Magamba ya ccm ni bomu lililokwisha ripuka

kwitega

Senior Member
Apr 10, 2012
166
49

Wakati huu na huko tuendako kama taifa; tutasikia na kuonamengi kutoka kwa wanasiasa wanaotaka urais 2015. Wapo wanaozunguka kila mahalihususani kwenye madhehebu ya Dini wakitoa jumbe zinazolenga kushawishi aina yawapiga kura tulionao ili waamini kwamba; wanasiasa hao wanafahamu matatizo yawapiga kura hao lakini serikali iliyoko madarakani imeyafumbia macho.
Katika pita pita yao huku na kule wakijaribu bahati yao yakupata urais 2015; wanasiasa hao kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambaochama hicho kinawaita magamba; wanafanyavikao rasmi na visivyo rasmi huku wakiionya na kuikosoa serikali ya rais Kikwetekwa kile wanachodai kuwa imeshindwakutatua tatizo la ajira kwa vijana kiasi cha kusema; changamoto hiyo ni bomulinalosubiri kuripuka.
Hakuna ubishi kuwa hoja yao ni ya msingi na haipaswikupuuzwa. Lakini wanasiasa hao ambao wamekuwa serikalini kwa muda mrefuwakishika nafasi mbalimbali za juu za uongozi wa taifa letu ikiwa ni pamoja nauwaziri ; wanaposhindwa kueleza bayana kiini cha tatizo la ajira kwa vijana waTanzania na kutoa ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo, tunashindwakuamini kama kauli zao zina dhamira ya dhati ya kukabiliana na changamoto hii.
Uongozi ni dira ya kuwaongoza na kuwafikisha wafuasi sehemuiliyokusudiwa. Kiongozi kazi yake ni kuonyesha njia kisha anatangulia mbele nawengine wanamfuata. Wanasiasa wa aina hii wanaposhindwa kuona na kueleza chanzocha tatizo la ajira kwa vijana na kuonyesha kwa vitendo ushiriki wao katikakutatua changamoto hii; binafsi naona kauli zao zimejaa tamaa iliyojifichanyuma ya pazia la siasa, lengo likiwa ni urais 2015.
Hatuwezi kubeza kauli zinazotolewa na wanasiasa wetu hasawanapoikosoa serikali hata kama wanataka urais 2015 na kwa kuzingatia ukwelikwamba; pamoja na mapungufu yake, Katiba yetu inaruhusu kila mtanzania kuwa nauhuru wa kutoa maoni.
Cha msingi hapa ni kuangalia na kupima hoja wanazotoa kamazina maslahi ya dhati ya taifa au zinalenga kuwajenga kisiasa wao binafsikuelekea 2015.
Moja ya vyanzo vikuu vya kukosekana kwa ajira ya vijana nimatumizi mabaya ya raslimali za taifa ikiwa ni pamoja na mali asili, matumizimabaya ya madaraka kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia watanzania kwanafasi mbalimbali ambapo hapa yanatokea masuala ya ubinafsi ambayo yanajielezakatika misingi ya na rushwa na ufisadi, nikitaja vyanzo hivyo kwa uchache.
Nimetaja mambo haya kuwa ni baadhi ya vyanzo vya kukosekanakwa ajira za vijana kwa sababu kuu moja kwamba; kwa pamoja hujuma hizi dhidi yawatanzania, zinaikosesha serikalimabilioni ya fedha ambapo pamoja na mambo mengine; fedha hizo zingewezakutumika kujenga mazingira ya kuongeza ajira kwa vijana.
Ukiangalia rekodi za uporaji na wizi katika Akaunti yaMalipo ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzanani (BoT), Kagoda, IPTL, Meremeta,Richmond, ununuzi wa rada, mgodi wa Kiwira, Uuzaji wa Mabenki na Mashirikambalimbali yaliyokuwa ya umma kwa bei za sawa na bure na mikataba ya madiniisiyozingatia maslahi kwa nchi ili ilimradi matumbo yao yanajaa; utabaini kuwa,mabilioni ya fedha zinazotokana na walipa kodi ambazo zingechangia kupunguzatatizo la ajira kwa vijana, zimeishia kwenye matumbo ya watu binafsituliowaamini kwa kuwapa nafasi za uongozi kupitia sanduku la kura.
Je, ni kweli kwamba; wanaoimba wimbo wa tatizo la ajira kwavijana hawaoni haya kuwa wao ni sehemu ya tatizo hilo ?
Kwa bahati mbaya kabisa wanasiasa hawa ni miongoni mwawatuhumiwa wa ufisadi. Hivyo; huenda wanalizungumza tatizo hili ili wasionekanekuwa wao wenyewe ni sehemu ya tatizo lenyewe.
Wanasiasa hao wanategemewa na chama chao kujiuzuru nyadhifazao bila shuruti kwa staili ya kuwataka wajivue magamba na kwamba wasipofanyahivyo watavuliwa kwa nguvu kwa madai kuwa ni mafisadi wanaokichafua chama hichombele ya jamii.
Ni kwa mtazamo na mazingira haya inapelekea baadhi yetu tuamini kuwa huendakweli wanasiasa hawa walishiriki kwa njia zote katika mkataba wa kitapeli waRichmond ambao madhara yake yatabaki kuwa historia ya mambo mabaya yaliyowahikutokea hapa nchini.
Kamati ya Bunge chini ya Mbunge wa Kyela Dkt HarrissonMwakyembe iligundua kuwa; wanasiasa hawa walitumia madaraka yao vibaya kwakushnikiza serikali kusaini mkatababaina yake na Richmond, kampuni ambayohaikuwa na sifa wala uwezo kifedha.
Hadi hivi sasa; wanasiasa hawa wanatetea maamuzi ya kuipa Richmondmkataba wa kuzalisha umeme kwa kigezo kuwa kulikuwa na uhitaji makubwa wanishati hiyo muhimu, na kwamba kuendelea kuchelewa kupata suruhisho la dhalurahiyo ya umeme; kungepelekea mtikisiko mkubwa wa uchumi wa taifa letu.
Hata hivyo; taratibu za kushughulikia suala nyeti kama hilo lilihitaji umakinimkubwa na kujiridhisha pasipo shaka kwamba maamuzi ya kuipa kampuni yoyote mkatabawa kuzalisha umeme wa dharura kweli yangeweza kutimiza lengo lililokusudiwa.
Ni dhahiri kuwa kilichotokea katika mchakato mzima wa kuipa Richmond mkataba wa kufuaumeme kinaonyesha jinsi taifa linavyopungukiwa viongozi wanaoweza kufanyamaamuzi sahihi ya utatuzi wa changamotozinazolikabili taifa zikiwemo za dharura.
Ni kutokana na maamuzi hayo ya hovyo kuwahi kufanywa nawaziri Mkuu katika miaka ya hivi karibuni; kwa mara ya kwanza nchi ilikuwa gizani kwa kipindi cha miezi mitano ambapo pamoja nasababu nyingine tatizo hili limechangia kwa kiasi kikubwa kuyumba kwa uchumi wetu kutokana na kushuka kwashughuli za uzalishaji.
Nishati ya umeme ni moja ya vyanzo vya ajira nyingi kwa vijana katika maeneo yaviwanda vidogo na vikubwa, mashine za kuranda mbao, kusaga nafaka, kuuzavinywaji baridi, saluni nk. Je, vijana wangapi waliathirika na mgao wa umemekutokana na serikali kuingia mkataba na Richmond?
Je, hili si bomu ambalo tayari lilitegwa na kulipuliwa nawanasiasa hawa hawa ambao leo wanapita huku na kule wakitafuta wachawi watatizo hili wakati wao binafsi ni miongoni mwa wachawi hao?
Tunafahamu kuwa hospitali zetu nyingi hazina mashine zakuzalisha umeme au mfumo wa umeme unaotokana na nishati ya jua. Hivyo; kwavyovyote vile wapo wagonjwa waliopoteza maisha kwa kukosa huduma ya upasuajikutokana na kwamba uendeshaji wa mashine za upasuaji hutegemea umeme wa Tanesco.Je, hili nalo si bomu lililotegwa na kuripuliwa na wanasiasa hawa hawa?
Kuna migomo mingi inatokea kiasi cha kugharimu maisha yabaadhi ya watanzania kama vile mgao wa madaktari. Fedha zinazotafunwa kwa njiaza kifisadi ikiwa ni pamoja na katika mikataba na makampuni ya aina yaRichmond, zingeweza kupunguza uhitaji wa madai ya watumishi wa umma wanaogomakutoa huduma kutokana na maslahi duni. Je, hili si bomu lililokwisha ripuka?
Wanasiasa hawa wanaposema tatizo la ajira kwa vijana ni bomulinalosubiri kuripuka na kuishia kuilamu serikali kwamba haifanyi vya kutoshaili kutegua bomu hilo; huku wenyewe wakijaribu kujipambanua mbele ya ummakwamba wana mawazo na mbinu za kutatua tatizo hili, ni vigumu kuwaamini kwaniwao binafsi wana mchango mkubwa katika kukua kwa tatizo lenyewe.
Tungekubaliana na hoja yao kama wangetaja chanzo cha tatizohili, kutoa ushauri na kuonyesha njia ya kulitatua kwa vitendo. Tungeaminikwamba; wanaongozwa na hisia za uzalendo zaidi na si maslahi binafsi yakisiasa.
Kwa nyadhifa zao tunazozijua wanauwezo wa kumfikia hata mkuuwan chi ili kumshauri jinsi ya kutatua tatizo hili lakini hatujaona dalilihiyo, badala yake wanasiasa hawa wanatumia vyombo vya habari na majukwaa yasiyorasmi kuisema serikali na dola ile ile ambayo wao ni sehemu yake.
Hapa tuelewe nini kama siyo kampeni za kutaka urais nakulaghai watanzania? Hivyo; kama wataendelea na hoja hizi hizi, wapuuzwe..
Kwa upande wake pamoja na kujitetea kuwa imeongeza ajiraserikali bado haijafanikiwa kuweka uwiano unaoonekana kati ya jitihadainazofanya na changamoto ya ajira kwa vijana iliyopo hivi sasa. Kutokana naukubwa wa tatizo; juhudi za serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa vijanahazionekani bayana mbele ya macho ya watanzania.
Mfano; hakuna jitihada za kuanzisha viwanda vinavyowezakuajiri vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali na kilimo cha kisasa ambacho kinawezakuwavutia vijana wengi au kuboresha uzalishaji wa umeme ili vijana wawezekujiajiri badala yake tunapigiwa porojo za kutengeneza mvua kutokana na mawingukwa maneno ya Waziri Mkuu mstaafu. Huku ndiko kuboresha kilimo na umeme kweli?
Jitihada za serikali katika kutatua tatizo hili haziwezikufanikiwa kwani mazingira yanayoweza kutoa fursa nyingi za ajira yanatakiwakujengwa kwa mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ambapo fedha zinazopoteleamifukoni na kwenye matumbo ya watu binafsi zinapaswa kutumika katika mkakatihuu.
Kama watawala na wanasiasa wetu wataendelea kukumbatiawatumishi wa umma wanaoisababishia serikali hasara kwa kutumia madaraka yaovibaya; huko tuendako watabebeshwa lawama sawa na wanasiasa wanaodaiwa na CCMkuwa ni magamba ambao bomu walilotega na kuripua linaendelea kuathiriwatanzania wakiwemo vijana.
 
Back
Top Bottom