au mzigo.

"Ukienda barabara ya Mandela, hujui kama kuna mkandarasi kwenye eneo lile ujenzi wa barabara nyingi kasi yake si nzuri, kama mkandarasi wa Mandela rafiki yako hafanyi kazi vizuri fukuza. Lazima niwaambiwe ukweli, mtu asiyetaka kuambiwa ukweli ajiandae kuondoka...," "...wananchi wamechoka kuona ubabaishaji huo, na kuanzia ni barabara ya Mandela, nataka taarifa ya ujenzi ndani ya mwezi mmoja, kwa maana mkandarasi sijui ni rafiki yenu au ni ndugu yenu kwani, hata kituo cha kazi hayupo sasa nataka ripoti yake alipofikia..." alisema Magufuli.

Akasema Watanzania wamechoshwa na maneno ya kubabaishwa na wataka barabara. "Maisha bora ni pamoja na barabara nzuri, nawapa mwezi mmoja mtafakari tuanze kujenga barabara za juu, tunaweza," alisema Magufuli.Alisema hakuna haja ya kuwasumbua askari wa usalama barabarani kuongoza msongamano wa magari, huku wakazi wa jiji wakilia na kulalamikia kero hiyo wakati nchi imesheheni wahandisi wa kutosha. Akasema kama maghorofa yanaweza kujengwa kipindi kifupi, iweje ishindikane kwa barabara za juu. “Hata barabara za juu zinawezekana, hivyo kazi ya matrafiki ibakie kukaa na kutulindia nguzo zetu na kukamata magari yanayofanya makosa,” aliweka wazi.

Waziri Magufuli alitoa maelekezo kwa bodi ya makandarasi kuwafutia vibali na kuwafukuza wale ambao wameweka zaidi maslahi kuliko kazi walizoomba. "Tutatumia sheria, lazima tuzihurumie fedha za Watanzania," alisema na kuongeza kuwa "...Serikali haiwezi kuendelea kuona kila kukicha makandarasi wanapanga bei wanazotaka," alisema.

Alionya wale wote wanaojihusisha na rushwa na kuwapatia ushindi wa zabuni makandarasi ambao ama hawana uzoefu au kwa kutaka pesa nyingi kutokana na gharama zao kuwa juu. "Tunajua rushwa ipo, hivi sasa makandarasi wapo katika mchakato tuache rushwa tutawaletea hata pesa za polisi...," “Magari yanazidisha uzito, ipo siku nitafanya msako wa kushtukiza kwa magari yanayozidisha uzito… nitaingia katika lori moja na kupanda halafu nitajibadilisha kwa kuvaa miwani na kofia ili nikamate wale wafanya kazi wenu wa mizani maana wanachukua rushwa sana...” “Sisi pia tutakuwa na kazi tutavamia maeneo na tukikuta mmeshindwa kufanya kazi tutafukuza mkandarasi na wewe ukifuata, hatutacheka na mtu tumekuja kufanya kazi maana barabara nyingi zilizochini ya Tanroads ndizo zenye matatizo, hivyo lazima malengo yatimizwe kipindi cha miaka mitatu,”alisema Waziri Magufuli na kuongeza kwamba kumezuka mtindo wa mtu anayetoa gharama za juu katika zabuni ndiye anapewa nafasi ya kwanza.

Ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Uwanja wa Ndege Songwe

Kuhusu mradi sugu wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Magufuli alionyesha kushangaza kuona ujenzi unasuasua na kutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuweka bayana kama hauwezi, atahakikisha linajengwa kwa fedha za serikali kwa kuomba kutoka Benki Kuu (BoT). "Kuna daraja moja refu sana kule China, urefu wake ni kwenda na kurudi Zanzibar mara tatu, walijenga kwa mwaka mmoja, sasa kwanini tunashindwa Kigamboni" alihoji. Aliitaka idara inayoshughulikia vivuko kuangalia uwezekano wa kununua vivuko vingine vinne, vitakavyokuwa vinafanya safari hadi Tegeta na Bahari Beach ili kupunguza msongamano wa magari barabarani.

"Tutasaidia wananchi badala ya kukaa kwenye foleni kwa saa nne hadi tano, sasa waweze kutumia dakika 45 kufika Tegeta," alisema na kuongeza kuwa kama serikali imenunua vivuko viwili, haishindwi kununua vingine kwa ajili ya kutoa huduma.

Kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege Songwe, alisema Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Prosper Tesha, anapaswa kuhakikisha na kusimamia kukamilika kwa uwanja huo uliopo mkoani Mbeya kutokana na mkandarasi kuchukua muda mrefu. “Lazima usimamie ukweli ni suala la kujiuliza kwanini ule uwanja haukamiliki na hauishi, inawezekana mnawabembeleza nini hao wakandarasi? naomba usimwogope mtu, fanya kazi hata siku ukifa amini utakwenda kuwa mkurugenzi mkuu wa viwanja vya ndege mbinguni,” alisema.

Kupoteza muda kwenye Majungu badala ya Kazi

Alisema baada ya kuapishwa, alikubaliana na naibu wake waanze kazi rasmi jana, kwani miaka mitano si mingi, ambapo aliwapa muda wa miaka mitatu wakurugenzi hao kuhakikisha yale yote yaliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi yanatekelezwa ndani ya kipindi hicho.

"Hatujawaambia wote muwe CCM, ila kwa sababu wananchi wameamua, serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, mnapaswa kuteleleza yale yote yaliyoahidiwa humu, kwa bahati mbaya sana mmeangukia katika mikono yetu, lazima mfanye kazi," alisisitiza.

Alisema wizara hiyo hivi sasa imegubikwa na majungu na rushwa, huku utendaji wa kazi ukiwa umezorota kwa hali ya juu. Alisema watendaji wazuri wamekuwa hawapewi umuhimu kwa sababu ya kuendesha majungu na kuwepo kwa makundi.

"Kuna mtu hapa amechora daraja la Umoja na lile na Mkapa, amefanya kazi nzuri sana, lakini hata siku ya ufunguzi, waliona kazi kumtambua kwa kumtaja jina tu, sasa nakurudisha kwenye madaraja endelea na kazi, najua ni fitina," alisema.

Muda wote wakati anazungumza, ukumbi ulizizima kiasi kwamba hakuna mtu yeyote aliyeweza kumnongíoneza mwenzie jambo, ambapo hata baada ya mawaziri hao kutoka, watumishi hao walikaa ndani kwa dakika kadhaa kila mmoja akisubiri nani aanze kutoka.

Kauli ya Dk. Mwakyembe

Awali, akizungumza Naibu Waziri Dk. Mwakyembe alisema Wizara ya Ujenzi katika miaka ya karibuni imepoteza sifa yake ya awali ya kuwa wachapakazi pamoja na kuwepo kwa wasomi wazuri. Alisema mwanzoni wizara hiyo ilikuwa mfano wa kuigwa lakini anashangaa kuona ufanisi umepotea na sasa imekuwa sehemu ya kunyoosheana vidole bila kujua ni kirusi gani huyo aliyeingia. Alisisitiza kuwa sasa wanahitaji kuongea lugha moja na kuimba wimbo mmoja na kuifanya wizara hiyo kuwa ya mfano na kuagiza taarifa za kukinzana zisipewe nafasi kwa kuwa hawaendeshi wizara kwa majungu na umbeya. Aliwataka wafanyakazi kuwa wakweli na kufanya kazi kwa uwazi zaidi. "Mmepoteza sifa, sioni kama wizara hii ni kitovu tena cha ufanisi, nasema bila kuchakachua, uteuzi wetu hautakuwa wa maana kama tutaachia hali hii iendelee," alisema. Aliwataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii, kwani muda ni mdogo na mambo ni mengi.

Ushirikiano "lay a strong foundation first" Mwanzo-Mwisho

Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli na Naibu wake, Dk. Harrison Mwakyembe, walikuwa na kikao rasmi jana na wakurugenzi wa idara na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, ambapo walitangaza kuanza kazi kwa kukabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Walisema wao hawakufika katika wizara hiyo kwa ajili ya kutengua Torati, bali kuitekeleza na kwamba wanaweza kufanya kazi na yeyote na kusisitiza kuwa yaliyopita yaachwe na wafanye kazi kwa pamoja, "ndiyo maana tumeamua kufanya ibada yetu leo hapa," “Tushirikiane, tupendane, majungu yaishe, tuache rushwa kwa kuwa tutawategeshea hata fedha ya Polisi… na hivi ndio maana Rais ametuteua mimi na Naibu mwenye taaluma ya Sheria,” alisema.

Waziri alisema ujenzi wa barabara mpya kwa kiwango cha lami utaanza kutekelezwa mara moja kama ilivyoanishwa katika Ilani, na kutaka apewe taarifa ya barabara zinazoendelea kujengwa za Tunduma/Sumbawanga, Sumbawanga/Mpanda, Arusha/Namanga, Singida/Kateshi/Babati na Babati/Dodoma/ Iringa.

credit ya habari magazeti ya UhuruPublications, HabariLeo na Mwananchi



from: Oho hou! Moto wa Magufuli umeanza... aluuu! -
 
Back
Top Bottom