Nimekerwa na tamko hili la Waziri wa Afya la kupiga marufuku mafuta ya vilainishi ya mashoga

aminiusiamini

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,577
2,220
Habari wakuu,

Kwanza,niseme nimechukia sana kusiki habari za Waziri wa Afya ambaye yeye na Naibu wake kila kutwa wamekuwa ni viongozi wa matamko.

Kwa kifupi kuna baadhi za teuzi za Rais naona kama zmepwaya kabisa.

Kitendo cha huyu Waziri kutangaza kupiga marufuku mafuta ya vilainishi vya mashoga mimi nimeona ni makele yaliokuwa hayana maana. Je anataka kutuambia kuwa ushoga umezidi kuliko tulivyodhani?

Je,hilo ni tamko la serikali nzima au yeye tu na utashi wake. Mimi nakumbuka Kikwete alishaulizwa BBC au nadhani CNN kuhusu ushoga. Mzee alijibu kwa kupotezea kuwa watz wana matatizo zaidi ya hilo na wala sio la maana muda huu. Na niliona ni bora Rais Kikwete alivyojibu maana katika mila zetu hatujui haya mambo. Haya yamekuja tu.

Kingine,kwani kusema kupinga utumiaji wa mafuta ya hao watu kutazuia wao kufanya mapenzi kinyume na maumbile?

Nadhani hawa viongozi wa Magufuli wanahitaji hekima na sio kutaka sifa za kuonekana wanajua kufanya kazi. Naomba sana tusijaribu kulipa hili suala muda wa majadiliano. Tuachane nalo kwasababu kuna mambo mengi ya msingi ya kuongelea na sio ushoga.
 
Haya mafuta pamoja na vingine vinavyochochea ushoga na ulawiti vipo kisheria na vinatambulika na vina kituo chake kamili pale hospitali ya Muhimbili, si kwamba vimeingizwa kimagumashi la hasha! ilikuwa ni mojawapo ya masharti ya kupata mikopo na misaada toka kwa wazungu, kutoa tamko kama lile ni upuuzi wa kiwango chake
 
Nadhani sio nathani.

Any publicity is good publicity. Ushoga unachanja mbuga kiulaini siku hadi siku kwa story na habari kama hizi.

Waziri wa afya ana pwaya sana ipo wazi.
 
Mkuu nakubaliana nawewe kabisa. Kuna vitu vingine anaweza kukaushia. Ushoga katika jamii na mila zetu ni kitu caha ajabu sana.
 
Nadhani sio nathani.

Any publicity is good publicity. Ushoga unachanja mbuga kiulaini siku hadi siku kwa story na habari kama hizi.

Waziri wa afya ana pwaya sana ipo wazi.

Mkuu hawa viongozi wanataka sifa tu waonekane na wao wanafanya kazi. Wanathani kila kitu ni cha kuongelea.

Nashukuru kwa mchango wako.
 
WEWE NAONA tamko la waziri wa afya kupiga marufuku VILAINISHI mahususi katika kuhamisisha NGONO ya jinsia moja katika hospitali za serikali limekumaliza acha hizo tabia utakufa MBIO!

Tatizo elimu yetu ndio mbovu. Nina uhakika hujasoma uzi na ukanielewa,ukaja mbio kupost upuuzi,na upumbavu wako.
 
Kawapa promo mashoga bila kujua mpaka waliokuwa hawajui kuwa kuna mafuta walikua wakipewa wameshafahamu,huku wengine wakihoji yawezekana serikali wameruhusu ushoga kimyakimya ila wanapinga kinafiki
 
Mkuu nakubaliana nawewe kabisa. Kuna vitu vingine anaweza kukaushia. Ushoga katika jamii na mila zetu ni kitu caha ajabu sana.

Si hajabu kihivyo, unaambiwa katika wanaume 10 mmoja kati yako anashika ukuta au stuli. Kwa kifupi ni hivi, wewe na wenzako 9 kati yenu mmoja au Zaidi ni mvaa shanga kiunoni.
 
Haya mafuta pamoja na vingine vinavyochochea ushoga na ulawiti vipo kisheria na vinatambulika na vina kituo chake kamili pale hospitali ya Muhimbili, si kwamba vimeingizwa kimagumashi la hasha! ilikuwa ni mojawapo ya masharti ya kupata mikopo na misaada toka kwa wazungu, kutoa tamko kama lile ni upuuzi wa kiwango chake

Hatari sana!! Sikujua hili kabsa. Kumbe serikali imehalalisha kwa mlango wa pembeni. Mungu atusaidie kabsa.
 
Back
Top Bottom