Mafuta yameanza kuchimbwa Tanzania

...labda ni mafuta ya fisadi Rostam na kishatoa onyo kali kwa Msanii kwamba asitwambie lolote Watanganyika. Kwa maoni yangu hata kama zingekuwa pipa 50 kwa siku basi Wabongo tunahitaji kufahamishwa.
 
ha ha ha ha isije kuwa ndo imefanya CUF kuolewa zenji ili muungano usivunjike ha ha ha ha ha
 
Uganda walisema wataanza kuchimba mafuta 2014,lakin mwezi uliopita kuna siri zimevuja wameishaanza kuchimba na wanauza kenya,na serikali imeshindwa kuwalipa waliofanya utafiti na kutengeneza mitambo,hivo kati ya mapipa billion 2 ya mafuta yoye yaliyomo,kampun itapata mafuta ya billion 1 kujilipa gharama zao,hivo mafuta ayataleta neema sana kwa uganda kama ilivyotegemewa,hivo serikali ya tanzania lazima iwe makin na mikataba,gharama zao za utafiti ni kubwa sana na kujilipa inabid wauze ayo mafuta hivo aitaleta neema kwa mtz
 
Wadau,leo asubuhi nilikua nasikiliza redio MAGIC FM katika kipindi cha morning magic,katika kile kipindi cha zaidi ya habari mwandishi Kibwana Dachi ametuambia leo ni siku ya tatu (3) tangu mafuta yaanze kuchimbwa Tanzania.Kwa siku wanachimba mapipa 100 (mia moja).Hii ina maana kwmba tayari watakua wamechimba mapipa mia tatu.
Swali la kujiuliza ni kwamba,mbona hii ishu ipo kimya kimya sana?
Ina maana serikali haijui au wanataka kutuambia kuwa bado jamaa wanafanya utafiti?
jamani hebu tulifuatilie kwa kina hili jambo isije kuwa ndo mtindo ule ule wa wachimba madini.
Nawakilisha.
Usitegemee kama kuchimbwa kwa mafuta kutaisaidia Tanzania kama serikali ilioko madarakani inaendelea kusaini mikataba jini. Tutaishia kupewa 1%
At least tunapata 3% kwenye dhahabu
 
Usitegemee kama kuchimbwa kwa mafuta kutaisaidia Tanzania kama serikali ilioko madarakani inaendelea kusaini mikataba jini. Tutaishia kupewa 1%
At least tunapata 3% kwenye dhahabu

1% yote hiyo? Usishangae wakivuna mwaka mzima bure ukiuliza unaweza ambiwa yanafanyiwa uchunguzi kama yanafaa
 
Labda huyo mwandishi alikuwa hajui ni nini alichoambiwa. Uchimbaji wa mafuta bado upo kwenye hatua za utafiti. Ni kweli kuna baadhi ya maeneo ya Ruvuma basin kumeonyesha dalili za kuwapo mafuta, na ndiko huko ambako utafiti huo unafanyika katika hatua za mwisho mwisho


Well said MN,
Mie mwenywe niko kwenye sekta hiyo hiyo ya nishati, hizo habari za magic si za kweli. Utafiti wa uwepo wa mafuta bado unaendelea Bahai ya Hindi, bonde la Ziwa Rukwa, bonde la Ziwa Tanganyika na maeneo mengine ya kando ya bahari. BADO mafuta hayajapatikana ingawa kuna dalili za uwepo wa miamba ya mafuta karibu na mpaka wa Msumbiji.
 
Ukifanya utafiti wa kina,migogoro mingi duniani inatokea either kwa nchi zenye mafuta au kwa wale wanaokodolea macho mauta yao.Vita vya wenyewe kwa wenyewe kama Nigeria,Mgogoro wa Dafur,matatizo yaliyopo Chad,vita vya Iraq,Kuwait,Libya na hata fukuto la migogoro ya nchi za kiarabu yote inatokana au kusababishwa kwa namna moja au nyingine na mafuta.
Watanzania wenzangu,mafuta yawe yamepatikana au kama utafiti unaendelea naomba tuwe makini tusije kutoana roho.
Nafikiri mnakumbuka jinsi wenzetu walivyogeuka mbogo pale ilipotajwa kuwa mafuta ni swala la muungano.
Tuwe makini.
 
Tanzania kama tumerogwa, mbona bado tunaishi kama enzi zile mzungu akionekana suspiciously basi ni kaburu anataka kulipua ikulu? Are we really in 2011 heading for 2012?????
 
Mafuta yaanza kuchimbwa mtwara,na kampuni husika imekiri na kuwa inatoa mapipa
300 kwa siku tangu tarehe 16/12/2011 ila waziri Ngeleja adai kampuni bado inafanya utafiti kwa miaka mitano.

Taarifa hii imetolewa na Mwanahabari wa magic fm (kibwana dachi) na kusisitiza
kuwa wananchi waamke

Source: Magic fm 19/12/2011, morning magic

Hivi iweje viongozi wetu tuliowapa dhamana katika maamuzi kuudanganya umma, hivi mafuta mapipa 300 kwa siku huo ni
utafiti kweli, je miaka mitano watakuwa wamechukua mafuta kiasi gani?

Rasilimali zetu lazima tuzilinde sisi wananchi la sivyo wataendelea kugawana na kuendelea kuwadanganya umma wa watanzania kwakujua kuwa sio wafuatiliaji wa
mambo. Tuamke jamani, tuache itikadi za kichama.

Source:mwanahakati wa fb
(Mbagala chadema Igunga mbegu).
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mafuta yaanza kuchimbwa mtwara,na kampuni husika imekiri na kuwa inatoa mapipa
300 kwa siku tangu tarehe 16/12/2011 ila waziri Ngeleja adai kampuni bado inafanya utafiti kwa miaka mitano.

Taarifa hii imetolewa na Mwanahabari wa magic fm (kibwana dachi) na kusisitiza
kuwa wananchi waamke

Source: Magic fm 19/12/2011, morning magic

Hivi iweje viongozi wetu tuliowapa dhamana katika maamuzi kuudanganya umma, hivi mafuta mapipa 300 kwa siku huo ni
utafiti kweli, je miaka mitano watakuwa wamechukua mafuta kiasi gani?

Rasilimali zetu lazima tuzilinde sisi wananchi la sivyo wataendelea kugawana na kuendelea kuwadanganya umma wa watanzania kwakujua kuwa sio wafuatiliaji wa
mambo. Tuamke jamani, tuache itikadi za kichama.

Source:mwanahakati wa fb
(Mbagala chadema Igunga mbegu).

Dah hi aibu
 
Asikudanganye mtu, ugunduzi wa mafuta nchini Tanzania BADO. Uzalishaji hauwezi kuanza kabla ya ugunduzi. Alichoeleza Mhe. Ngeleja (Mb) ni nadharia inayowasukuma wawekezaji kufikia uamuzi wa kuwekeza mitaji katika utafutaji wa mafuta (zaidi ya US$200 milioni kwa miaka 25), hususan, na kama kigezo cha kufikia mgawanyo wa maduhuli kati ya Serikali na mwekezaji.
 
kama jicho langu la tatu halijapoteza kumbukumbu,muheshimiwa katika ziara yake mikoa ya kusini alisema karibuni wataanza chimba mafuta natumaini ndio haya wameanza.
makabwela haina haja yakuambiwa mbona tunayo natural gas ya kutosha ila nchi wanaruhusu kuingizwa mitambo inayo tumia mafuta mazito badala ya Gas
 
hahahaha pipa100 kwa siku hata dsm hazitosh

Nini Dar es salaam; pipa moja si lita 200?! kama ndivyo, pipa moja si linatosha kuhudumia wabunge 4 (@ 50 lts) kwa siku?! Maana yake nini, pipa 100 si wabunge 400?! Hawajafika 400 hawa?! Kama hawajafika, ukichanganya na wakuu wilaya je?! Du, nahisi nimeenda mbali, delete wakuu wa wilaya, paste makatibu wakuu wa wizara...kwisha kazi!
 
Back
Top Bottom