MAGNUS PAUL JACOB ULUNGI Ateuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
______________________

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana MAGNUS PAUL JACOB ULUNGI kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.

Bwana Ulungi anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Kinemo W.D. Kihomano ambaye amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Ulungi alikuwa Kamishna wa Uhamiaji Kitengo cha Sheria. Uteuzi huu unaanzia tarehe 09 Desemba, 2010.

(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI



IKULU,
DAR ES SALAAM.
14 Desemba, 2010
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana MAGNUS PAUL JACOB ULUNGI kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.

Bwana Ulungi anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Kinemo W.D. Kihomano ambaye amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Ulungi alikuwa Kamishna wa Uhamiaji Kitengo cha Sheria. Uteuzi huu unaanzia tarehe 09 Desemba, 2010.

(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI



IKULU,
DAR ES SALAAM.
14 Desemba, 2010
 
Thank you invisible

Nina spesho interest na uhamiaji kwasababu hawa jamaa wanatoa vibali vya kazi kwa mzungu yeyote tu, na i hope huyo ajaye atakua mkali zaidi. Wana agents wao siku hizi mitaani ambao hutumika kuanzia ku-process barua za applications hadi justification za kazi.

Ukizunguka kwenye ma_NGO wengi wameshavuka vile viwango vya taifa na ukijaribu kuonyesha interest ya kujua what is happening unakuta mabosi wako wanajua kila kitu.

THERE IS PETTY AND SHAMEFUL CORRUPTION HAPO UHAMIAJI MPAKA INATIA KICHEFUCHEFU

Kuna mijitu hadi inachana noti wakati haina hata digrii lakini inadunda na kudhalilisha wazawa wenye elimu na uwezo na moyo zaidi wa kufanya kazi... hayo yapo sana Dar, Mwanza na Arusha
 
Jamani hoja zetu ni katiba mpya tuuuuuuuuuuuu sehemu zote za huduma za jamiii ni rushwa tupu kwenda mbele
 
Acheni majungu nyie.

Uhamiaji inafanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni zake. Suala la Wazungu kupewa vibali vya kufanya kazi hapa nchini hata kama wataalamu wazawa wapo linatokana na ufadhili mnaoupokea toka kwao na masharti yake. Juzi mmepokea Waalimu toka Marekani ulitegemea Uhamiaji iwakatalie kuwapa vibali? Wachina wanatoa msaada wa ujenzi wa barabara na ma-foreman lazima watoke China.

So tuacheni kulaumu tu, tuangalie na mazingira kwanza.
 
Hakuna lolote wakenya,wamegeuza soko la kazi,kwa vibali toka uhamihaji.

wakenya wamejaa bongo kwa kuwa nyie mmelala. Milango ya soko la pamoja la Afrika Mashariki imefunguliwa, nendeni nanyi kenya mkatafute ajira.
 
Hakuna kipya hapo alikuwepo mwanzo hana lolote mvivu mwoga kwenye maamuzi kichaka cha mafisadi ;mshikaji wa Masha baada .Amekaimu ukamishna kwa muda mrefu hakuna jipya leo hii hakuna hata pass za muda mikoani kama Arusha,Mwanza,Kilimanjaro na hata DSM kwenyewe ambako ndio makao makuu watu tuna rudishwa namanga kupata hatiza zarura Arusha mjini ambako hakuna na nikipindi hiki cha mwisho wamwaka ambapo wa Tanzania wengi hasa wenyeji wa Bukoba tunapenda kurudi makwetu kupitia Kenya,Pia wajasilia mali ambao huvuka mipaka kwenda kenya na Uganda inashindikana kwa ukiritimba wa Idara hii ya kikabila iliyo ficha watoto wa vigogo sehemu za ulaji kama KIA,JKNIA NAMANGA,KASUMURO TUNDUMA na sehemu ambazo wana waweza kula viza kiulaini niwa badhilifu mbaya kabisa.Tatizo wanainchi hawaijui kwa undani Idara hii,Wama JF chokonoeni mtumwagie humu
 
Naitwa Swamadu Abdu nikijana mwenye umri wa miaka 20 naishi Temake, wailes nina mazungumzo na kamishna wangu mkuu wa uhamiaji bwana Magnus Paul Jacob Ulungi samahani sana naomba kama naweza pata mawasiliano yake binafsi itakuwa nzuri zaidi mimi namba yangu ya simu ni 0718794405
 
Yani mnachangia habari ya 2010!!!!! Mbona katibu mkuu ni Luhanjo!!!!! YANI!!
 
huyu Poti wangu sijui kachemshaje hapo maana ameka muda mfupi sana !!!
 
Swamadu, naomba Mungu wakupigie, lakini usisahau kuwaonyesha ile nymba wanayowaficha wasomali na wasudan wengi wageni ndani!
 
Back
Top Bottom