Magari Yalioibwa Yapatikana

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Kikosi cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kimekamata magari 10 yaliyoibwa katika sehemu mbalimbali nchini, yakiwa safarini kuelekea mkoani Shinyanga na Mara kwa ajili ya kuuzwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa kanda hiyo, Abdul Nina, alisema magari hayo yalikamatwa juzi yakiwa yamebadilishwa rangi na yakiwa na namba za usajili za bandia.

Nina aliyataja baadhi ya magari hayo kuwa Toyota Nadia lenye namba ya usajili T 889 BJJ, lenye rangi ya damu ya mzee na Toyota RAV4 namba T 488 AYY lenye rangi ya kijani. Alisema magari hayo yalikuwa ndani ya uzio wa nyumba ya kulala wageni ya Sane, inayomilikiwa na Richard Nchambi, mkazi wa Kahama.

Kaimu kamanda alisema Juni 23, mwaka huu, gari lenye namba ya usajili T 796 BLZ, aina ya Toyota Spacio, lenye rangi nyeupe, lilikamatwa likimilikiwa na Musoma Anthony. Alisema watuhumiwa walipohojiwa walidai magari hayo waliyapata kutoka kwa Yusuph Ramadhani.

Nina alisema uchunguzi wa awali unaonesha magari hayo yaliibwa Sinza, katika Baa ya JJ yalikokuwa yameegeshwa.

Akasema jioni ya Juni 24, mwaka huu, polisi walikamata gari lenye namba ya usajili T 170 ABD, aina ya Toyota Corolla, lenye rangi nyekundu. Erick Yona, ambaye ni fundi mitambo wa kampuni ya tiGO tawi la Shinyanga, alikutwa na gari hilo akidai amelinunua kutoka kwa Yusuph Ramadhani. Gari jingine lililokamatwa ni Cresta GX100 ambalo liliuzwa mkoani Shinyanga.

- via magazeti ya Mwananchi na Uhuru
 
naona wizi wa magari umetinga tena tanzania, nilishaanzaga sahau sikia habari hizi.
 
Back
Top Bottom