Magamba ya JK yameganda

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
LICHA YA KUTOLEWA SIKU TISINI AMBAZO KIMAHESABU ZIMEISHA JUMAMOSI YA TAREHE 25 JUNI 2011 BADO MAGAMBA YAMEGANDA CHAMANI
HAWA JAMAA WANA UTANI KWELI NA WATANZANIA

WACHA TUONE WATAKUJA NA SERA GaNI BAADA YA MAGAMBA KUGANDA
 
Jk hana uwezo wa kuondoa magamba ndio maana lowasa akamponda juzi juu ya udhaifu wa kuchukua maamuzi magumu

hata gamba linajua jk hawezi kuliondoa
 
Tangu lini gamba la kobe likatoka kirahisi? Unataka atoke damu na kufa?
Umena ukweli hapa! Hata kobe anajua gamba lake ni mzigo mzito kwake na ndio maana hata tembea yake ni ya pole, huwa anatamani kuling'oa lakini akikumbuka anajua atakufa. Na hata c....c....m.... wanalitambua hilo! Ukishajua tu kuwa huu ni mkaa usitegemea rangi nyeupe!
 
Hawakuwa na hoja za msingi bali walikurupuka na mwenyekiti wao, ngoja tuone Jakaya atatwambia nini kama magamba waliovua yanaendelea kutengeneza nguo zao wenyewe.
 
wayatoe hayo magamba unataka wabaki na mifupa? hawa magamba tutawatoa cc wenyewe kama wameshindwana!
 
Jamani mbona mi sioni asiye na Gamba pale CCM, atatoka nani abaki nani? na pia hawa watu wametufanya sisi watoto, tukichukulia Gamba la kobe, huwa halitoki, ukilazimisha kutoa na mwisho wake, ukisema la nyoka inamaana unamng'arisha zaidi, na baada ya muda mfupi litazeeka tena na kuwa uchafu, so ni magamba yapi? kwa mantiki hii ni kwamba huu ni ulaghai, hamna kipya zaidi ya kutuambia hawatabadilika ng'o kama tukifuata maana kamili za magamba!
 
Nafikiri kuvua magamba ni msemo tu wa CCM kama misemo mingine ya kujipa moyo kinafiki huku wakijua hawawezi kuyatekereza.Hizi ni propaganda zilizoshindwa kabla ya kuanza.Tusipoteze muda wetu kujadili Magamba ya CCM hizo ni mbinu zao za kuhadaa wananchi.CCM wanapoteza muda.
 
Gamba limeanzia kwake, unadhani kuvua gamba chama kitabaki?
Hayo ni maigizo ambayo mtaalamu mmoja amekusudia kuyaandikia
script ili yafanywe thamthilia
 
Magamba yanaujasiri usiopimika, kushindwa kwao ndio furaha yetu! Magamba oyeeeee?
 
The chairman doesn't have the balls,mark my words akijaribu tu linavuka hadi la kwake anajua hili vizuri tu,ajaribu tuone.
 
Back
Top Bottom