Magazeti na takwimu za maafa ya ajali ya meli

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Magazeti mengi ya leo 19/07/2012 yametoa taarifa ya iadadi ya abiria waliokuwemo kwenye meli, wanaohofiwa kufa, maiti zilizopatikana, waliookolewa, na ambao hawajaonekana. Cha kushangaza takwimu hizi zinapishana kwa asilimia kubwa sasa je hivi tatizo liko wapi? Kwa watoa takwimu kuwa wengi? Au kwa waandishi wetu wa habari?
 
wabongo kukurupuka si ndo zao? hawana muda wa kutafiti na ku confirm takwimu. matokeo yake kila mtu anatoa lake! God help us!
 
Mbona Biblia moja inamuelezea Yesu lakini katika Injili zake 4 kila moja inatoa maelezo tofauti ya Yesu, moja inamtaja kama mwana wa Daud, nyingine vingine?
 
Unaposoma Biblia ili uielewe, kubali kuanza kama mtoto wa chekechea. Tafuta kanisa la Neno la Kristo ukae chini ya waalimu ufundishwe. Biblia haina makosa bali ufahamu wako katika mambo ya rohoni ni zero.
 
Kuna waandishi wa habari basi bongo, wanaofahamu kuandika wako busy na michakato ya urais 2015. Waliobaki wote walikimbia umande, hivyo muda mwingi wanavizia milungula ya kuwachafua watu. Ukikuta kuna habari haijakosewa basi haihitaji muda au uchunguzi wa kina. Acha hivyo hivyo tutajifunza practically!
 
Back
Top Bottom