Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuta ya Samaki

Discussion in 'JF Doctor' started by stephot, Jul 12, 2012.

 1. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 2,127
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 63
  Wana Jf hebu tusaidiane hapa,nilimtembelea jirani yangu wiki iliyopita kwa ajili ya lunch,baada ya msosi nikaona anabugia vijiko 2 vya kimiminika kilichokuwa kwenye chupa,nika muuliza unaumwa,akasema kuwa kila baada ya mlo yeye huwa anatumia vijiko 2 vya mafuta ya Samaki akanieleza kuwa yanasaidia kuboresha ubongo na kuufanya uwe na uwezo mkubwa wa kukumbuka,kwa wale wataalamu hebu tujuzane jamani kuna ukweli wowote katika hili?
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,090
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 83
  mimi sijui sana ila kwa uzoefu wangu mdogo ni kwamba mafuta ya samaki yana vit A hii inasaidia mambo mengi sana mwilini ikiwamo kukumbuka kuona na pia ni anti oxidant ambayo inatumika ku absorb macro molecules a radiations ambazo mtu umezipata kutoka kwenye mazingira. zaid ya hapo sijui na naomba nisahihishwe hapa kama nimekwenda chaka manaake nisije nikawa sijui.
   
 3. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 18
  Kwa ufahamu wangu mafuta ya samaki kwa mtu nzima ambaye uwezo wake wa kukua umefikia kikomo yanawasaidia kuepukana na magonjwa ya misuli ya moyo(Myocardial infaction) na kuganda kwa rehemu kwenye mishipa ya damu.
  Kwa watoto ambao bado wanaendelea kukua, mafuta ya samaki yanawasaidia kuweza kukua vizuri na kuwaongezea joto mwilini
   
 4. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya mafuta ni mazuri sana mkuu pia inashauriwa apewe pia mtoto mchanga, inamfanya anakuwa active sana kwa mambo mengi hasa darasani.
   

Share This Page