Mageuzi hayaepukiki!

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Nakumbuka tukiwa shule ilikuwa ukitokea mgomo wanafunzi tukagoma siku ya 1, 2 , siku ya 3 munkari ilikuwa ikipanda sana, wote tulikuwa tayari hata kufukuzwa, moyo wa kuendelea na mgomo ulikuwa ukiongezeka kila siku kiasi cha kuwa tayari kwa lolote. Ki fizikia hii huitwa escape velocity!no turning back!
Hali ya watanzania kwa sasa iko kwenye escape velocity ya mageuzi; watu wengi vijana kwa wazee wamefikia mahali pa kutaka mageuzi kwa gharama yoyote, politically macho yao yako kwa CHADEMA kama chama cha kubadili hali iliyopo.
Maoni yangu ni kwamba, kama CHADEMA kitashindwa kujipanga kushika dola badala ya ccm na kama ccm watafanya ujanja ili waendelee kutawala, nchi yaweza tumbukia kwenye vurugu kwa kuwa njaa ya mageuzi waliyonayo wananchi haitatulizwa kwa ahadi zile zile na mfumo uleule uliokuwepo kwa niaka 50 ya uhuru, wako kwenye escape velocity!
Nawasilisha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom