Magufuli 2015-2020: Matarajio ya uchumi na changamoto zake

Sekta ya Afya nchini imejengwa na ‘a three tier system” kama
Pamoja na kwamba aslimia sabini na tano (75%) ya mahitaji ya afya kwa wananchi yapo katika ngazi ya KWANZA (i.e. basic clinics and dispensaries), huku asilimia ishirini na tano (25%) mahitaji ya afya ya wananchi yakiwa katika ngazi ya JUU (i.e. referral hospitals and specialty), katika upangaji wa bajeti za Wizara ya Afya miaka nenda miaka rudi, serikali huwa haitengi fedha kwa kufuatana na mahitaji haya. Badala yake, asilimia 75% ya ‘resources’ (madawa, vifaa, mishahara, posho, education and training, nk) huwa zinapelekewa kwenye ngazi ya juu (referral hospitals na Specialties).
Naomba ufafanuzi kuhusu hizi takwimu.
 
Mkuu , siku za nyuma sekta ya afya ilijengwa katika 'four tier system'
1. Clinic na dispensaries (zahanati)
2. Hospitali za Wilaya
3. Hospitali za mikoa
4. Hospitali za rufaa na zile maalum

Kwasababu zisizoeleweka kitaalamu awamu ya nne ikapandisha hadhi hopsitali za mikoa kuwa za rufaa. Hili halikuzingatia maana halisi ya hospitali za rufaa

Jambo hili limekuwa na matokeo haya

1. Kupoteza nguvu za hospitali za mikoa ambazo hazikidhi haja ya kuwa kuwa za rufaa
Hospitali za mikoa zimekosa eneo lake kama ulivyoonyesha 'three tier system'

2. Kudoroa hospitali za mikoa kumepelea ongezeko la 'mzigo'hospitali za rufaa/maalam.

3. Ongezeko la hospitali bila mpangilo limezaa tatizo la 'resource allocation' .
Kwa hali hiyo, huduma zinazotolewa na hospitali za rufaa ni za kiwango cha chini.
Kupandishwa hadhi kwa hospitali za mikoa kuna affect vipi accessibility ya huduma za afya zilizokuwa zikitolewa kabla ya kupandishwa hadhi kwa hospitali hizo?

Nadhani wakuu mnachanganya sana mambo, twendeni taratibu msianze kutuchanganya!! please!
 
Kuhusu trend ya deni la Tanzania

  1. Halikukua mara 7 katika miaka 5

  2. Kukopa 1.4 billion ndani ya miezi sita tu, hakumaanishi tutakopa 2.8b ndani ya mwaka, so that’s a misleading statement na imekaa kipropaganda. Otherwise, whats the point?

  3. Deni la nje ni bora kuliko deni la ndani na ni nafuu zaidi (refer to interest rates, Non -HPIC)
 
Attachments

  • upload_2016-5-21_4-29-37.png
    upload_2016-5-21_4-29-37.png
    24.9 KB · Views: 20
  • upload_2016-5-21_4-30-3.png
    upload_2016-5-21_4-30-3.png
    24.9 KB · Views: 20
  • upload_2016-5-21_4-30-26.png
    upload_2016-5-21_4-30-26.png
    10.8 KB · Views: 18
  • upload_2016-5-21_4-33-1.png
    upload_2016-5-21_4-33-1.png
    42.1 KB · Views: 18
Kupandishwa hadhi kwa hospitali za mikoa kuna affect vipi accessibility ya huduma za afya zilizokuwa zikitolewa kabla ya kupandishwa hadhi kwa hospitali hizo?

Nadhani wakuu mnachanganya sana mambo, twendeni taratibu msianze kutuchanganya!! please!
Mkuu mbona nimeeleza vizuri tu! ukisoma bila 'prejudice' utaiona hoja.
 
Kuhusu trend ya deni la Tanzania

  1. Halikukua mara 7 katika miaka 5
Umezoeleka kwa uvurugaji wa mada miaka yote kwa hisani ya Lumumba. Serikali ya ovyo iliyopita uliitetea kwa kila namna, sembuse hii ya maigizo?

Unaposema 'halikukuwa mara 7 katika miaka 5', unalenga kupoteza mwelekeo wa mjadala. Kwanini usiweke hoja husika kwa kunukuu kilichowasilishwa na badala yake unaokota okota ovyo namba na kuzirushia bila ukamilifu?

Kukopa 1.4 billion ndani ya miezi sita tu, hakumaanishi tutakopa 2.8b ndani ya mwaka, so that’s a misleading statement na imekaa kipropaganda. Otherwise, whats the point?

Hapa vile vile, tuwekee hapa nukuu ya kilichowasilishwa.

Deni la nje ni bora kuliko deni la ndani na ni nafuu zaidi (refer to interest rates, Non -HPIC)
Hakuna ukweli wowote kuhusu unafuu wa deni la nje vis a vis deni la ndani. Inaonekana wazi jinsi gani usivyokuwa na uelewa, na jinsi gani hamjaandaliwa vizuri kuja kujadili masuala kama haya. Fuatilia hoja juu ya concessional versus non concessional lending. Fuatilia hoja kuhusu historia ya deni la taifa, na hasa kuhusu changes in the debt portifolio, what has been replacing concessional loans and the associated costs and risks. Leta hoja kama ilivyowasilishwa kisha uje na hoja mbadala. Weka kilichowasilishwa, kilivyowasilishwa, nukuu kitu kamili, usitafute upenyo wa spinning zako za siku zote kutuondoa kwenye hoja ya msingi.

Na una maoni gani kuhusu hidden debts kwa uso wa 'Public Private Ownership projects' kwenye sekta ya nishati nilizowasilisha - IPTL, Songas na Symbion?
 
Naomba ufafanuzi kuhusu hizi takwimu.

Nitaleta reference, nimeichanganya kwenye makabrasha, lakini huo ndio uhalisia na Serikali justifies that kwa hoja mbili kuu:

1. Kwanza ni kwamba matumizi makubwa zaidi yanahitajika ngazi za juu kwa sababu Serikali inahitaji to produce wahitimu wengi na wa kutosha (wa afya) kwa sababu wanahitajika kwenda kutoa huduma katika ngazi za chini za mfumo wa Afya.

2. Pili, ni kwamba matumizi makubwa zaidi yanahitajika ngazi za juu hasa kwenye hospitali za rufaa na hospitali maalum kwa sababu wananchi wengi ni maskini, na hawawezi kugharamia matibabu yanahohitaji huduma za ngazi za rufaa au hospitali maalum.

Lakini cha ajabu ni kwamba, zaidi ya 70% ya vifo vinavyowamaliza watanzania vinatokana na magonjwa yanayotibika, tena bila ya ulazima wa kufuata huduma kwenye referral and specialty hospitals. Magonjwa hayo yanaweza kutibika na hata kuepukika kabisa iwapo ngazi za chini zitapatiwa vitendea kazi, madawa na wataalam wa kawaida.
 
Kupandishwa hadhi kwa hospitali za mikoa kuna affect vipi accessibility ya huduma za afya zilizokuwa zikitolewa kabla ya kupandishwa hadhi kwa hospitali hizo?

Nadhani wakuu mnachanganya sana mambo, twendeni taratibu msianze kutuchanganya!! please!
Pamoja na kukusihi usome bila 'prejudice' kuona hoja za wengine, napenda nikujibu swali lako kama ifuatavyo

1. Endapo kupandisha hadhi za hospitali hakuna effect katika accessibility ya huduma za afya, basi haingekuwa na maana ya kuzipandisha hadhi! Hii ni kwa mujibu wako

2. Kupandisha hadhi ya hospitali ni suala la kitaalamu likizingatia vigezo vinavyopaswa.
Miongoni mwa vigezo hivyo, ni wataalam hasa specialists na vifaa.

Si jambo la kisiasa, kuamka asubuhi na kutangaza Hospitali X ni ya rufaa kama tawi la chama kuwa ofisi ya mkoa asubuhi moja kwa matakwa ya kisiasa

Huduma zetu kama alivyosema Mchambuzi ni primary , secondary na tertiary. Tetiary ndiyo referral hospital.

Utakubaliana nami ya kuwa Hospitali za mikoa hazina hadhi ya kuwa referral

a)Hazina wataalamu wa kuzi qualify kama referral Hospitals
b)Hazina vifaa vnavyoweza kukidhi haja ya referral hospital

Mgonjwa akitoka kituo cha afya kwenda Hospitali ya Wilaya, likely atakuwa na referral ya Clinical Officer. Huko Wilayani atakutana na Assistant Medical office (AMO).
Naye anaweza kumfanyia referral Hospitali ya mkoa. Hapo ndipo tatizo lililpo

Hospitali za mikoa bado zina upungufu wa Medical officers( Dr) na mgonjwa atapata huduma ya Clinical officer au AMO na kwa bahati Dr. Hakuna Specilists

Hata kwa zile zenye Specialists, bado wanafanya 'clinical work' kwasababu hawana vifaa vya kuwawezesha kutenda kazi zao.

Mathalani, mgonjwa aliyepewa referral kwa matatizo ya maumivu makali ya tumbo akiwa mja mzito, kuna differential diagnosis nyingi nyuma yake
Inawezakana kuwa ni ruptured appendicitis au ectopic pregnant

Huko mikoa X-ray hazifanyi kazi na haziwezi kutoa diagnosis kwasababu kazi yake ni imaging, na inapokuwa suala la soft tissue ni useless.
Vifaa vinavyoweza kutoa mwanga au diagnosis ni kama Ultra sound au MRI.

Hospitali ngapi zina vifaa hivyo nchini achilia za mikoa?

Wataalam katika ngazi ya Clinical officer au AMO hawana uwezo wa kufanya invasive therapy kwasababu ni nje ya wigo wao(isipokuwa simple procedure kwa AMO)

Ikitokea Medical officer anafanya kazi hiyo, naye anaweza kukutana na kikwazo.
Kwanza, atategemea history na clinical examination na pengine ku opt Laparotomy.

Hapo inaweza kumlazimu atafute Obstetric and Gynaecology (OBGY) specialist aje kutoa ushauri au kufanya complicated procedure kama Hysterectomy ikitokea.

Je, specialists wa OBGY wapo wangapi mikoani?

Mfano wa pili, huko mikoani kuna archaic x-ray tech ambayo ina limitations nyingi katika diagnosis. Ni Hospitali ngapi za mikoa zina technology Zaidi ya hiyo?

Hoja hapa ni kuwa kupandisha hadhi hospitali kwa matamko ya kisiasa ni kutoa 'false hope' Ukweli,Hospitali za mikoa hazina hadhi hiyo, na kuzipa hadhi ni kuwadanganya wananchi.Ni kuwa limiti wasipate huduma haswa za hadhi ya referral hospital.
Ni kuwanyima accessibility kwa kuwadanganya

Kumbuka, Hospitali za mikoa zinapata mgao wa resource kama za rufaa, je ni kipi bora, kuziimarisha katika huduma au kuzipandisha hadhi ili zi compete na referral Hospital katika limited resources tulizo nazo zikitoa huduma below stnd?

Nikusikilize kwanza
 
Lakini cha ajabu ni kwamba, zaidi ya 70% ya vifo vinavyowamaliza watanzania vinatokana na magonjwa yanayotibika, tena bila ya ulazima wa kufuata huduma kwenye referral and specialty hospitals. Magonjwa hayo yanaweza kutibika na hata kuepukika kabisa iwapo ngazi za chini zitapatiwa vitendea kazi, madawa na wataalam wa kawaida.
Na hapa ndipo hoja ilipo, kwamba, kutengea bajeti kubwa kwa referral hosp ni ku invite more problems badala ya kuzuia

Primary healthcare ni muhimu sana, kwamba kinga na kuzuia magonjwa yanayouzilika pengine bila matibabu. Hivi kwanini referral Hospital itibu magonjwa ya mlipuko?

Mfano, measles inazuilika kwa proper vaccination, the likes of Diphtheria and Polio.
Kwamba, single shot of DPT inaweza kuzuia vifo vingi na kupunguza 'resource strains' katika referral hospitals.
 
Pamoja na kukusihi usome bila 'prejudice' kuona hoja za wengine, napenda nikujibu swali lako kama ifuatavyo

1. Endapo kupandisha hadhi za hospitali hakuna effect katika accessibility ya huduma za afya, basi haingekuwa na maana ya kuzipandisha hadhi! Hii ni kwa mujibu wako

2. Kupandisha hadhi ya hospitali ni suala la kitaalamu likizingatia vigezo vinavyopaswa.
Miongoni mwa vigezo hivyo, ni wataalam hasa specialists na vifaa.

Si jambo la kisiasa, kuamka asubuhi na kutangaza Hospitali X ni ya rufaa kama tawi la chama kuwa ofisi ya mkoa asubuhi moja kwa matakwa ya kisiasa

Huduma zetu kama alivyosema Mchambuzi ni primary , secondary na tertiary. Tetiary ndiyo referral hospital.

Utakubaliana nami ya kuwa Hospitali za mikoa hazina hadhi ya kuwa referral

a)Hazina wataalamu wa kuzi qualify kama referral Hospitals
b)Hazina vifaa vnavyoweza kukidhi haja ya referral hospital

Mgonjwa akitoka kituo cha afya kwenda Hospitali ya Wilaya, likely atakuwa na referral ya Clinical Officer. Huko Wilayani atakutana na Assistant Medical office (AMO).
Naye anaweza kumfanyia referral Hospitali ya mkoa. Hapo ndipo tatizo lililpo

Hospitali za mikoa bado zina upungufu wa Medical officers( Dr) na mgonjwa atapata huduma ya Clinical officer au AMO na kwa bahati Dr. Hakuna Specilists

Hata kwa zile zenye Specialists, bado wanafanya 'clinical work' kwasababu hawana vifaa vya kuwawezesha kutenda kazi zao.

Mathalani, mgonjwa aliyepewa referral kwa matatizo ya maumivu makali ya tumbo akiwa mja mzito, kuna differential diagnosis nyingi nyuma yake
Inawezakana kuwa ni ruptured appendicitis au ectopic pregnant

Huko mikoa X-ray hazifanyi kazi na haziwezi kutoa diagnosis kwasababu kazi yake ni imaging, na inapokuwa suala la soft tissue ni useless.
Vifaa vinavyoweza kutoa mwanga au diagnosis ni kama Ultra sound au MRI.

Hospitali ngapi zina vifaa hivyo nchini achilia za mikoa?

Wataalam katika ngazi ya Clinical officer au AMO hawana uwezo wa kufanya invasive therapy kwasababu ni nje ya wigo wao(isipokuwa simple procedure kwa AMO)

Ikitokea Medical officer anafanya kazi hiyo, naye anaweza kukutana na kikwazo.
Kwanza, atategemea history na clinical examination na pengine ku opt Laparotomy.

Hapo inaweza kumlazimu atafute Obstetric and Gynaecology (OBGY) specialist aje kutoa ushauri au kufanya complicated procedure kama Hysterectomy ikitokea.

Je, specialists wa OBGY wapo wangapi mikoani?

Mfano wa pili, huko mikoani kuna archaic x-ray tech ambayo ina limitations nyingi katika diagnosis. Ni Hospitali ngapi za mikoa zina technology Zaidi ya hiyo?

Hoja hapa ni kuwa kupandisha hadhi hospitali kwa matamko ya kisiasa ni kutoa 'false hope' Ukweli,Hospitali za mikoa hazina hadhi hiyo, na kuzipa hadhi ni kuwadanganya wananchi.Ni kuwa limiti wasipate huduma haswa za hadhi ya referral hospital.
Ni kuwanyima accessibility kwa kuwadanganya

Kumbuka, Hospitali za mikoa zinapata mgao wa resource kama za rufaa, je ni kipi bora, kuziimarisha katika huduma au kuzipandisha hadhi ili zi compete na referral Hospital katika limited resources tulizo nazo zikitoa huduma below stnd?

Nikusikilize kwanza

Attached ni takwimu ambazo zinaweza kutoa mwanga juu ya human resource levels nchini. Ni takwimu za 2002. Naandaa takwimu za kipindi cha hivi karibuni zaidi, nitaziwasilisha.
 
Attachments

  • afya stats.docx
    15.7 KB · Views: 2
Nguruvi3, attached ni takwimu za work force in the health sector kwa mwaka 2014. Ingawa kwa ujumla wake idadi imeongezeka ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2002, lakini bado hatuoni matokeo chanya kwenye PHC.
 
Attachments

  • takwimu HR afya 2014.docx
    16.9 KB · Views: 5
Naomba mniwie radhi kwamba majedwali niliyowasilisha katika bandiko la msingi tarehe 12 Mei 2016 ambayo yalibeba takwimu mbalimbali hayakutoka vizuri. Nawasilisha tena kama 'attachments' hapo chini.

Kama tulivyojadili awali, mikopo ya nje yenye gharama na pia masharti nafuu ni “Concessional loans” kwa maana ya very low interest rates, fixed interest rates, long grace period and debt maturity. Kwa miaka mingi (1970s – late 2000s) sehemu kubwa ya deni la nje ilitokana na vyanzo hivi vya mikopo. Lakini kwa miaka sita sasa, vyanzo hivi vya mikopo vimeendelea kupungua kwa kasi. Hii inatokana na wahisani kuamua kujiondoa pole pole kwa sababu mbalimbali, ikiwepo ile ya walipa kodi katika nchi zao kutoridhishwa na kasi ya kupungua kwa umaskini nchini Tanzania, lakini pia kutokana na ongezeko la mahitaji ya ndani/kikanda kwa nchi wahisani.

Pamoja na vyanzo hivi vyenye gharama na pia masharti nafuu kuendelea kupungua, deni la nje limeendelea kukua kwa kasi kubwa na sehemu kubwa ya mikopo mipya imekuwa ikitokea kwenye vyanzo vyenye masharti ya kibiashara kwa maana ya high interest rates, variable interest rates, shorter grace period, shorter debt maturity. Kwa mfano, tukitazama jedwali #1 hapo chini, ndani ya kipindi kifupi sana (2010-2015), concessional lending zimepungua kutoka 86% ya deni lote la nje na kufikia 60%, huku ‘non-concessional lending’ (yani commercial banks and Export Credit Agencies) zikiongezeka kutoka 2.55% ya jumla ya deni lote la nje(2010) na kufikia 32% (mwaka 2015).

Pia Gazeti la ‘The Citizen’ la tarehe 16 March 2016, liliripoti taarifa kutoka Exim India kwamba serikali ya Tanzania inatarajia kukopesha Dola za Kimarekani Bilioni KUMI kutoka Exim India kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu. Jumla ya mkopo huu unatarajiwa kuwa ni Dola za kimarekani Bilioni 10.4, sawa na takriban TZS 23 trilioni. Kati ya hizi, Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) peke yake linatarajia kuchukua jumla ya TZS Trilioni 6.2 kwa ajili ya miradi yake ya ujenzi wa makazi arusha, kigamboni city na DSM. Hili ni janga!
 
Attachments

  • Jedwali#1 - Mgawanyiko wa Deni la Nje According Creditors.docx
    17 KB · Views: 5
  • Jedwali #2-Gharama na Masharti ya Mikopo ya nje pamoja na orodha ya wakopeshaji wakubwa.docx
    15.7 KB · Views: 2
Jedwali #3 hapo chini linaonyesha “Cost of debt” (Gharama za mkopo wa nje).

Tunaona kwamba Weighted Average Interest Rate (wastani wa riba) kwa mwaka 2010 ulikuwa ni 0.4%. Wastani huu uliongezeka hadi 1.9% miaka mitano baadae (2015), ikiwa ni ongezeko la karibia mara tano. Tukumbuke kwamba sehemu kubwa ya ongezeko hili ni la mikopo ambayo vyanzo vyake ni vya kibiashara kuliko ‘concessional’.

Refinancing Risk

Deni linaloiva katika kipindi cha mwaka mmoja kati ya deni lote kwa mwaka (2015) ilikuwa ni 4.7%, ikilinganishwa na mwaka 2010 ambalo ilikuwa ni 6.2% ya jumla ya deni lote kwa kipindi hicho. Hili ni punguzo la 1.5%. Kwa kuangalia juu juu inaonekana walipa kodi wamepata ahueni lakini uhalisia haupo hivyo. Jumla ya deni la nje (2010) ilikuwa ni takribani TZS 6.7 trilioni. Kwa maana hii, deni lililokuwa linaiva ilikuwa ni jumla ya TZS takribani 415 billioni. Kwa mwaka 2015, deni la nje lilifikia takribani TZS 25 trilioni. Kwa maana hii, deni lililokuwa linaiva ilikuwa ni karibia TZS 1.2 trilioni. Kwahiyo wakati kulikuwa na punguzo la 1.5% katika kipindi hicho, kwa upande wa fedha za walipa kodi, kulikuwa na ongezeko la zaidi ya TZS trilioni moja. Rejea mjadala wa refinancing risk huko juu.

Interest rate risk

Kufikia mwaka 2010, jumla ya deni ambalo lilikuwa linahitaji ‘refixing of interest rate’ kutokanana kuiva ilikuwa ni 6.2% ya jumla ya deni lote. Hii ilikuwa ni sawa na karibia TZS 415 billion. Kufikia mwaka 2015, kiwango hiki kilifikia 23%, ambayo ilikuwa ni sawa na karibia TZS trilioni 6 (trilioni sita). Tukirejea mjadala wa awali juu ya gharama/hatari ya ‘roll over of debt’, maana yake ni kwamba kufikia kipindi husika, TZS karibia trilioni Sita zilikuwa zinasubiri kuwa rolled over kwa riba ya juu zaidi kuliko awali wakati mikopo husika ilipochukuliwa na serikali.
 
Attachments

  • Jedwali#3 - Costs and Risks Indicators (deni la nje).docx
    15.4 KB · Views: 1
Kutokana na mzigo mkubwa Wa Deni la Taifa, Je Serikali ya JPM italazimika kuchapisha fedha mpya?

Serikali ya awamu ya tano inakabiliwa na changamoto kubwa. Mojawapo ni matarajio makubwa kutoka kwa wananchi kwamba Serikali ya JPM ni serikali ya “Mabadiliko ya Kweli” katika maisha yao, hasa kiuchumi na kijamii. Lakini uhalisia wa mambo unazidi kutuonyesha kwamba matarajio haya yanaweza kuota mbawa kutokana na mzigo mkubwa wa deni la taifa. Kwa mfano katika mjadala wetu tuliona jinsi gani serikali ya awamu ya tano tangia iingie madarakani imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi zinazokusanywa kila mwezi kulipa deni kubwa la taifa linaloendelea kuiva, badala ya fedha hizi kwenda kugharamia miradi ya maendeleo kwa lengo la kuboresha maisha ya walipa kodi/wananchi.

Vyanzo vya fedha kutoka nje ya nchi vinazidi kukauka, lakini pia vyanzo vya ndani navyo havitoshi, je Serikali itachukua uamuzi wa kuchapishwa fedha ili kupunguza mzigo wa deni la taifa na vile vile kugharamia miradi ya maendeleo kuboresha maisha ya wananchi?

Kutokana na changamoto tajwa, Serikali inaweza kuwa ‘tempted’ kuchapisha fedha mpya. Iwapo itachukua uamuzi huo, ifahamike kwamba uamuzi huo hautaongeza national/economic output kwa namna yoyote vile, badala yake itapelekea mfumuko wa bei, suala ambalo litazidi kuongeza gharama za maisha kwa wananchi. Tutumie mfano wa mazao ya Kilimo. Tuseme uchumi wetu unazalisha mazao ya chakula yenye thamani ya TZS trilioni 15 na serikali inaamua kuchapisha fedha mpya. Kitachotokea ni kwamba, uchumi utakuwa na kiasi kile kile cha bidhaa za vyakula, lakini wananchi watakuwa na fedha nyingi zaidi mikononi (mzunguko wa fedha katika uchumi utaongezeka) dhidi ya kiasi kile kile cha biadhaa za vyakula. Kwa vile uchumi utakuwa na fedha nyingi zaidi zikifukuzia bidhaa chache, mahitaji makubwa ya wananchi yatalazimisha bei ya bidhaa/ vyakula kuongezeka (mfumuko wa bei).

Kwahiyo kuchapisha fedha mpya kutapelekea wananchi kuwa na fedha nyingi zaidi mikononi lakini kwa vile hali hii pia itapelekea kupanda kwa bei za bidhaa, kuwa na fedha nyingi zaidi mikononi hakutapelekea maisha ya wananchi kuwa bora zaidi, badala yake, gharama za maisha zitaongezeka zaidi.
 
Waziri Muhongo: Miradi ya Umeme IPTL, Songas na Symbion haina tija kwa taifa.

Hatimaye Waziri wa Nishati na Madini ametamka kile kile ambacho tulikisema katika bandiko letu. Akiwa anawasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha, Waziri Muhongo alieleza wazi jins igani miradi ya umeme ya IPTL, Songas na Symbion ilivyokuwa ni jipu. Tulijadili suala hili katika sehemu ya tano ya uzi huu.

Tulijadili kwa kina kwanini kama taifa, tuna haja ya kuwa waangalifu na miradi ya aina hii, hasa kwa sababu serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutekeleza miradi mingi ya miundo mbinu ya aina mbalimbali pamoja na ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa njia hii (PPPs).

Tofauti na Waziri Muhongo ambae yeye aligusia tu sekta yake (Nishati), huku akiacha kueleza kwa undani juu ya matatizo yatokanayo na miradi ya PPP, katika mjadala wetu tulijadili suala hili kwa mapana na marefu zaidi, hasa tukieleza jinsi gani miradi ya PPP ni jipu. Katika mjadala wetu, tulisema kwamba Ubia Wa Sekta ya Umma na Binafsi – Public – Private Partnerships (PPPs) una athari kubwa kwa walipa kodi/Deni la Taifa.

Tukajadili kwamba - Miradi ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi - Public – Private Partnerships (PPPs) huchukua sehemu kubwa sana ya uwekezaji wa sekta ya miundo mbinu. Miundo mbinu ni pamoja na ile ya mawasiliano (telecommunications), nishati, bandari, barabara, reli, maji nk. PPPs zimeendelea kupata umaarufu mkubwa kwa sababu zinawezesha ‘debt repayments’ za nchi kutoonekana kwa urahisi kwa wananchi na hata kwa wawakilishi wao bungeni. Miongoni mwa PPP schemes maarufu ni pamoja na “The Private Finance Initiative” ya Uingereza.

Taasisi za aina hii zinasaidia sekta binafsi kutoka mataifa makubwa kuwekeza katika nchi maskini lakini kwa masharti kwamba serikali za nchi maskini zitoe ‘guarantee’ ya malipo kwa wawekezaji bila ya kujalisha hali ya uchumi itageuka vipi baade. Pia serikali za nchi maskini hutakiwa kujifunga (commit) ‘to bail out the private operator’ kama biashara itakwenda kombo. Kwa namna hii, PPPs zinakuwa na athari ile ile kwenye fiscal system ya nchi kama ilivyo kwa mikopo kwa sababu kimsingi serikali bado inakopa moja kwa moja, lakini tofauti na mikopo mingine, ‘payment obligations’ za serikali under PPP projects huwa hazionyeshwi kwenye takwimu za deni la nje la taifa.

Miradi ya PPP kwa kawaida hugharimu zaidi serikali kuliko ambavyo serikali ingeamua kukopesha yenyewe kutoka vyanzo vingine na kuwekeza katika miradi hiyo hiyo kwa mfano ujenzi wa miundo mbinu nk. Hii ni kwa sababu mikopo hii inatoka kwenye sekta binafsi, na kama tulivyojadili awali, ni mikopo yenye vyanzo gharama kubwa, na ukiachilia gharama zinazohusiana na viwango vya riba, pia private contractors huwa wanahitaji faida kubwa sana na vile vile ‘negotiations’ mara nyingi huwa zinapendelea sekta binafsi kuliko serikali husika.

Kwa mujibu wa utafiti wa Griffiths et al (2014), [“Financing for development post 2015: Improving the contribution of Private Finance”]:

“PPPs are the most expensive way for governments to finance infrastructure, ultimately costing more than double the amount than if the investment had been financed with bank loans of bond issuance”.

Katika hili, Mchumi Maximilien QueyRanne kutoka dawati la “Fiscal Affairs” la Mfuko wa kimataifa wa fedha (IMF), anaongeza kwamba:

“The fiscal risks of PPPs are potentially large because they can be used to move spending off budget and bypass spending controls and move debt off balance sheet and create contingent and future liabilities. They also reduce budget flexibility in the long term.”

World Bank pia kupitia utafiti wake huru hivi karibuni (World Bank’s independent evaluation Group) ilibaini kwamba kati ya miradi 442 ya PPP iliyo chini ya uangalizi wake, tathmini ya athari za miradi hii katika kutokomeza umaskini ilifanyika kwenye miradi tisa tu (sawa na 2%). Vile vile, tathmini juu ya ‘fiscal impact’ ya miradi hii ya PPP ilifanyika kwenye miradi 12 tu (sawa na 13%). Pamoja na haya yote, cha ajabu ni kwamba ‘debt payment obligations’ zinazotokana na miradi ya PPP bado huwa haipo covered katika ‘Debt Sustainability assessments’ zinazofanywa na World Bank/IMF. Maana yake ni kwamba, uhalisia juu ya obligations za malipo ya mbeleni ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha za walipa kodi kuliko kile kinachowasilishwa kwenye ‘Debt Sustainability assessments.’

Tukatolea mfano wa Sekta ya Nishati ambapo tulisema kwamba - Serikali ya Tanzania ina ‘three hidden obligations’ zilizotokana na mikataba ya nyuma ya PPP. Miradi hii ni ya Umeme ambayo ilikua implemented kwa ajili ya kuiuzia serikali (Tanesco) umeme ‘at a pre-determined price’, ambayo ni guaranteed na serikali ya Tanzania (Kodi za wananchi). Mradi wa kwanza ulikuwa ni IPTL, na mradi wa Pili uliofuatia ukawa ni ule wa Songas. Majipu makubwa!

Kwa mujibu wa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) mwaka 2007/2008, miradi hii miwili ilikuwa inaigharimu Tanesco 90% ya mapato yake na kufanya Tanesco kulemewa na mzigo mkubwa wa purchase agreements ambazo hazikuzingatia Public Procurement ACT pamoja na regulations zake. Lakini kama vile hiyo haitoshi, bado serikali ya ikaingia mkataba na Kampuni nyingine ya Richmond/Symbion/Dowans mwaka (2007/2007).

Kutokana na kulemewa na miradi hii ya kinyonyaji, mwaka 2009 Tanesco ililazimika kuongeza ‘tarrifs’ kwa 40%, lakini bado shirika hili likaendelea kujiendesha kwa hasara. Kwa mujibu wa ripoti ya IMF (2013), ruzuku ya serikali kwa tanesco iligharimu serikali 10% ya fedha za walipa kodi, na sehemu kubwa ya fedha hizi zilienda kulipia ‘inflated costs’ za miradi hii ya PPP ya uzalishaji wa umeme. Kwa maana hii, ruzuku ya serikali (10% ya kodi za wananchi kila mwezi) ilikuwa ni ruzuku kwa makampuni binafsi yaliyowekeza kupitia PPPs, na sio ruzuku kwa walipa kodi, ambao ndio wanaostahili kufaidika na ruzuku husika. Kwa mfano, inasemekana kwamba malipo ya fedha za walipa kodi kwenda IPTL ni TZS bilioni nane kwa mwezi.
 
Pamoja na kukusihi usome bila 'prejudice' kuona hoja za wengine, napenda nikujibu swali lako kama ifuatavyo
Unaweza ku-access hospitali ya wilaya au mkoa hata kama una mafua. So a dispensary is a subset of a District Hospital.
Kuhusu kuelekeza mafungu dispensary, local governments huwa zinaharibu kwa sababu pesa nyingi huishia wilayani (according to research by WHO/Africa).
Hospitali za mkoa na taifa ndiyo zipo directly controlled na Wizara pamoja na Ofisi ya Rais tawala za mikoa.
Hospitali za wilaya kwenda chini zipo chini ya halmashauri. Kwa hiyo ukimwona kijana Nasari ananunua vitanda Guangzhou ujue yupo kwenye capacity ya Ditrict/municipal council. kitaifa huwa wanapata pande la bima ya taifa (marejesho) na takrima kidogo.
Kwa hiyo serikali kupandisha hadhi hospitali ya wilaya ni sawa na kuizidishia uwezo na mafungu ya fedha, na hufanywa kufuatia utafiti. Toa research paper links.
Mimi nakuambia soma researches za Twaweza tu, utapata mwnga Fulani.
It's not about prejudice, it's about writing things without listing credible sources ... now, that is very prejudicial.
 
Listing credible things ni muhimu, lakini kwa wengine tunaishi 'we live in'. Tumeyaona na kuyatenda kwa mikono na macho yetu, tunajua tunaaandika nini wala si kutegemea Twaweza wanaokusanya takwimu kutokwa kwetu!

Nikikuambia DPT/Measles vaccine najua kuanzia Sanofi/GSK hadi inaingi katika jokofu la mafuta Pale Nakapanya, Mkirira, Malinyi, Katoma,Busega au Mkuzi.

Nafahamu supply chain yake ipoje, nani ana fund kiasi gani na kwa muda gani

Nikukueleza AMO anafanya CS au Hydrocelectomy najua anafanya katika mazingira gani, ni procedure gani ina ukubwa gani na complicated kiasi gani

Nikikueleza MD anafanya Laparatomy najua ni kitu gani, kinafanyikaje, kinatumia nini na kina gharama gani

Nikueleza specialist( OBGY) anafanya Hysterectomy najua nazungumzia nini

Mkuu, nikiandika X-ray, ultra sound au CT scan najua ni kitu gani kinafanya nini katika mazingira gani na limitations zake n.k.

Ukiingia kwa Graham stain au Florence Nightingale tutaongea kwa lugha njema kabisa kama unaifahamu

Ndiyo maana nakuambia naifahamu system yetu kuanzia zahanati hadi referral level si kupitia Twaweza, nimeishi katika hilo and I know it !

Sijengi hoja za Twaweza , huko ni kwako!
Tunazungumzia WHO inside siyo kwa kusoma abstract!

Ukiona tunaandika lugha rahisi , lengo ni umma uelewe, ndilo la muhimu.

Mifano tukitoa ni lazima ilingane na umma unavyoelewa na kuishi

Mkuu tumeshuhidia watoto wakipoteza maisha mikononi mwetu kwasababu unazoweza kulia ukisikia. Nikisema measles I mean it!

Tumeshuhudia akina mama wakipoteza maisha kwa tofauti ya dakika 15.

Tumeshuhudia wazee wakipoteza maisha kwa sababu tu ya oxygen tank.

Mkuu usitukumbushe machungu kwa habari za Twaweza

Kwa hili nitendee haki, tujadiliane kwa nidhamu!
 
  1. Listing credible things ni muhimu, lakini kwa wengine tunaishi 'we live in'. Tumeyaona na kuyatenda kwa mikono na macho yetu, tunajua tunaaandika nini wala si kutegemea Twaweza wanaokusanya takwimu kutokwa kwetu!
Nikikuambia DPT/Measles vaccine najua kuanzia Sanofi/GSK hadi inaingi katika jokofu la mafuta Pale Nakapanya, Mkirira, Malinyi, Katoma,Busega au Mkuzi.

Nafahamu supply chain yake ipoje, nani ana fund kiasi gani na kwa muda gani

Nikukueleza AMO anafanya CS au Hydrocelectomy najua anafanya katika mazingira gani, ni procedure gani ina ukubwa gani na complicated kiasi gani

Nikikueleza MD anafanya Laparatomy najua ni kitu gani, kinafanyikaje, kinatumia nini na kina gharama gani

Nikueleza specialist( OBGY) anafanya Hysterectomy najua nazungumzia nini

Mkuu, nikiandika X-ray, ultra sound au CT scan najua ni kitu gani kinafanya nini katika mazingira gani na limitations zake n.k.

Ukiingia kwa Graham stain au Florence Nightingale tutaongea kwa lugha njema kabisa kama unaifahamu

Ndiyo maana nakuambia naifahamu system yetu kuanzia zahanati hadi referral level si kupitia Twaweza, nimeishi katika hilo and I know it !

Sijengi hoja za Twaweza , huko ni kwako!
Tunazungumzia WHO inside siyo kwa kusoma abstract!

Ukiona tunaandika lugha rahisi , lengo ni umma uelewe, ndilo la muhimu.

Mifano tukitoa ni lazima ilingane na umma unavyoelewa na kuishi

Mkuu tumeshuhidia watoto wakipoteza maisha mikononi mwetu kwasababu unazoweza kulia ukisikia. Nikisema measles I mean it!

Tumeshuhudia akina mama wakipoteza maisha kwa tofauti ya dakika 15.

Tumeshuhudia wazee wakipoteza maisha kwa sababu tu ya oxygen tank.

Mkuu usitukumbushe machungu kwa habari za Twaweza

Kwa hili nitendee haki, tujadiliane kwa nidhamu!
Hapo ndipo unapokosea. Hapo ndio prejudice inapotokea.
Kuaminisha watu ni kazi rahisi. You are basically disseminating opinions. Which is a wrong precedent kwa sababu hujafanya utafiti.
Kuna watu wamefanya utafiti na wameelezea utafiti wao wameufanyaje.
It's s simple, tunazungumzia allocation of funds kwenye dispensaries na clinics.
That is simply a local government issue.
Hospitali za mikoa na Taifa, hiyo ni central government issue.
When you try to move funds to local governments, lazima uhamishe sources too. Sasa kama dispensaries za ukerewe zinapitwa na za Mkuranga (Mkuranga has better dispensaries) hilo ni suala LA councils za LGAs.

Sometimes tunachanganya mambo.

System iliyopo imegawanyika sehemu mbili, Central na Local in terms of governance. Ukizungumzia funding make sure governance inakuwa included.
Don't demand a government that can't fund itself. Blame it on the local govt. Some are doing way better.
Central government na dispensaries have minimal relationship.
Ni hilo tu mkuu, tunachanganya mambo.
Ukiwa na mafuta unaweza kwenda Mwananyamala, ipamba. Mwamama alitaka kujifungua Mount Meru, Patandi, Hindu Mandal au Hata home hakatazwi. So simply because hospitali ni ya mkoa haimaanishi huwezi kwenda bila kibali.

Don't force me or assume that nitakuamini wewe by just claiming that you know things .... Nah! Hatuendi hivyo.
 
Hoja nzuri, swali , unawezaje kutenganisha majukumu ya central gov na local gov ikiwa wizara inayoshughulikia local gov ipo chini ya central gov directly

Pili, huoni kwa muktadha huo twakimu za Mchambuzi zina make sense ingawa unaziponda?
 
Unaweza ku-access hospitali ya wilaya au mkoa hata kama una mafua.
Unaweza kutusaidia na takwimu kuhusu idadi ya wananchi wanaoenda kwenye hospitali za wilaya na mikoa kutibiwa mafua?

Kuhusu kuelekeza mafungu dispensary, local governments huwa zinaharibu kwa sababu pesa nyingi huishia wilayani (according to research by WHO/Africa).

Pesa nyingi ni kiasi gani cha jumla ya bajeti? Na ni asilimia ngapi ya mahitaji ya afya katika ngazi husika? Unaweza kutuwekea hiyo research hapa tuelewe kwa undani?

Hospitali za mkoa na taifa ndiyo zipo directly controlled na Wizara pamoja na Ofisi ya Rais tawala za mikoa.
Hospitali za wilaya kwenda chini zipo chini ya halmashauri. Kwa hiyo ukimwona kijana Nasari ananunua vitanda Guangzhou ujue yupo kwenye capacity ya Ditrict/municipal council. kitaifa huwa wanapata pande la bima ya taifa (marejesho) na takrima kidogo.
Kwa hiyo serikali kupandisha hadhi hospitali ya wilaya ni sawa na kuizidishia uwezo na mafungu ya fedha, na hufanywa kufuatia utafiti. Toa research paper links.
Mimi nakuambia soma researches za Twaweza tu, utapata mwnga Fulani.
It's not about prejudice, it's about writing things without listing credible sources ... now, that is very prejudicial.

Je unazungumziaje suala la 'disbursements' of funds? Kwa sababu suala hili lina athiri the efficient use of limited funds. Nyakati zote, Wizara ya fedha/Hazina hutoa less than approved budgets; Sekta ya afya inakabiliwa na tatizo kubwa la irregular disbursements; Pia huwa inachukua muda mrefu sana kabla ya fedha zilizotolewa kufikia kwenye health facility accounts, kwa mfano MSD. Kwanini?

MSD inakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha kwa sababu ni kawaida kwa serikali pengine to assume kwamba vifaa au dawa zikifika kutoka nje (MSD is largely donor funded), tatizo limeisha. Lakini huwa tunasahau juu ya umuhimu wa 'working capital' for MSD, hasa distribution costs for externally financed products. Dawa zikifika, nani anagharamia usambazaji wake? Definitely not donors, huo ni wajibu wa serikali, na huwa haitimizi wajibu wake huu ipasavyo. Limited cash flow at MSD inaathiri sana stock levels pamoja na fulfilment rates kwa madawa na vifaa vingine.

Vile vile tukumbuke kwamba uwezo wetu kama taifa wa kutengeneza dawa haukidhi mahitaji ya nchi. Uzalishaji wa ndani unakidhi mahitaji ya ndani kwa 30% tu, the deficit inakuwa covered na dawa kutoka nje ya nchi. Hapa tunajiuliza, je fedha nyingi za bajeti kwenda kwenye upper tier kwa justifications za research and development, kwanini hatuoni matokeo yake? Bajeti za kila mwaka katika hili huwa zinaenda kufanya nini? Kama ni kweli zingekuwa zinatumika on research and development, matokeo yake tungeyaona katika quality and quantity of drugs manufactured in the country.

Hapo chini pia nime 'attach' takwimu zinazoonyesha health expenditures kwa kipindi cha 2001-2012. Katika figure (1) tunaona kwamba karibia 50% ya matumizi katika sekta hii yanategemea donors (wahisani), ambao serikali ya CCM imekuwa ikiwapiga vijembe kwamba 'hatuwahitaji", kufuatia sakata la Uchaguzi Zanzibar na Sheria Kandamizi ya mtandao. Vile vile tunaona jinsi gani serikali imakuwa ikisua sua katika kuchangia matumizi kwa ajili ya sekta hii muhimu ya Afya ambapo katika kipindi husika, matumizi ya serikali katika sekta hii ni kidogo kuliko matumizi ya wananchi. Tunaona pia sekta binafsi ikiwa na mchango mdogo sana, usiovuka 5%.

Katika figure (2), tunaona jinsi gani Kobello anavyotudanganya pale anaposema kwamba fedha nyingi zinaishia wilayani. Tunaona kwamba Local Government Authorities matumizi yake kwenye sekta ya afya hayavuki 15% ya matumizi yote. Out of pocket expenditures (fedha za mifukoni mwa wananchi) zinabeba sehemu kubwa ya matumizi (wastani wa karibia 30%), huku Central government kupitia Wizara ya Afya ikifuatia (wastani wa takribani 27%). Mfuko wa Bima wa taifa (NHIF) mchango wako bado ni mdogo sana, haufiki hata 5%.
 
Attachments

  • Figure 1 - Total health expenditure by financing source.docx
    13.3 KB · Views: 1
  • Figure 2 - Total health expenditure by financing source.docx
    13.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom