Magonjwa haya ya zinaa

Babu Swahili

Member
Jan 8, 2009
41
6
Wenyeji wenzangu, nilikuwa na maswali machache kuhusu magonjwa haya ya zinaa

1) Kuna tofauti gani kati ya gonorea, kaswende, na kisonono.

2) Kaswende na kisonono yanaitwaje kwa kiingereza?

3) Human Papillomavirus (HPV) infection inaitwaje kwa kiswahili?

Mujaaliwe
 
1) gonorea ni sawa na kisonono kinaambukizwa na bacteria aina ya gonococcus wakati kaswende inaambukizwa na aina ya treponema. gono - inaanza kuonyesha dalili mapema kuliko kaswende na kaswende yaweza kwenda muda mrefu bila kugundulika - ambapo yaweza kuathiri mpaka ubongo.
2) kaswende ni syphilis wakati kisonono ni gonorrhea
3) sijawahi kusikia kiswahili cha HPV, tusubiri wataalam waseme zaidi.
 
Mh kumbe kisonono ndio kiswahili cha gonorrea!

Shukrani
 
hivi haya magonjwa yanayoitwa genital na oral herpes ambayo yanasababishwa na Herpes simplex virus yanaitwaje kwa kiswahili?
 
Leprosy ni Ukoma, ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na vimelea waitwao (Mycobacterium leprae au M.Leprae), huathiri ngozi na mishipa ya fahamu. Ugonjwa huu huunezwa kwa njia ya hewa, mgonjwa wa ukoma ambaye haajanza matibabu akipumua au kupiga chafya husambaza vimelea hivyo kwenye hewa. Dalili zake ni baka au mabakamyasiyo na hisia yenye rangi ya shaba na kuvimba kwa mishipa ya fahamu ya mikono, uso na miguu.
 
Hivi kaswende siku hizi bado ipo? tatizo hili kubwa kiasi gani kwa Tz na dalili zake ni zipi? Je wanaoathirika zaidi ni akina baba au akina mama?
 
HPV ni kifupi cha Human Papilloma Viruses. Kama ilivyo kwa wadudu wengi hakuna tafsiri ya kiswahili rahisi. HPV ni kundi la virusi ambalo wako aina nyingi na huambikizwa kwa njia ya zinaa. Mara nyingi inaleta genital warts. Kuna aina tatu ikijumuhisha HPV 11, 16 na 18 ambao wanadhaniwa kuwa wana uhusianao mkubwa na kansa ya kizazi (cervical cancer). Siku za karibuni kumetengenezwa dawa ya kinga (vaccine) ambayo imeonyesha mafanikio mazuri ya kuzuia wale virusi kubaki mwilini kwa muda mrefu (persistence) na pia zile dalili za kwanza za kansa ya kizazi (lesion in situ). Hii kinga imeanza kutumika ulaya na Amerika kwa wasichana ambao hawajaanza kujamiiana. Bahati mbaya kama ilivyochelewesha ile kinga ya hepatitis B na Infuenza type B itachukua muda mrefu kabla ya waafrica kufaidi matunda ya hii kinga dhidi ya HPV. Kumbuka Kansa ya kizazi ndiyo inayoongoza kwa kansa za kina mama. Ukienda Ocean Road kuwa wagonjwa wengi sana ambao kwa bahati mbaya huwa wakukwenda hospitali too late kupata matibabu.
Willy
 
Back
Top Bottom