admissionletter
JF-Expert Member
- Sep 20, 2010
- 329
- 157
Huyu Maggid ni mnafiki (hypocrite) kweli kweli. Kabla ya uchaguzi alikuwa akijikomba kwa CCM na kubeza mabadiliko kwa kukejeli kwa maneno mbali mbali kama vile kumuita Slaa ni "mti mmoja ambao hauwezi kujenga msitu." Sasa ameona mabadiliko yanatokea na yeye anabadilisha mwelekeo wa maoni yake. La muhimu kwenye makala yake hii ni kwamba anakiri CCM ni ya mafisadi. Hata hivyo, sikupenda hiyo analogy ya mtu "kuhangaika na kushika titi na kunyonya hata kama si la mama yake" sababu inakejeli mabadikiko. Inabidi aombe radhi kwa hii kauli. Na vive vile, inaonesha bado anadhani CCM itabadilika. Ujumbe wangu kwako Maggid ni kwamba: Its too late for CCM, the train has left the station :
................................................................................................
Na Maggid Mjengwa,
MTOTO anayetegemea maziwa toka titi la mama anafanyaje anapolikosa? Jibu lake; mtoto huyo atahangaika sana, na kama ataliona titi lingine, atalishika alinyonye, hata kama si la mama yake. Na mtu mzima anafanyaje? Nawe una majibu yako.
Hatimaye Watanzania tumeshiriki tena kwenye zoezi la kuwachagua viongozi wetu. Katika nchi , matokeo ya uchaguzi yana maana pia ya ujumbe au salamu zinazotolewa na walioshiriki uchaguzi huo, yaani wananchi kwenda kwa viongozi. Nionavyo, matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu yamebeba ujumbe mmoja mkubwa, lakini mfupi sana; MABADILIKO.
Kwamba umma umeanza kwa dhati kabisa kuonyesha unataka mabadiliko. Hamasa ya kisiasa imeongezeka. Kazi ya wanasiasa na hususan vyama vya siasa ni kusaidia kuyaongoza mabadaliko hayo katika njia salama. Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, kwa mara nyingine tena, kama kutakuwapo na dhamira ya kisiasa, yanakipa Chama Cha Mapinduzi, jukumu hilo kubwa la kuyaongoza mabadiliko hayo.
Kama Chama Cha Mapinduzi kina nia ya kupunguza kupotea kwa imani ya umma kwa chama hicho, basi, kutahitajika sio tu kufanyika mabadiliko makubwa ndani ya muundo wa Serikali na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, bali kufanyika kwa mabadiliko makubwa yenye kishindo.
Kuna watakaopuuza, lakini, kuna ukweli, kuwa tuhuma za ufisadi zimeipaka matope mno CCM. Kwenye macho ya umma, Chama hicho kimechafuliwa na tuhuma hizo za ufisadi. Kuna wana CCM leo wanajiuliza kama wavae sare za chama au la wapitapo mitaani. Maana, kuna Watanzania walioanza kuchukia rangi za chama hicho. Wanazihusisha na ufisadi.
Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yawe ni fundisho kwa chama tawala. Kama CCM inataka kubaki kwenye mioyo ya Watanzania wengi, kuwa na uhalali wa kubaki madarakani, basi, ina lazima ya kujipambanua kwa vitendo kutoka kwenye yote makubwa yenye kuhusiana na ufisadi na maovu mengine. Ibaki kuwa kimbilio la wanyonge. Isifike mahali, Chama kikajikuta katikati ya mgogoro na umma. Hilo laweza kuharakisha mazishi ya chama yasiyo na kisomo. Na hilo ni Neno La Leo.
( Neno hilo ni sehemu tu ya makala yangu Raia Mwema, juma hili)
Maggid,
Iringa,
http://mjengwa.blogspot.com/