Magori, Rage, Madega, warudishwa TFF

Mfumwa

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
1,456
42
Magori, Rage, Madega, warudishwa TFF
William Mjema
Daily News; Saturday,January 31, 2009 @21:15

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana lilitangaza kamati ndogo ndogo za shirikisho hilo huku baadhi ya wanamichezo waliopata kuongoza shirikisho hilo miaka ya nyuma wakirudishwa.

Pia katika kamati hizo yupo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow na Makamu wa Pili wa Rais wa TFF wa zamani Ismail Rage, ambaye pia amepata kuwa Katibu Mkuu wa TFF wakati huo ikiitwa FAT.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, alisema majina hayo yalipitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana jana, ambapo pia kulingana na Katiba ya TFF, inampa Rais wa Shirikisho hilo, uwezo wa kuteua majina mawili ya wanamichezo wa kuingia kwenye Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo.

Alisema kutokana na hali hiyo Rais wa TFF, amewateua aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho hilo, Crescentius Magori na mwanasheria wa TFF, Alex Mgongolwa kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo.

Katika kamati hizo ndogo, Kamati ya Fedha na Mipango Mwenyekiti atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Athumani Nyamlani, wakati Makamu Mwenyekiti ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Amir Roshan, wajumbe ni Samuel Nyalla,
Eliud Mvella, Andrew Sikoko, Yakub Kidula na Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan.

Kamati ya Mashindano itaongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Ramadhan Nassib, Makamu wake atakuwa Wallace Karia, wakati wajumbe ni Lawrance Mwalusako, Said George, Ahmed Yahaya, Leopold Tasso na Salum Chambuso.

Mwakalebela alisema Kamati ya Ufundi itaongozwa na Teofrid Sikazwe, ambapo Makamu wake ni Khalid Mohammed, wajumbe ni Joseph Mapunda, Charles Boniface, Elizabeth Kalinga, Charles Masanja na Arthur Mwambeta.

Kamati ya Soka la Vijana itaongozwa na Ahmed Mgoyi, ambapo Makamu ni Athumani Kambi wakati wajumbe ni Ally Mtumwa, Daudi Yassin, John Mwangakala Charles Mbuge na Aaron Sokoni, huku Kamati ya Soka ya Wanawake itaongozwa na Lina Mhando (Mwenyekiti), Haule Gervas (Makamu Mwenyekiti), ambapo wajumbe ni Grace Madereka, Furaha Francis, Teddy Mapunda na Josephine Kulwa.

Kamati ya Waamuzi Mwenyekiti ni Shaibu Nampunde, Makamu Mwenyekiti Stanley Lugenge, huku wajumbe wakiwa ni Omar Abdulkadir, Leslie Liunda na Soud Abdi, wakati Kamati ya Habari na Masoko Mwenyekiti atakuwa Crescentius Magori, Makamu William Khalaghe, wajumbe ni Amin Bakhressa, Boniface Wambura, Angetile Osiah, Mohammed Nassor na Philemon Ntahilaja.

Kamati ya Sheria, Maadili na Wachezaji, Mwenyekiti ni Alex Mgongolwa, Makamu Mwenyekiti Hussein Mwamba, wajumbe ni mjumbe wa zamani wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye hivi sasa ni Mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega, Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA), Venance Mwamoto,

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Omary Gumbo na Makamu wa Pili wa Rais wa zamani wa TFF, ambaye amepata pia kuwa Katibu Mkuu wa TFF wakati huo ikijulikana kama Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Ismail Aden Rage. Kamati ya Ukaguzi wa Ndani wa Hesabu Khalifa Mgonja (Mwenyekiti), Muhsin Balhabaou (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe ni Rwechungura King, Said Soud, Fabian Samo, Epafra Swai na Adam Brown.

Kamati ya Uchaguzi Mwenyekiti ni Deo Lyato, Makamu Mwenyekiti , Hamidu Mbwezeleni wajumbe ni Moses Kaluwa, Hassan Dyamwalle na Kitwana Manara. Mwakalebela aliwataja walioteuliwa katika Kamati ya Nidhamu, ambayo ni moja ya kamati maarufu sana ndani ya TFF na yenye kukabiliana na mikikimikiki mbalimbali ni Alfred Tibaigana (Mwenyekiti), Makamu Mwenyekiti ,

Mustafa Kambona, wajumbe ni Mussa Azzan ‘ Zungu’ ambaye ni Mbunge wa Ilala, Yussuf Nzowa, Jamal Bayser, ambaye amepata kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Kaimu Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Lloyd Nchunga na Mohamed Msomali. Kamati ya Rufaa itaongozwa na Profesa Mgongo Fimbo (Mwenyekiti),

Ong’wanuhama Kibuta (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe ni Iddi Kipingu, Mohamed Misanga ambaye pia ni Mbunge, Dk Mshindo Msolla, Henry Tandau na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow. Kamati ya Afya na Utabibu itaongozwa na Profesa Lawrence Museru, Makamu Mwenyekiti, Dk Slyvester Faya na wajumbe ni Anthony Ngome, Mwanandi Mwankemwa, Helen Semu Elias Maige na Joachim Mshanga.

Alhamisi wiki hii wakati akizungumza na waandishi wa habari, Tenga alisema baadhi ya wajumbe waliokuwapo kwenye kamati mbalimbali za TFF waliomba wapumzike, ingawa hakuwataja majina, lakini baadhi ambao hawapo katika kamati ni Said el Maamry aliyekuwa Mwenyekiti Kamati ya Nidhamu, Jaji John Mkwawa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani. Tandau aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi yupo katika Kamati ya Rufaa akiwa mjumbe.
 
Perfect!!...wafanye kazi kazi sasa sio kuturudisha katika mambo ya waka 47...
 
Back
Top Bottom