Maggid Mjengwa ana Virus?

Kwa tunaomfahamu, Ni kweli si rahisi kumnunua Mjengwa, japo kwa hulka yake, ni mtu wa kuangalia upepo unavuma kutokea wapi!
 
Mungu atamnusuru yeye na sie inshallah.
majjid amedai mwanafunzi wake ndiye aliyeweka izo picha...hapo 2mekuelewa, lkn naamini ulikuwa unafaham kuwa kuna tamasha lingine la vinega ambalo lina shindana na clouds, kwa nn majjid alipoona picha za tamasha la clouds hakuhoji za vinega zitafutwe na ziwekwee?
 
mimi namlaumi kwa kuandaa shindano la wabunge bila kuonesha vigezo
sikuwai kufikiri kuwa mjenge anaweza kuzembea kiasi hiki


Marytina,

Usiishie kulaumu tu. Kipyeenga kimeshapulizwa. Nenda . ukampigie kura mbunge kijana unayemwona yuko juu.

Na hapa soma updates ya kura zilivyoenda katika siku ya kwanza.

Pima-Maji ya Mjengwablog: Zitto Kabwe Na John Mnyika hapatoshi!

Ndugu zangu,


Labda ilitarajiwa, lakini si kwa kiwango hiki. Hata kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura http://mjengwablog.com haijamalizika saa chache zijazo, ushindani mkubwa wa kukusanya kura za wafuasi unaonekana ni kati ya Zitto Kabwe na John Mnyika.

Wengine wanaokuja kwa kasi ni Godbless Lema na Mohammed Dewji. Joseph Sugu Mbilinyi na January Makamba wanachuana vikali katika nafasi ya tano wote wakiwa na idadi sawa ya kura walizopigiwa.

Kati ya washiriki 19 ni washiriki sita tu watakaopita katika hatua hii ya mchujo na kupambanishwa na wenzao sita kutoka kundi la wabunge vijana wanawake. Mchakato huo wa wanawake umeshakamilika.


Kwenye hatua ya mchujo kinachotafutwa ni nani zaidi kati ya wabunge vijana wanaume na wanawake. Baaba ya mchujo tutaingia katika kitakachoitwa ‘ Mjengwablog Young Leaders Award ‘ – Hapo atapatikana mbunge bora kijana kwa mwaka 2011.

Na siku zote siasa ni vitu viwili; uwezo wa mwanasiasa na jinsi anavyokubalika na watu. Mwanasiasa anaweza kuwa na uwezo wa kisiasa, lakini hakubaliki na kinyume chake.

Pima-Maji ya Mjengwablog ni jaribio la kuwapa nafasi wabunge wetu vijana kupima jinsi wanavyopokelewa na jamii kutokana na michango yao kwa nchi, ndani na nje ya bunge. Ni kipimo pia cha uwezo wao wa kujenga mtandao hata kupitia teknolojia hii ya kisasa.


Zimebaki siku kumi na saa kadhaa za kupiga kura- Nenda http://mjengwablog.com kumpigia kura mbunge wako kijana!

Maggid Mjengwa,
Mratibu,
 
ama kweli uandishi, umaarufu ni kazi ngumu sana. hata kutokufanya usichokijua ama kama hukukisikia ni shida pia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom