Magazeti haya yanachefua-kila siku CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wadau,
Kuna haya magazeti ya uhuru,jambo leo na habari leo.Imekuwa ni ajabu kwani ni lazima kila siku kuwe na heading kubwa inayouza gazeti inayohusu chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.Nimekuwa nikijiuliza wasipoandika chadema hawauzi?? Katika nchi hii kuna vyama vya siasa 18,ina maana ni chadema tu inaonekana?? Ninashangaa gazeti la uhuru badala ya kuandika mambo ya chama chake CCM imekuwa ni wimbo wa Taifa Chadema.Habari leo badala ya kuandika habari za Taifa kama gazeti la serikali imekuwa kila siku ni Chadema.Gazeti jambo leo lenye uhusiano na CCM badala ya kuhangaika kusafisha chama chake limekuwa kila siku ni Chadema.Hivi hawa wahariri hawaoni aibu?? Hivi mnadhani msipoandika chadema hamtauza habari? Kwa mfano leo magazeti yote matatu Uhuru,Habari leo na Jambo leo yana heading moja inayofanana kuhusu chadema.Inaonekana ni mtu mmoja nayesambaza habari za chadema kwenye haya magazeti matatu.Hakika inakera!!
Nawasilisha
 
Angalia wamiliki wake utapata majibu. Kwenye mti wa maembe, ni embe bivu ndilo
ndilo linalo tupiwa mawe kupopolewa!.
 
Mbona huwasemi mwanahalisi,raia mwema na tanzania daima? Wao kila siku ni habari za lowasa, me natamani hayo magazeti yangebadilishwa majina na kuitwa lowasa newspapers
 
Mkuu bado unasoma hayo magazeti? You must be out of the country! Magazeti yanayofanya kazi inayofanana na ya Tambwe Hiza. Sina ushahidi ila wa kimazingira unathibitisha kuwa wanafanya kazi pamoja!
 
Ufinyu wa mawazo.Ina maana Mwanahalisi ni gazeti la serikali?? Na raia mwwema ni gazeti la chama??
 
Kwani hayo ni mageti au vipeperusi vya matangazo. Mimi nilishayasahau hata rangi yake. Achana nayo!
 
Mkuu bado unasoma hayo magazeti? You must be out of the country! Magazeti yanayofanya kazi inayofanana na ya Tambwe Hiza. Sina ushahidi ila wa kimazingira unathibitisha kuwa wanafanya kazi pamoja!

Salute you!
 
Wadau,
Kuna haya magazeti ya uhuru,jambo leo na habari leo.Imekuwa ni ajabu kwani ni lazima kila siku kuwe na heading kubwa inayouza gazeti inayohusu chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.Nimekuwa nikijiuliza wasipoandika chadema hawauzi?? Katika nchi hii kuna vyama vya siasa 18,ina maana ni chadema tu inaonekana?? Ninashangaa gazeti la uhuru badala ya kuandika mambo ya chama chake CCM imekuwa ni wimbo wa Taifa Chadema.Habari leo badala ya kuandika habari za Taifa kama gazeti la serikali imekuwa kila siku ni Chadema.Gazeti jambo leo lenye uhusiano na CCM badala ya kuhangaika kusafisha chama chake limekuwa kila siku ni Chadema.Hivi hawa wahariri hawaoni aibu?? Hivi mnadhani msipoandika chadema hamtauza habari? Kwa mfano leo magazeti yote matatu Uhuru,Habari leo na Jambo leo yana heading moja inayofanana kuhusu chadema.Inaonekana ni mtu mmoja nayesambaza habari za chadema kwenye haya magazeti matatu.Hakika inakera!!
Nawasilisha
ni sawa tu na kubenea vs. lowassa

we have to accept alternative thinking.... ndio demokrasia yenyewe hiyo
 
Anzisha gazeti lako uwe unawasifia chadema na mkeo daily, tutalinunua.

Aksante "greater thinker" kwa constructive ideas zako. Nilidhani humu tunadeal na issues sasa haya ya mkewe yanatoka wapi????
 
Mbona tanzania DAIMA, Mwananchi na Raia mwema kila siku CCM.........acha ushabiki.

Acha uongo unasema mwanahalisi na Tanzania daima kila siku CCM.Mbona Tanzania daima la leo halina habari ya CCM? Mbona mwanahalisi la J5 hii halikuwa na habari ianyohusu CCM kama chama??
 
ni sawa tu na kubenea vs. lowassa

we have to accept alternative thinking.... ndio demokrasia yenyewe hiyo

MTM,
Its true but the problem is how they are reporing issues.Habari leo ni gazeti la serikali,haiwezekani kila siku likawa linaandika habari za kukashifu chama kimoja tu cha siasa.Kweli hii ni sawa?? Huoni hawa wahariri wake wanalipwa kutokana na kodi ya watanzania wote?? Wanachadema hawastahili haki katika gazeti hili ilihali pia wanalipa kodi??
 
Habari za Chadema zinauza kaka, huwezi kuandika habari za UPDP, JAHAZI ASILIA, DEMOKRASIA MAKINI nk, halafu ukategemea kuuza gazeti. Kwa sasa Chadema ndo chama pekee cha siasa, vingine ni SACCOS
 
Ni kweli kaka.Ndio maana hata gazeti la Uhuru badala ya kuandika mambo ya chama cha CCM wanaandika ya chadema...Very true..Umenifumbua akili sasa.Yako kibiashara zaidi
 
Mwanahalisi Vs Lowasa and Chenge.......lazima ujifunze kuangalia pande zote, na si upande mmoja tu.
 
Hivi imeandikwa wapi kila gazeti Tanzania lazima liisifie CDM? Usiwe unakurupuka! Kuna Chama kinabebwa na Magazeti kama CDM, Tanzania Daima, Raia Mwema, Mwananchi, Mwanahalisi, Nipashe, jamani kweli nyie ni wabinafsi wakubwa
 
Back
Top Bottom