Magazeti ya Kenya na dhihaka kwa Rais wetu

WanaJF nilikuwa napitia gazeti la The East African lililotoka Jumamosi tarehe 16.07.2011 nikakutana na kichwa cha habari kisemacho A record Four East African Presidents Set to Retire. Mwandishi amewaongelea Marais wa EA kwa upande wa Rais wetu nikaona sentensi zifuatazo;

"Tanzania’s Jakaya Kikwete, re-elected to a second term last year, will step down in four years. Hobbled with the reputation of a lazy, foreign-trip-loving president who is soft on corruption, Kikwete seems to be busy sprucing his image. Amidst signs that the long-ruling Chama Cha Mapunduzi is in the midst of a shake-up, Kikwete has been pushing some of the more controversial and scandal-tainted politicians off the cliff, or a few of them have saved themselves the humiliation and jumped."

Haya maneno hayakunifurahisha kwa kuwa magazeti ya Kenya yamekuwa mstari wa mbele kudhihaki viongozi wetu wakati magazeti yetu hayajawahi kuwadhihaki viongozi wa Kenya. NAkumbuka kuna wakati Gazeti moja kama si hili la East African lilichora kikatuni kikionyesha kiongozi wetu akilamba viatu vya wazungu. Nadhani ni wakati muafaka dhihaka hizi zikomeshwe.

Source:The East African:  - News |A record four East African presidents set to retire

Lazy
Foreign trip-Loving
Soft on corruption
busy spruicing his image
Chama cha Mapinduzi is in the midst of shake-up
Pushing his friends off the cliff

Jamani, nimeyarudia rudia hayo maneno hapo juu kama mara saba hivi,
sijaona tatizo lake except plain truth.
 
Kumbe ni story za Marais wa East Afrika.,sio issue mwandishi alikuwa anatoa taswira ya Marais wetu wa EAST AFRICA wanavyoonekanaje kwenye SIASA za NJE.SIONI TATIZO
 
Wanasiasa wetu ni wa ajabu sana. Wakisifiwa na watu wa nje wanajiona wamewin na wanajitapa kwetu watanzania. Sasa wanadharauriwa na watu wa nje wana ...................
 
WanaJF nilikuwa napitia gazeti la The East African lililotoka Jumamosi tarehe 16.07.2011 nikakutana na kichwa cha habari kisemacho A record Four East African Presidents Set to Retire. Mwandishi amewaongelea Marais wa EA kwa upande wa Rais wetu nikaona sentensi zifuatazo;

"Tanzania’s Jakaya Kikwete, re-elected to a second term last year, will step down in four years. Hobbled with the reputation of a lazy, foreign-trip-loving president who is soft on corruption, Kikwete seems to be busy sprucing his image. Amidst signs that the long-ruling Chama Cha Mapunduzi is in the midst of a shake-up, Kikwete has been pushing some of the more controversial and scandal-tainted politicians off the cliff, or a few of them have saved themselves the humiliation and jumped."

Haya maneno hayakunifurahisha kwa kuwa magazeti ya Kenya yamekuwa mstari wa mbele kudhihaki viongozi wetu wakati magazeti yetu hayajawahi kuwadhihaki viongozi wa Kenya. NAkumbuka kuna wakati Gazeti moja kama si hili la East African lilichora kikatuni kikionyesha kiongozi wetu akilamba viatu vya wazungu. Nadhani ni wakati muafaka dhihaka hizi zikomeshwe.

Source:The East African:  - News |A record four East African presidents set to retire
Si huwa wanasema Rais anasifiwa nje ya nchi? Weldone The East African. Magazeti yetu hayaandiki? Mbona kila Jumatano Kubenea anamchapa Mkulu? Magazeti mengine yanaogopa lakini ukweli ni kwamba jamaa ni goigoi zaidi ya hivyo walivyosema
 
Wameandika Wakenya mnaona wamewaonea! I do congratulate mwandishi wa Kenya kutusaidia katika hili 'Keep it up pls reveal more kwani uongo' Ukweli unauma siku zote. Alichosema uongo hapo ni nini? Sio Kenya tu wanaliona hili ni ulimwengu mzima wacha watusaidie wanaoona au kujisikia uchungu basi hamuitakii mema Tz.
 
wenye akili fupi wanaotawaliwa na fikra na itikadi zisizo huru watashangilia kitendo hiki na hawa ni wale wenye fikra fupi wasiotaka kuona mbali, wenye uwezo wa kuona mbali wataishia kusikitika hata kama anayosemwa nayo kikwete ni ya kweli ila je yanasemwa kwa lengo gani? Baba yako hata kama kakunyima hela ya mtaji wa biashara haimvui thamani ya kuwa baba na hata kama ikitokea anasemwa kwa mabaya hata kama ni kweli inapaswa uzalendo ukuguse, na haya ndo mapenzi ya kweli kwa taifa lako. Kijana mwema ni yule ambaye hujenga nyumba kwa mikono na aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Huu ujumbe wako unamfaa Ridhi 1 unaonaje kama ungemtumia yeye?
 
Mkuu unatakiwa uelewe kwamba gazeti la East African pamoja na kuminilikiwa na nation media group ambayo makao makuu yake ni Nairobi si mali ya wakenya au serikali ya Kenya kama unavyotaka kupotosha, na upotoshaji huu unaufanya makusudi ili kuneutralize hoja. Gazeti hili ndiyo the only one linalocover habari za east Africa almost equally kiusawa wa no. of pages. Ni gazeti linalokubalika na kuaminika, it is "the economist" of East Africa.

Tukija kwenye hoja yako kwa kumbukumbu yangu maraisi wote wa East Africa wamekuwa wakichambuliwa vilivyo ndani ya gazeti hili, ishu kama ya mke wa Kibaki waliiandika ina way mama Salma angeandikwa vile na gazeti kama majira au "la kenya" (mwananchi) basi lingefungiwa. Na kama alivyosema Pasco hapo juu, these guys they just call a spade a spade. Ni kipi hapo unachokiona si kweli kuhusu JK?


Your are damn right!! Big up!!!
 
Mkuu kwa kuajiri waganda, wakenya na watz kuna maana gazeti si la Kenya? Ukenya wake unatokana na lilikoandikishwa!! Kama jina ni hoja basi News of the World lingekuwa si la Uingereza bali la Dunia!!

Tuachane na lilikosajiliwa pamoja na wamiliki mkuu maana itabidi tufunge pia safari hadi brella nk...... turudi kwenye hoja yako ya msingi. Kosa la gazeti hatulioni Afande!
 
baba yangu mwenyewe aliwahi kusema kuwa kikwete is the worst president we ever had


wewe mleta mada unadhani mzee wangu alikua anamsingizia jk?
 
Hajadhihakiwa kaambiwa ukilema wake,kuna kosa,waziri wake wa habari si yupo alifungie basi tuone kama anaubavu.Issue hapa kaambiwa ukweli bila kutafuna maneno gazeti hilo si sawa na uhuru wala mzalendo hizo ndizo sifa za jk kama unauchungu kuwa mwenyekiti wako kachafuliwa basi tuambie kati ya hayo aliyoambiwa ni lipi kabambikiwa la kama umeumizwa sana nenda mahakani kwa niaba ya raisi wako.
 
Habari hiyo ni sahihi kabisa, ila kinachonishangaza ni jinsi Kenya walivyo active sana kwa siasa za hapa kwetu. Ilifikia hata wakaja kumpigia Kikwete kampeini wakati wa uchaguzi, na wala hakuingilia kati kuwaonya kuwa wasiingilie politiksi za kwetu. Kwa hali hiyo kwa, vile walishiriki kumpigia kampeini, ni lazimawashiriki kumpiga madogo, na wala asilalamike,
 
a yAANI THE EAST AFRICAN HAWAJAKOSEA KABISA. NDO SIFA ZAKE HIZO HUYU PREZIDAA WETU.
 
Huwezi kumpa mtu kitu ambacho huna...atasifiwaje kwa kazi asiyofanya? Where on earth could I be rewarded free lunch so that I could go?? Kwani ni uongo anasafiri mno kuliko muda anaokaa kuongoza nchi akiwa ndani? Kwani ni uongo anaogopa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa rushwa ati kwasababu hana ushahidi hata kama ushahidi upo?
Huyo ndio kiongozi mkuu wa nchi ambaye ametuletea mgao mkubwa wa umeme kwasababu yeye sio Mungu wa kuamuru mvua inyeshe. Do we know we have other sources of energy from thermal such as coal and gas? Au ndio tunasubiri tuwalete wawekezaji ambao ni lazima wakubali kutuweka kama shareholders ndio hizo project zifanyike??? I see something wrong with the leadership we have....I salute those who have jumped out of the boat because before we know, we would find ourselves hitting the rock in the mid of chaotic ocean.
 
Gazeti liko sahihi na hakuna udhalilishaji wa aina yoyote. Zaidi ya hilo, nasikitika gazeti limeacha kusema mengin mengine ambayo ni stahiki ya JMK
 
Wenye akili fupi wanaotawaliwa na fikra na itikadi zisizo huru watashangilia kitendo hiki na hawa ni wale wenye fikra fupi wasiotaka kuona mbali, wenye uwezo wa kuona mbali wataishia kusikitika hata kama anayosemwa nayo kikwete ni ya kweli ila je yanasemwa kwa lengo gani?

Baba yako hata kama kakunyima hela ya mtaji wa biashara haimvui thamani ya kuwa baba na hata kama ikitokea anasemwa kwa mabaya hata kama ni kweli inapaswa uzalendo ukuguse, na haya ndo mapenzi ya kweli kwa taifa lako. Kijana mwema ni yule ambaye hujenga nyumba kwa mikono na aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

mkuu hujawahi kuona mtu anamkataa baba yake kwasababu ya tabia chafu? km wewe baba yako ni mlevi wa kupindukia hadi kufikia hatua ya kujinyea barabarani kila siku ama kuvuliwa nguo na watoto utamthamini kweli?
 
Back
Top Bottom