Mkulima wa Kuku
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,270
- 533
Asante kwa ujumbe wako ila nadhani wakenya wamezungumza ukweli kuhusu Rais wetu na kupenda kwake safari za nje na kuwa soft kwenye suala la rushwa. Hayo ni malalamiko ya watanzania wengi na Rais hataki kuyasikiliza kwa sababu anazojua mwenyewe. Najua wakenya wamepata mambo hayo kutoka kwa watanzania wasioridhika jinsi nchi inavyoendeshwa na jinsi JK anavyopenda safari za nje (yaweza kuwa kwa manufaa binafsi akiogopa kupokea rushwa waziwazi ila ajilipe kutoka kwenye posho za safari).
Mtazamo huo umekuwa ukizungumzwa na watanzania na wakenya wamecopy toka kwa watanzania kama mimi wasioridhishwa na mwenendo wa mkuu wetu wa kaya. Sioni tatizo la kutuchonganisha na wakenya hapa!
Kama unasema unaridhika na hali ilivyo tutakushangaa mwenzetu.