Magonjwa ya Kurithi Yapatikanayo Katika Familia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078



Je, unajua historia ya magonjwa ya familia yako? Pengine unajua tu kuhusu mambo makubwa. Usishangae kwa mfano, kugundua kuwa nyanyako mkuu na dada zake watatu wote walikufa kutokana na saratani ya matiti, ingawa ugonjwa huu haukujitokeza kwa mama yako. Ama pengine unajua kuwa babako na ndugu zake wana ugonjwa wa Shinikizo la Damu mwilini na hujui iwapo ni la juu au la chini ama namna ugonjwa huu ulivyowaathiri.

Saratani ya Matiti

Wanawake walio hatarini kuupata ugonjwa huu ni:

  • Ajuza
  • Wenye asili ya kihindi au kizungu
  • Wanawake ambao washaugua saratani ya matiti mbeleni
  • Walio na jamaa wa karibu ( mama,dada,binti) ambao washawahi kuuguwa ugonjwa huu
  • Wanawake wenye hitilafu ya kinasaba kutoka kwa mzazi aliyeugua ugonjwa huu
  • Wanawake tasa au waliowapata watoto baada ya umri wa miaka 30.
  • Wanawake waliopata damu yao ya hedhi wakiwa na umri mdogo kabla miaka 12.
  • Wanawake waliokatika hedhi wakiwa wamechelewa baada ya miaka 50.
  • Wanawake wenye matiti makubwa(daktari anaweza kukuelezea baada ya uchunguzi wa mammogram)
  • Wanawake waliotumia tembe za uzazi,waliokosa kunyonyesha, wanaokunywa pombe kila siku,wanaonenepa sana baada ya kukatika hedhi,wanaomeza vidonge vya kubadilisha nasaba,na wale ambao hawakunyonyesha.
Dalili ya saratani ya Matiti:

  • Uvimbe kwenye matiti au kwapa
  • Mabadiliko katika umbo la matiti
  • Chuchu kutoa usaa ama titi kuwa nyororo
  • Chuchu kupotelea ndani ya matiti badala ya kujitokeza nje
  • Madutamaduta kwenye matiti kama yale ya maganda ya machungwa
  • Kubadilika kwa ngozi ya matiti na chuchu kuonekana zimefura
Ukiwa na mojawapo ya dalili hizi muone daktari,ni vyema kufanyiwa uchunguzi wa mammograms.
Fanyiwa uchunguzi wa matiti mapema ili kutambua saratani ya matiti mapema.Kujichunguza kila mwezi na kufanyiwa uchunguzi wa mammograms mara moja kwa mwaka hasa wanaozidi miaka 40 in bora.
 
Saratani ya kifuko cha mayai ya uzazi cha mwanamke.

Vifuko hivi ni viwili vidogo vilivyo kila upande wa mji wa mimba. Saratani hii huwaambukiza wanawake walio zidi umri wa miaka 50. Ni vigumu kuitambua kwa hivyo ni muhimu kumtembelea daktari wako kila mwaka kwa uchunguzi wa fupanyonga bila kujali miaka yako.
Baadhi ya mambo yanayowatia wanawake hatarini kupata saratani ya kifuko cha mayai ni:

  • Ikiwa mtu yeyote wakike katika familia (mama,dada,nyanya) amewahi kua nao huu.
  • Umri kuzidi miaka 50.
  • Ukiwa tasa.
  • Ikiwa umewahi kuwa na saratani ya matiti au utumbo mpaua
Wanawake hutambua ungonjwa huu kama umeshaenea sana.

Ishara zengine ni kama:

  • Maumivu tumboni kama uliyejawa na hewa tumboni.
  • Kuendesha au kufunga choo
  • Kutohisi njaa au kutokula vizuri
  • Kupoteza au kuongeza uzito bila kisababu
  • Kuvuja damu wakati haupo katika hedhi.

Dalili hizi zaweza kuwa kitu kingine, lakini ni vyema kuongea na daktari unapoziona.
 
Shinikizo la Damu Mwilini – Ukweli wa Mambo

Shinikizo la juu la damu mwilini ni nini?

Namna ambavyo damu yako hupiga kwenye ukuta wa mishipa ya mwili wako huitwa shinikizo. Kwa kawaida shinikizo la damu la mtu hupanda na kushuka siku nzima. Kwa wengine hubakia juu kila wakati. Hawa ndio watu walio na shinikizo la juu la damu mwilini au Hypertension.

Hali hii huweza kuathiri na kuharibu moyo wako, macho na figo. Huzidisha nafasi yako ya kushikwa na ugonjwa wa pigo (Stroke) au hata kushikwa na ugonjwa wa moyo.

Hivyo basi dalili zake ni nini?
Ugonjwa huu hujulikana kama "muuaji mnyamavu" kwa maana, mtu hukaa nao kwa miaka bila kujua. Njia ya pekee ya kujua iwapo una ugonjwa huu, ni kwenda kupimwa shinikizo lako la damu.

Nitazuiaje ugonjwa huu au hata kuutibu?

Jambo la kushangaza ni kuwa, hatua za kuchukua katika kuzuia shinikizo la juu la damu mwilini ni sawa na za kuutibu ugonjwa huu. Jambo muhimu sana ni kuhakikisha kuwa, unapimwa shinikizo lako angalau mara moja kwa mwaka na mhudumu wa kiafya aliyehitimu. Ni muhimu kwa sababu, kipigo cha damu cha mtu kwa kawaida huendelea kupanda maishani mwake. Njia nyingine ni pamoja na;

  • Kufanya mazoezi ya mwili ya mara kwa mara
  • Uepukane kabisa na kuvuta sigara na kulewa
  • Ule lishe bora lisilo na chumvi
  • Punguza uzani iwapo wewe ni mkubwa
 
Saratani ya Ngozi

Watu wengine wamo hatarini zaidi kupata saratani ya ngozi:

  • Walio weupe, na macho na ngozi ilio parara.
  • Walio na mabakabaka mwilini.
  • Wanaoishi sehemu ambayo kuna jua jingi.
  • Walio na maturuturu kutokana na miale ya jua.
Dalili za Saratani ya Ngozi ni nini?

  • Uvimbe au mabaka katika ngozi
  • Uvimbe katika ngozi usiopona
  • Katika hatua za mwisho unahisi mwasho, ngozi inayowaka moto na kutokwa damu.
Saratani ya ngozi inaweza kutibika ikitambulikana mapema. Hata wale wasiokuwa hatarini ya kupata saratani ya ngozi lazima watumie mafuta ya kujipaka ili kuzuia miale ya jua hasa kati ya saa 4 asubuhi na saa 9 mchana.
 
Kolestroli ya juu (High Cholesterol)
Unaweza kudhibiti hali hii kupitia kwa lishe bora iwapo mchunguzi hali hii na unaye mzazi au rafiki ambaye amewahi kupata ugonjwa wa moyo kabla afikie miaka 55 kuna uwezekano kuwa unaweza kupata ugonjwa huu. Hakikisha kuwa unakaguliwa kila mara.


Ugonjwa wa Sukari

Diabetes.jpg




Watu walio na ugonjwa wa Sukari (kama watu wale wengine) lazima watilie mkazo afya yao ya kila siku.Tofauti imo: walio na ugonjwa wa Sukari, kila siku lazima wapime sukari, wafanye mazoezi na wazingatie afya yao. Ikiwa wewe au mtu unayemjua ana ugonjwa wa Sukari na ameamua kuishi maisha yenye afya, basi Sehemu ya Kujifundisha itakuongezea maarifa kuhusu huu ugonjwa na kukuelekeza kuishi ukiwa na afya.
Hatua ya 1: Jifunze kuhusu ugonjwa wa Sukari
Ni vizuri kujua mambo mengi kuhusu ugonjwa wa Sukari ili uweze kuukimu. Hapa ni yale unayotakikana kujua na kufanya.
Jua ni aina gani ya ugonjwa wa sukari unayo na hatari zake


Usiogope kuuliza maswali na kujua pale utakapopata majibu.

Elewa kuhusu kiwango cha sukari damuni mwako na ni tiba ipi utakayo tumia.

  • Fanya mtihani mdogo kuhusu Insulini.
  • Insulini 101
  • Video: Insulini
  • Ugonjwa wa sukari: Kile unachohitaji.
  • Fungua uchapishe hati, inayokufundisha kufuatilia kiwango cha sukari damini yako.
Fungua uchapishe mpango wa afya nzuri waliye na Ugonjwa wa Sukari.

 
Glaucoma – Ugonjwa wa Macho
Iwapo katika familia yako kuna historia ya Glaucoma, kuna uwezekano mkubwa wako kuupata ugonjwa huu kwa sababu una uhusiano wa uzazi. Hali hii haitibiki kabisa lakini inaweza kuzuiliwa.

Majonzi na huzuni


Majonzi na huzuni ni nini?
Ni ugonjwa unaohusisha mwili, kupanda na kishuka kwa hisia za hasira na mawazo. Ni hali ambayo huwezi kuiondosha mbali kwani unashindwa kujizuia na hizi hisia.

Hakuna sababu moja kunayosababisha majonzi na huzuni mwingi. Hali hii hurithishwa katika historia ya familia. Hata wale ambao hii hali haijawahi kuonekana katika familia zao hujikuta nayo, taabu na dhiki za kupambana na maisha, mpenzi ama ugonjwa mkali. Watu wengine, hata madaktari, hudhani kuwa ni hali inayokumba tu watu wazee pekee la hasha.

Dalili

  • Kuhuzunika kila mara na kujiona bure
  • Kukosa shughuli na tama katika vitendo ulivyokuwa umenipenda hapo awali
  • Kuhisi kuchukizwa hata kwa jambo dogo
  • Kulia sana
  • Kuona hufai na kujihukumu huku ukijihurumia
  • Kulala sana ama hata kutolala kabisa
  • Kula sana au hata kuishindwa kabisa kula.
  • Kupata shida katika kufanya maamuzi au kufuatilia jambo
  • Kuwa na fikira za kutaka kujitia kitanzi au kufa.
  • Kulewa na kutumia dawa za kulevya.
Unaijuaje?
Ukihisi mojawapo ya dalili hizi kwa zaidi ya majuma mawili, ni muhimu upate usaidizi na kitaalamu. Huzuni ba majonzi huweza kutokea iwapo mtu ana shida ya kiafya, hasa kuna ugonjwa wa Sukari mwilini, ugonjwa wa moyo, kupata kipigo. Matibabu yanaweza kusababisha huzuni na majonzi pia. Ugonjwa wa kiakili na matumizi ya mihadarati, kupata nasaha bora na matibabu husaidia.

Unatibuje?
Iwapo kemikali katika ubongo wako hazitoshani unaweza kupata majonzi na huzuni kwa watu wengine, matibabu husaidia kwa wengine, nasaha bora huwasaidia. Kupata matibabu pamoja na nasaha bora huweza kutibu. Iwapo dawa au nasaha haisaidii endelea kujaribu hadi pale ambapo utapata tiba kamili. Watu tu baada ya majuma machache.
 
Alzheimer's/Dementia


Alzheimer's ni nini?
Ni mojawapo ya hali zinazo sababisha usahaulifu na kuchanganyikiwa. Huwashika sanasana wazee. Huwa wasahaulifu na mara nyingi huchanganyikiwa. Hali hii hutendeka wakati ambapo seli (cells) kwenye sehemu fulani za ubongo hufa.

Kinachosababisha hali hii hakijulikani hata hivyo, kuwa na hali hii huweza kusababishwa na ugonjwa wa Parkinson's, homa, ama hawili wa mtu unaposhindwa kukatiliana na dawa fulani. Dalili za Alzheimer's ni sawa na usahaulifu na kuchanganyikiwa lakini ni muhimu daktari wako akufanyie uchunguzi tofauti iwapo wewe ama mtu unayemjali ana huu ugonjwa.

Ni zipi baadhi ya dalili zake?

  • Kupoteza kumbukizi kwa muda kwa kurudiaerudia swali moja mara kadhaa.
  • Shida katika kukumbuka maneno rahisi kama vile kusema "Kile kitu ninachotumia kuandikia" badala ya kusema "kalamu"
  • Kutotaka kufanya vitu ambayo kwa kawaida huwa unafurahia kurifanya.
  • Kufanya uamuzi usio stahili kama vile kuweka moto wa juu sana, kutembea muuani kukinyesha badala ya kujikinga kwa kutumia mwavuli, kusahau kula ama hata kumpatia mtu usiyemjua pesa nyingi, bila sababu yoyote.
  • Mabadiliko makubwa sana ya kitabia ya kuwa na hasira na huzuni.
  • Kuchanganyikiwa kutambua watu wa kitambo na wa kisasa.

Unatibuje hali hii?
Hapana matibabu ya ugonjwa huu. Hata hivyo ni muhimu uweke akili yako katika afya nzuri na changamfu. Tafuta utambue namna ya kufanya hivyo.
Iwapo wewe au mtu unayefahamu anaonyesha dalili zifuatazo pata ushauri wa daktari mara moja. Atakusaidia kutambua kinachousababisha.

Iwapo hali ya kimatibabu inasababisha hali hii, badilisha madawa na utumie yale ya vitamini. Ama kunywa vinywaji vingi ili hali hii isikidhoofishe. Iwapo hali ya Alzheimers inasababisha kusahau na kuchanganyikiwa, kuna aina ya dawa zinazoneza kupunguza hali hii.
 
Pumu (Asthma)

Asthma ni ugonjwa katika mapafu unao sababisha shida za kupumua. Mishipa inayopeleka hewa katika mapafu hufura kiwango cha kutopata hewa safi ya oksijeni (oxygen). Shambulio kali la Asthma laweza leta maafa.

Kuna vitu vingi vinavyo sababisha Asthma kushambulia mtu.Visababu ni vingi mfano: Vumbi, moshi, mazoezi, baridi au nyuzi za wanyama kama paka na mbwa.

Ishara za shambulizi la Asthma

  • Shida za kupumua
  • Mkoromo (kupumua kwa shida) na kutoa sauti kwa kifua wakati unapumua
  • Kukohoa Uchovu na wasiwasi

Fuata maagizo ya daktari jinsi ya kutumia dawa za Asthma au muite daktari ikiwa hujui cha kufanya mtoto wako akishambuliwa na Asthma.

Asthma inahatarisha maisha, nenda katika chumba cha dharura ikiwa:

  • Mwanao ana matatizo ya kuhema
  • Midomo au makucha inapogeuka kijivu
  • Ngozi sehemu ya shingo ya mtoto inajivuta.

Hakikisha una habari kuhusu afya ya mtoto wako na nambari za daktari na unapompeleka hospitali kwa chumba cha dharura, hakikisha una majina ya dawa zote mtoto wako anatumia
 
Back
Top Bottom