Magari yote ya kwenda kaskazini yamekwama wami muda huu

NICK2275

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
3,931
918
Magari yote yanaoyokwenda mikoa ya kaskazini na mikoa mingine yamekawama wami baada ya gari moja kugonga mtoto na wanakijiji wamevamia barabara na kuiziba wakidemand kuwekewa matuta-
hadi sasa hali si shwari
 
iyo barabara c ni highway, matuta ya nini? Mpaka mifugo kama ng'ombe, mbuzi, kondoo wanazurura pembezoni mwa hiyo barabara.
 
iyo barabara c ni highway, matuta ya nini? Mpaka mifugo kama ng'ombe, mbuzi, kondoo wanazurura pembezoni mwa hiyo barabara.
Nani alikwambia kuwa high way haiwekwi matuta? Ni huko kwenye mapori ndipo kusikowekwa matuta lakini kama barabara inapita maeneo yenye makazi ya watu lazima kuweka matuta vinginevyo madereva wenu walevi hawa watamaliza watu....They are very right hawa wanakijiji:whoo:
 
Mwana!Pole sana.Inabidi,serikali,iwawekee matuta.Vinginevyo hao madereva,watazidi kuwaua.

Matuta highway hayatakiwi...Yenyewe pia ni hatari kwa magari..elimu na tahadhari kwa watumiaji wote,iwe madereva na waenda kwa miguu ambao hudhani dereva anawaona na atafunga brake
 
Hivi ndani ya mipaka ya Tanzania kuna barabara yenye "hadhi" ya kuitwa "highway"?

DAR-Chalinze?
DAR-Morogoro?
Dar-Tanga?
Dar-Moshi-Arusha?
DAR-Mbeya-Tunduma?
Dar-Songea?

Nikiangalia upana wa hizi barabara - zote zinaonekana kama "Feeder Roads"!
 
Matuta highway hayatakiwi...Yenyewe pia ni hatari kwa magari..elimu na tahadhari kwa watumiaji wote,iwe madereva na waenda kwa miguu ambao hudhani dereva anawaona na atafunga brake
hapo kwenye nyekundu nisheria au...maana hapa kwetu tuna tuta kubwa kuliko yote Africa mashariki...lol
 
Matuta highway hayatakiwi...Yenyewe pia ni hatari kwa magari..elimu na tahadhari kwa watumiaji wote,iwe madereva na waenda kwa miguu ambao hudhani dereva anawaona na atafunga brake
Mbona mikumi wameweka, inamaana swala wanaumuhimu sana kuliko binadamu eeh??
 
hapo kwenye nyekundu nisheria au...maana hapa kwetu tuna tuta kubwa kuliko yote Africa mashariki...lol

Ni sheria lakini tunazioverlook kutokana na udhaifu wetu na mtazamo wa kizimamoto..ukiangalia kwa upande wa pili matuta hayo ndo chanzo cha ajali nyingi...mfano pale Wami immediately baada ya daraja kuna tuta,sasa lori la tani 40 likifika hapo shurti apangue gia aanze na low na mzigo ni mzito linafail linarudi kinumenyume...hayatakiwi
ELIMU kwa watumiaji
 
Hivi ndani ya mipaka ya Tanzania kuna barabara yenye "hadhi" ya kuitwa "highway"?

DAR-Chalinze?
DAR-Morogoro?
Dar-Tanga?
Dar-Moshi-Arusha?
DAR-Mbeya-Tunduma?
Dar-Songea?

Nikiangalia upana wa hizi barabara - zote zinaonekana kama "Feeder Roads"!

Baba Enock,kwani barabara yenye hadhi ya highway ikoje??lami ya inakuwa ya randi gani au barabara inakuwa na upana gani??na kwanini barabara iitwe highway road.....!!!ipende nchi yako Baba Enock
 
Hapa tunaona umuhimu wa bagamoyo kiwete tuwekee kituo bagamoyo yetu tuachane na laana za wami
 
Hiyo ni NEWS! Hivi kule RSA (Kruger National Park) zinaingia Bajaj tu?

Baba Enock
kupitisha barabara kuu kama ya Tanzam katika park ni uharibifu wa mazingira
unahatarisha maisha ya wanyama kwa kugongwa,kupewa sumu,kuibiwa nk
kunawatisha wanyama wanadimika
kunaondoa pato la taifa kwa kuwa watumiaji barabara wanafanya utalii bure
pia ni hatari kwa wasfiri pindi itokeapo dharura ,ajali nk
 
Ni sheria lakini tunazioverlook kutokana na udhaifu wetu na mtazamo wa kizimamoto..ukiangalia kwa upande wa pili matuta hayo ndo chanzo cha ajali nyingi...mfano pale Wami immediately baada ya daraja kuna tuta,sasa lori la tani 40 likifika hapo shurti apangue gia aanze na low na mzigo ni mzito linafail linarudi kinumenyume...hayatakiwi
ELIMU kwa watumiaji
Kwa madereva wetu watanzania matuta yaliyoko pale wami yanasaidia sana....vinginevyo watu watakuwa wana pita wakiwa kwenye 120...
 
Hivi kama kila anapogongwa mtu patawekwa tuta hiyo barabara si itakuwa milima? Mara nyingi hakuna dereva anayedhamiria kumgonga mtu na kuna wakati pia watembea kwa miguu wanakuwa ndo wana makosa. Suluhisho la kugongwa watu siyo matuta bali watu wa karibu na barabara kuu waelimishwe jinsi ya kumbea na kuvuka barabara kwa usalama. Wanafunzi wa shule wapewe elimu ya kuvuka na kutembea barabara kubwa ili kupunguza ajali.

Nasema hivi kwa sababu tarehe 21/06/2010 nilikuwa na drive kutoka Arusha kwenda Morogoro nilipofika maeneo ya Mzundu mzee mmoja akiwa na baiskeli akatokea uchochoroni kwa kasi na kuvuka barabara bila kuangalia upande wowote. Lingekuwa basi lingemzoa kwani nilitumia nguvu ya ziada kusimamisha gari ili kumkwepa. Kwa tukio kama hili hata ukiweka matuta yatasaidia nini kwa watu wazembe kama hawa?
 
Kinachotakiwa ni elimu kwa watumiaji wote wa barabara, kuweka matuta siyo suluhisho la kudumu na wananchi wanaoishi kando ya barabara kuu watataka yawekwe matuta kwenye sehemu zao na mwisho barabara yote itakuwa ni matuta tu.
 
Ndugu haishauriwi kuweka matuta kwenye highway ndio sababu kama wewe ni mzururaji mzuri utagundua kuwa tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na matuta mengi kwenye highway. Kinachotakiwa kufanyika ni kwa serikali kuhakikisha sheria za barabarani zinafuatwa na wala sio kuweka matuta. Nakumbuka hata magufuli aliwahi kusema hakuna kitu anachukia kama matuta kwa highway. sana sana hayo yanaongeza ajali especialy usiku.

Back
Top Bottom