ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
Kwa muda sasa nimesikia huyu kijana amekuwa kitandani kutokana na malazi. Hivi karibuni nilisikia kuwa jamaa anaumwa 'seriously' kwa nyeti za juu juu ni kwamba anaugua saratani ndani ya kichwa. Binafsi ikaja taswira jinsi huyu dogo na wenzake kina Msanja, Seki na wengineo jinsi walivyotumika na CCM katika kampeni zao za uchaguzi. Kama sijakosea, hawa jamaa walipita kila mahali nchini kote ambako magamba walijua kuna mtaji wa kura za wananchi. Hakuna ubishi kwamba kwa sehemu kubwa ushindi wa magamba mwaka 2005 ulichangiwa pia na hili kundi ambalo nadhani sikosei nikiliita TOT namba 2. Binafsi nilidhani kwamba walau CCM wangemkumbuka huyu dogo hata kwa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi maana namuona ni kama familia ya magamba kwa jinsi alivyokuwa akipigania kura zao kuliko walivyomtosa sasa ambapo nna uhakika kwa muda aliokaa hospitalini, ni wazi uwezo wa matibabu ya juu na yenye ubora kwa sasa hana. Wakati dogo anaendelea kuugua pale muhimbili, tafadhalini kwa wale ambao ni wafuasi wa magamba humu jamvini, wafikishieni kina Miraji taarifa hizi wazifikishe kule kwa watoto wa magamba-UVCCM-walau waonyeshe ubinadamu kwa kumsaidia huyu kijana kwani mchango wake kwa magamba ulikuwa si haba. Nawasalimu wote, Asanteni!