Magdalena Sakaya: Pengine Ungekuwa na tija zaidi kama ungekuwa CHADEMA

magdalena yupo SAHIHI kama aliwatetea kwa kufuata sheria,,..Isije kuwa aliandamana pasipo sababu halafu anajifanya anawatetea wanyonge,,.maana sasa hivi watu wanavunja sheria wanazingizia Nguvu ya UMMA,sasa kwa mpango wa namna hii mbona nchi haita tawalika.
 
WANAJF
Jamani naombeni kufahamu kuhusiana na mbunge huyu maana simuelewi
Je ni mbunge kuteuliwa kupitia mkoa gani Tabora ama Kilimanjaro kama ni kupitia Tabora mbona hana makazi huko tabora maana taarifa za kiintelejensia ni kuwa alipaswa kuwa kilimanjaro kama kweli ni sawa basi Lipumba ajiangalie mara mbili uteuzi walioufanya maana atakuwa anajiandaa kukata mti huku amekaa huu yake
Magdalena sakaaya alikuwa akifanya wapi kazi kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge

Mkuu, mbona ueleweki nakushauri kama unataka habari zake bibi Magdalena Sakaya, tembelea web site ya CUE au nenda makao makuu CUF Buguruni utapata habari zake
 
Ni mbunge wa CUF viti maalum, mbunge pekee wa viti maalum wa CUF aliye active bungeni. Magdalena Sakaya kwa kweli ananifurahisha sana akisimama bungeni na kuongea. She talks sense and she means business. Hata akiwa hewani kwenye radio au tv yaani anaongea kitu kinaingia akilini. Na anaonekana anajielimisha vya kutosha, pengine siyo mmoja kati ya wale wanaosubiri kuandaliwa cha kusema bungeni!

Nimekuwa nikijiuliza kama angekuwa Chadema angeweza kufanya mengi zaidi kiasi gani. Kwa maana ya kwamba I feel she is being under utilized huko aliko.

Unataka kunambia kuwa wapo wasiofaa huko CHADEMA ambao nafasi yao ingechukuliwa na Sakaya?
 
Unataka kunambia kuwa wapo wasiofaa huko CHADEMA ambao nafasi yao ingechukuliwa na Sakaya?

As far as I know wasiofaa wako kila mahali tofauti ni idadi na uwanja wakuchezea. Wasiofaa wakiwa wachache kwenye chama wana-play underground kwasababu wananyimwa uwanja wakucheza hivyo ni vigumu kuwatambua. Wasiofaa wakiwa wengi kwenye chama, play ground nayo inakuwa kubwa(hamna wakuwasumbua) hivyo wanaishia ku-run the show. Therefore naunga mkono wanaosema Sakaya abaki CUF. Tunahitaji wazalendo kwenye kila chama.
 
mkuu bila shaka chama pekee ambacho mtu anapaswa kuwa ni chadema peke yake, haahaa! Kweli hayo ni maoni yako! Zinduka kutoka usingizini wewe

ofcourse CUF is a dying part trying to make sure it sinks other parties, au ulitaka awe CCM?
 
Back
Top Bottom