Magari ya Rais yazimika tena

Kikwete anatakiwa aondolewa kwa box la kura lakini sio kumfanyia vitu vya aina hii vya kutaka kuhatarisha maisha yake bila sababu amfute kazi mkuu wa itifaki ikulu akingojea mengine yatokee watammaliza,hawana nia njema mambo gani hayo bwana waache uzembe ujinga mtupu kabisa yaani hawana vituo maalumu wanaweza wakajaza mafuta popote pale ,hii ni hatari sana hatuna tena watu tuliokuwa tunawaamini waliokuwa wnalinda viongozi wetu ,mbaya,mbaya mbaya ,KIKWETE fukuza mkuu wa itifaki hapo IKULU wanakula bure kodi za wananchi

mtafukuza wote lakini yeye mwenyewe anawajuwa wabaya wake ..kwa majina ....maana alilowafanyia anayajuwa...my take is kwamba ni bora watu wakajifunza kusameheana!!!
 
Jamani mimi sina hata la kusema manake siku ile yalipochomoka matairi nilizoza weee

1. Gari ya Rais itawekwaje mafuta mtaani?
2. Moshi hakuna TEMESA na recommended stations?
What the hell is this?
Rais, wawahi kabla hawajakuwahi. Mi sielewi kabisa, ni kama naota vile. Haya mambo hata mtoto mduchu hawezi kuelewa.
 
Kikwete anatakiwa aondolewa kwa box la kura lakini sio kumfanyia vitu vya aina hii vya kutaka kuhatarisha maisha yake bila sababu amfute kazi mkuu wa itifaki ikulu akingojea mengine yatokee watammaliza,hawana nia njema mambo gani hayo bwana waache uzembe ujinga mtupu kabisa yaani hawana vituo maalumu wanaweza wakajaza mafuta popote pale ,hii ni hatari sana hatuna tena watu tuliokuwa tunawaamini waliokuwa wnalinda viongozi wetu ,mbaya,mbaya mbaya ,KIKWETE fukuza mkuu wa itifaki hapo IKULU wanakula bure kodi za wananchi

Huwezi fukuza kila mtu. kama inawezekana basi waanze na wawekezaji waliopewa sekta nyeti. Maana yake tangu tulipowaingiza hadi jikoni ndo tumeanza kuvuna tulichopanda. habari ndiyo hiyo...:roll:
 
Hao adui zake si wasubiri tu amalize kazi na wamshitaki kwa kuvunja katiba?

Sasa haya ya kuuwa, watakuwa wamejipaka damu za mtu bure.

Ila nafikiri kwa HUJUMA, Tanzania tuna uzoefu sana.

Walimuhujumu Nyerere na mipango yake na wakauwa kila kitu.

Sidhani kama Muungwana watamsalimisha kama wamedhamiria.

Tunaenda PABAYA. Labda Muungwana akae nao meza moja na ang'atuke.

Mambo yamemshinda kwa kweli si mchezo.

Anajitahidi tu kukutana na wanamichezo maarufu. Mengine, mhhhh!!!!!!!
 
Kusema kweli kwa mji wa Moshi kituo hicho cha Total cha Laswai ni kati ya vinavyoaminika sana. Mimi mwenyewe nikiwa huko huwa ni mteja wao na hakuna hata siku moja nimepata shida ya gari kutokana na mafuta yao.

Sawa inaweza kuwa kweli wamechanganya mafuta (labda ndio kawaida yao au siku hiyo ndio ya kwanza baada ya kuletewa mafuta na Mt Meru), lakini KWA NINI MAGARI HAYO YA IKULU TU NDIO YAZIMIKE?? Au hayo magari hayafanyiwi matengenezo ya mara kwa mara? Au huwa yanapakiwa tu hapo ikulu ya Moshi hadi ugeni wa rais utokee (what a waste!)?

Ushauri wangu ni huu, wote waliohusika na uandaaji wa hayo magari wawekwe chini ya ulinzi.

Halafu we Kikwete siku nyingine utembelee Landrover 110
 
wasimuue mzee wa watu kwa presha bure...tujiulize jambo moja..kama mafuta ya kituo yalikuwa machafu ni kwa nini magari mengine ya binafsi yaliyojaza mafuta ....kwenye batch hiyo hiyo hayakuzimika ......yazimike hayo 5...tu ya msafara wa rais...mtaumiza watu wa nje ..wakati hizo ni hujuma za ndani..ya UT..........jichunguzeni wenyewe kabla ya kuchunguza wengine!!!..mwananchi wakawaida hana access na jikoni kwao.
 
Hebu tujikumbushe:

Kikwete chupuchupu

na Juma Kasesa (Tanzania Daima)

RAIS Jakaya Kikwete amenusurika kupata ajali baada ya gari alilokuwa amepanda kulegea gurudumu na kisha kung'oka muda mfupi baada ya yeye mwenyewe kuteremka katika gari hilo kwa dharura wakati akiwa ziarani jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9:15 katika Barabara ya Kilwa maeneo ya karibu na zilipo ofisi za makao makuu ya kampuni ya mafuta ya BP.

Kabla ya tukio hilo, msafara wa Rais Kikwete ulisimama ghafla na rais akahamishwa kutoka katika gari hilo aina ya Land Cruiser VX na kwenda katika gari jingine.

Watu walioshuhudia tukio hilo walilieleza Tanzania Daima kuwa, muda mfupi baada ya msafara wa rais kuendelea na safari, dereva wa gari alilohama rais alijaribu kulisogeza pembeni ya barabara, hatua iliyosababisha gurudumu la gari hilo kung'oka na kusababisha ligote chini upande wa mbele kulia.

Tukio hilo liliwashtua watu waliokuwa katika eneo hilo, ambao walianza kujadili ni nini kingetokea iwapo gurudumu hilo lingeng'oka wakati rais akiwa ndani ya gari hilo.

Tukio hilo la rais kulazimika kuhama kutoka katika gari alilokuwa amepanda lilikuwa ni la pili baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza akiwa katika maeneo ya Kimara Mavurunza.

Kikwete alikuwa katika ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi ya maji jijini Dar es Salaam.

Msafara huo ukiwa unaondoka Kimara ulisimama ghafla na kuzua taharuki kwa maofisa usalama na wananchi baada ya kuona Rais Kikwete akishushwa ndani ya gari alilokuwa amepanda na kuingia katika gari jingine baada kupata hitilafu huku mvua kubwa ikinyesha.

"Ni kweli matukio hayo yalitokea, katika tukio la kwanza gari alilopanda lilipata hitilafu baada ya gea kugoma kubadilika wakati katika tukio la pili, gari alilopanda lilipata pancha," alisema Rweyemamu.

Alipoulizwa kuhusu taarifa za gari la pili kung'oka gurudumu hata kusababisha kuitwa kwa gari la kubeba magari mabovu, Rweyemamu alikanusha habari hizo na akasema hazikuwa sahihi.

"Ndugu yangu yaani ninyi mnaona taarifa za matatizo ya kawaida ya magari aliyopata rais ni muhimu kuliko adha za maji ambazo alikuwa akikagua katika Jiji la Dar es Salaam?" alihoji Rweyemamu.

Mwandishi wa habari hizi alimweleza Rweyemamu kuwa, gazeti hili liliona umuhimu wa suala hili kwa kuwa lilikuwa likigusa usalama wa kiongozi mkuu wa nchi moja kwa moja.

Jibu hilo lilisababisha Rweyemamu amuombe mwandishi afuatilie kuhusu ukweli wa taarifa hizo na ndipo baada ya muda usiozidi dakika 30 alipiga simu chumba cha habari na kulihakikishia Tanzania Daima
kuwa hitilifu za magari alizokabiliana nazo Rais Kikwete zilikuwa ni za kawaida.

MY TAKE: Gari kuzimika kwa kuwa na mafuta machafu, ni jambo la kawaida.
 
Kwenye hiyo bluuu...tatizo si kuzimika kwa gari, tatizo ni imefikiaje magari ya msafara wa rais yakawekewa mafuta machafu/yasiyo ya kiwango??!!! Inakuwaje magari ya msafara wa rais yakaweke mafuta kwenye vituo vya watu binafsi???? Haingii akilini...
 
Please Mheshimiwa Rais kama unanisoma hapa
REACT BASI MAANA SISI HATUNA IMANI NA WASAIDIZI WAKO.
Haiwezekani maisha yako yakawa hatarini two times halafu unaendelea kuwaga smile na bashasha kana kwamba kilichotokea ni mkono wa MUNGU.

Halafu kama magari yako yanajazwa mafuta uswazi basi tujue kuwa kuna hitilafu ktk menejiment yako.

REACT BANA AU LA TUNAKUNGOJA JUKWAANI UJIBU MASWALI YETU
 
Hapo ndio watapata sababu ya kununua hayo ma-VX V8 kisa yana sensors
 
zamani magari yote ya serikali yalikua yakijazwa mafuta ujenzi na kufanyiwa service huko au TEMESA. Lakii sasa tunaona magari hayo yakifanyiwa service katika gereji bubu na hata kujazwa mafuta ya ''dripu''i.e. mafuta ya wizi yanayohifadhiwa kwenye madumu. Huu ni ufisadi na usishangae VX la milioni 200 kupaki kisa injini imeharibika kwa mafuta yalichakachuliwa. Vilevile kuna haja ya mabadiliko kwa wale wanaoitwa watu wa system, hii ni hatari kwa usalama wa viongozi wetu. Yasipofanyika mabadiliko, ipo siku yakatokea makubwa...Naogopa sasa mara ari limezima, mara tairi limechomoka...kesho je....................
 
Wataalamu wa magari.

Naomba kujulishwa kuzimika kwa gari kuna effect gani na maisha? ama jari.

Mimi nafikiri magari hayo yana sensor kwamba kama kuna kitu kibaya yanazimika dwiiiiiiiiiiiiii. Kama zilivyo senso za binafsi mfano gari yangu bila kuona vidole vyangu haiwaki inazimika dwiiiiii.

Magari ya wengine yawezekana hayazimiki kwa sababu hayana senso ya ku monitor maji. Ni hoja tu nawakirisha
 
bandugu, niliongea siku moja kuwa urafiki ni mbaya sana usipokuwa na kikomo, urafiki hadi kwenye usalama wa taifa, kuweka watu ambao wasio na elimu na uzoefu wa idara hiyo, sasa hilo ndio tatizo lake bwana. Sio idara hiyo tu, idara nyingi wamewekwa watu ambao hawafai kabisa na ndio wamechangia kwa asilimia 100% kutuletea maisha duni yaliyopo hivi sasa.

MR. PRESIDENT WAKE UP, KIKULACHO KI NGUONI MWAKO.
 
Uongozi upi bora kati ya Sudan na Tanzania?
Kwanini sudani wanatuacha mbali yani sie ni masikini zaidi karibu mara mbili yao? Sie watanzania propaganda nyingi kuongea sanaaaaaaaa bila kufanya kazi. Kila mmoja akituma na kufanya kazi uongozi wa kidhalimu una uawa wenyewe. Lakini kama sisi ni wazee wa domo kaya na uvivu uongozi wa kidhalimu kamwe hatakoma hata kije chama kutoka kwa Malaika wa Mbinguni.
 
Bona

Mafuta ya magari ya serikari yalikuwa hayawekwi Ikulu ndogo. Mikoa yote ina ofisi za Bohari ya Mkoa, ambazo mara nyingi zilikuwa ndani ya compounds za Ujenzi (TANROADS). Inaelekea UFISADI umeua utaratibu huo, na matokeo yake ndio hayo.
 
bandugu, niliongea siku moja kuwa urafiki ni mbaya sana usipokuwa na kikomo, urafiki hadi kwenye usalama wa taifa, kuweka watu ambao wasio na elimu na uzoefu wa idara hiyo, sasa hilo ndio tatizo lake bwana. Sio idara hiyo tu, idara nyingi wamewekwa watu ambao hawafai kabisa na ndio wamechangia kwa asilimia 100% kutuletea maisha duni yaliyopo hivi sasa.

MR. PRESIDENT WAKE UP, KIKULACHO KI NGUONI MWAKO.

...Nakuunga Mkono. Ndio maana siku hizi unaangalia watu wnaopaswa kuwa walinzi wa raisi unajiuliza kama ni mameneja fulani. Angalia kwenye ile thread ya Walinzi wa Viongozi uone tofauti ya wa kwetu na wale wa Wenzetu! Mizaha na kujuana Kila Mahali hata pasipostahili.
 
Ngojeni matokeo ya uchunguzi kabla ya kuendelea na conspiracy theories zenu
 
.......likely more to come!!! tatizo kubwa kabisa ninaloliona ni Mkuu mwenyewe kuwa kimya na haya mauzauza yanayomtokea kwenye msafara au ratiba zake. Hii inanifanya nishawishike kuamini kwamba Mkuu anajua kwamba hiyo ni subotage ya wahathirika wa fujo zake za 2000 na 2005 ndio maana anakuwa kimya probably anaishughulikia kiutu uzima. Hofu yetu sijui,ni mkasa gani utafuta!!
 
Tatizo hapa sio sabotage ya maadui zake, maadui huwa wapo tu ndo maana viongozi huwa wanalindwa na wanakuwa na taratibu zao, tumezidi uzembe na ujinga ndo maana wakenya wanatusema.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom