takashi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 905
- 188
Umeelewa kilichoandikwa? Kama hukuelewa tuambie tutakusaidia, imeandikwa kwa lugha abayo si yetu kwahiyo uwezekano wa kutoelewa ni mkubwa na si kosa ni lugha tu kama vile mtu mwingine asiyeweza kuelewa kiarabu n.k
Sitta amesema kama kaimu waziri mkuu wa serikali ( sio maoni yake) akifanya majumuisho ya wizara husika. Amesema hakuna suala la serikali tatu akatoa mfano wa kiungwana, kama Zbar haiwezi kulipa Tanesco itaweza kulipa fees ya muungano. Akaendelea hakuna cha serikali tatu, kama kuna wanokereka kuna njia rahisi jitokezeni muungano uwepo au uvunjike. Kumbuka ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni (kaimu PM) na kauli zake zipo katika Hansard ya bunge kama kauli ya serikali na sio Sitta.
Kuna aliyewadanganya wzbar kuwa ikiwepo serikali ya Tanganyika mambo yatakuwa mazuri. Watanganyika wanasema vunja muungano hawana cha kupoteza na hawako tayari kubeba mzigo wa serikali ya tatu, ndio maana nimeweka hiyo aricle ya kuonyesha south sudan wako namna gani.
Wabara hawahitaji kura ya maoni, ya nini!!! kura ya maoni bara itapigwa ili iweje.
Hamna haja ya kura ya maoni nani amewaliazimisha muishi bara! ondokeni msasani, kigamboni, makorora, ilala, Tabora, Lindi, n.k muungano utakuwa haupo. Hamuwezi kubebwa mgongoni halafu mnarusha mateke, hapo lazima mtadhibitiwa.
Hakuna mbara anayehitaji kura ya maoni, ili iweje na ya nini, imsaidie nini. Zbar inahusu nini maisha ya mbara, what's Zbar.!!
Mimi hiyo article yako nimeielewa vizuri...Kuhusu lugha ya kiingereza mimi naelewa vile vile, nasio kiingereza tu, kiarabu,kituruki na kijapani...
Unachojaribu ni kuwatisha wazanzibari eti muungano ukivunjika ete wao ndio watapata hasara, think again... Sitta, na kundi lake wanajulikana kama hao ndio wakina Nyerere walio bakia... Bado ana mawazo yale yale ya miaka ya 60s,70s,80s na 90s. Kama na wewe uko katika kundi lao basi muda wenu umekwisha... Nyakati hizi sio zile. Mambo ya kikoloni yamepitwa na wakati...
Kuhusu serikali tatu, sio wazanzibari tuu,hata watanganyika wengi wanataka hivyo. Sitta na kundi lake wako katika utawala na hicho ndicho kinacho mdanganya...Vyama vyote vya upinzani vina support kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu...Mkae na mkumbuke kuwa utawala wa CCM unaelekea ukingoni...Hakuna mtu wala chama cha siasa kitakacho weza kuzuwia vugu vugu la mabadiliko katika siasa za TZ...
Deni la TANESCO, wazanzibar hawatalilipa waziri wa nishati alishawafahamisha hao wahusika...Siri ya deni inajulikana na hizo ni mbinu za mtawala ,kumpandikizia madeni anaemtawala... Wakati utafika , wanzanzibari watarudi kwao na watanganyika walioko zanzibar watarudi kwao...
Nyakati za kikoloni zimekwisha...