MAFUTA yanamwagika bandarini

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,712
Kuna mtapanyiko wa mafuta (diesel/ petrol) pwani yote eneo la pwani ya bandarini. Kuna speculations kwamba kuna meli imevujisha hayo mafuta ama bomba la tipper limepasuka....

Nimepiga picha kwa simu yangu ila mchina amegoma kusend file through buetooth.

Kinachoendelea ni kwamba wananchi wamejazana kwenye pwani wakipembua na kuchota mafuta yaliyomwagika. Eneo lote la feri linanuka mafuta na kikosi cha wanamaji wanajitahidi kumwaga DAWA kupunguza makali ya harufu. Mnaokwenda kigamboni mjihadhari sana na utelezi kwenye gati na pantonin.

Ni hatari sana eneo hilo endapo atatokea mzembe akaamua kutupa kichungi cha sigara.

Kama kuna anayejua chochote atupe taarifa kamili
 
Kwa taarifa nilizododosa pale ni kwamba yalianza kumwagika jana jioni kama si usiku....

Ila pwani yote imeshatota mafuta kwa mda huu
 
Walio karibu na maeneo ya ferry.
kuna any progress?
 
mafuta bado yanamwagika kwa wingi.... na watu ndio wanazidi kuchota... maskini wasiokuwa makini gari zao zitakufa injini mda c mrefu na hasa wenye madaladala kwani hao naamini ndio watakuwa victims wakubwa ... hence madereva na makonda wao nao wamejumuika kuchota mafuta hayo.... CAUTION kwa wamiliki wa madaladala usikubali dereva akaenda kujiwekeA MAFUTA
 
07_10_29scnw.jpg
Akina mama lishe wa eneo la Feri, Posta wa zamani Jijini Dar es Salaam wakiwa wamebeba madumu ya mafuta aina ya dizeli baada ya kuyachota majini. Inasemekana kuwa kuna meli ilikuwa imetoboka na hivyo kumwaga mafuta baharini( Picha na Evance Ng'ingo)
HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania
 
vipi hakuna askari waliotokea kuzuia vurugu hizo ? Hayo mafuta sio hatari kushika moto tusije anza omboleza
 
vipi hakuna askari waliotokea kuzuia vurugu hizo ? Hayo mafuta sio hatari kushika moto tusije anza omboleza

wenyewe wanadai wamepata bure...ni sadaka....in fact wanaokota 'hela'....mambo ya moto hayo wala hayapo vichwani mwao walau kwa sasa
 
jamni naomba mtume picha nyingi ili tuone maana ni issue inayosikitisha!
 
Nilipita feri jumapili ahsubui nikakuta ile pantoni ndogo inatumika kubeba gari ya faya wakimwaga dawa kupunguza nguvu ya harufu na mafuta pwani. Kwa mnaofahamu masuala ya mazingira naomba mkajionee jinsi fukwe ilivyoharibika kwa mafuta yanayounguzwa na jua maji yakipwa.

Niliona statement ya Injinia Chambo akielezea kuwa ni bomba lilipasuka likawaga mafuta. Ila mimi nina doubt kwamba isije ikawa ndo wajanja wamekunywa wese halafu ili kuua soo wakaamua kuvujisha bomba baharini ionekane ajali.

I am doubtfull
 
Back
Top Bottom