Mafuta ya IPTL yamenunuliwa wapi?

Labda ingechukua miezi sita kufika hapo bongo ingependeza zaidi

Mkuu Kibs,

Mimi naheshimu haki yako ya kuji-express!! Ina maana wewe hushangai haya maajabu!! Sote tunafahamu utaratibu wa kununua; haiwezekani ndani ya siku tatu supplier apatikane, apewe oda na mafuta yawe yamefika Dar port!!

Ukiangalia wizi wote wa nyuma, IPTL, Richmond huwa unafanyika katika mzaingira kama haya; "emergence" as they call. Ina maana tatizo la maji kupungua tunaliona leo? Kwanini tunapenda ku-solve matatizo yetu kwa zima moto?

They should wake up now na kujua enzi za zamani nimeisha, HATUOIGWI MCHANGA WA MACHO kamwe!!!:mad:
 
Bhaghosha,

Kwanza ni kampuni gani Iliopewa tenda ya kutuletea mafuta? Na kama ni kampuni yetu me sishindwi kuamini waka kwapua hata meli bandari yoyote ili mradi iwe na mafuta hata kidogo japo waje wayamalizie kwa mitambo ya IPTL na yatakayo pelea wataongeza wao, Kwani hamjiulizi walikokotoa wapi hayo mahesabu ya kuwa itatumia gharama ya zaidi ya bil 27 ati gharama ya mafuta, kulifanyika vitu vya kijanja janja tu.

twaielewa desturi na utendaji kazi wao na ndio maana watu wamewashtukia mapema ati kutaka kujifanya wamewahisha kutatuta tatizo la mgao wa umeme hiyo ni kwa muda huu tu,

Je kama wana weza watupe long term plan ya kutatua tatizo la umeme Tanzania nzima now now??

Kama hawajikanyaga hapo, si twajua tatizo la umeme tumelikuta tokea tumezaliwa mpaka leo ni stories tu
 
Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....

Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...

Ni mawazo yangu.

Du! Kumbe Zitto Kabwe alikua part ya hii Game? Yeye aliambiwa aanzishe wimbo wa washa IPTL na Dowans Taifisha... halafu hiyo ilikua pima joto tu! Deal na IPTL ilikuwa zamani mafisadi walisha maliza mahesabu... poleni wadanganyika!
 
Hapana Mkuu Kibs haya maswali lazima yaulizwe maana nchi yetu ufisadi umekithiri mno! Unakumbuka ni Watanzania wa US walioanza kufuatilia kuhusu Richmond kudai ni kampuni ambayo ina HQ Houston. Baada ya kugundua kwamba hili si kweli ndiyo kidogo kidogo uwongo wa RA na Richmond yake ukaanza kudhihirika. Hapa kuna neno Mkuu.
Kuna uwezekano wa kuwepo na neno, hata hivyo aina nyingine ya udadisi inatia shaka....
Anyway tuendelee kukata ishu, Vipi huo mgao umeshakwisha? manake huku Zenj haukufika!



hii ni aina nyingine ya akili za mtu mwenye ukakasi wa mawazo, kuhoji namna serikali yako inavyotenda ni haki yako ya kikatiba mtanzania mwenzangu, katika mazingira ya dharula kama hivi , NDIO Richmond ilizaliwa, katika mazingira kama haya , tulisign mkataba kituko wa IPTL, DHARULA hizi wajanja hutumia katika kujineemesha ....
Akili yako lazima iwaze hatua moja kwenda mbele, usiamini kila uambiwacho na hasa hawa wanasiasa uchwara, na wezi wa mali ya umma.
Ta'adabu

Mada mama imelenga kwenye hisia na kutaka kujua inachukua siku ngapi kwa meli ya mafuta/mizigo toka Arabuni hadi Bandari ya Dar.

Ili kunitoa huo ukakasi wa mawazo hebu nieleze inachukua muda gani kusafirisha shehena ya mafuta toka Uarabuni. Zaidi sio lazima meli itoke moja kwa moja Uarabuni, Mombasa kuna deport za mafuta ya Uarabuni vilevile.
 
maumivu ya kichwa juaza polepole,unajisikia maumivuuuuuuuu
yaani tanzania yetu hii bwana,,,lakini labda wameamua kutafuta pesa ya kampeni kidogo kidogo kutoka vyanzo mbalimbali kuepuka kushtukiwa wakitumia mtindo wa kapu moja kama la EPA.
 
...Kuna mwingine nasikia aliagiza makontaina 6 ya futi 40 yamejaa generators kwa ajili ya kuuzia wadanganyika..Si kwamba hawa walishajipanga kuwa mgao unaanza kwa hiyo wanataka kutuingiza mjini??
 
Kwenye hili suala la meli kuwahi sio ajabu. Mambo kadhaa yanaweza kuwa yamefanyika mafuta haya yakawahi. Kwanza, International trade ya bulk cargo (mafuta ya magari, mafuta ya kutengeneza sabuni na kula, sukari, ngano, mkaa wa mawe na kadhalika), wauzaji wanaweza kupakia mzigo bila mnunuzi kufahamika. Meli huamua kuelekea ukanda fulani kulingana na mahitaji. Mara nyingi meli hupakia mafuta na kuja ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki, zikakaa hapo kusuburi order. Mnunuzi akipatikana tu, mzigo unakuwa karibu. Ngano inaweza kupakiwa kutoka Canada na kuja ukanda wa Africa mashariki kusubiri Order, Azam wakinunua tu ngano inakuwa karibu kabisa na eneo linalohusika. Haya mafuta ni hayatumiki IPTL pekee, inawezekana yalikwa yanapelekwa sehemu nyingine lakini kutokana na umuhimu TOTAL wakaamua walete kiasi Tanzania baada ya kupewa order na umuhimu wake. Tujue kuwa meli hiyo inabeba mafuta mengi zaidi ya hayo.
Pili, ni speculation za kibishara. Kuwa walitonywa tangu siku ya kwanza ya mgao wa umeme kuwa IPTL itawashwa hivyo wakasogeza mzigo karibu.
 
Mkuu Nguvumali, swali lako ni zuri sana hata mimi hili nililitafakari kwamba inakuwaje hata siku 10 hazijapita tangu Kikwete aiamrishe IPTL kuwasha mtambo wake tunaambiwa mafuta yaliyoagizwa na Serikali yameshaingia nchini. Hapa naona kuna neno na si ajabu kuna ufisadi wa hali ya juu. Maana hili tatizo la umeme nchini linatumiwa na wengi sasa kujitajirisha kwa kuifisadi nchi yetu. Si ajabu mafuta hayo itadaiwa yamenunuliwa kwa bei mbaya na pia kuna uwezekano yalikuwepo nchini siku nyingi sasa wameamua kutumwagia changa la macho ili kuonyesha kama yameagizwa toka nje.
Mkuu, inabidi tuelewe kuwa suala hili halikuanza kushughulikiwa siku ambayo agiza la Kikwete liliskika publicly. Mpaka siku il nchi ilikuwa kwenye mgawo kama wiki mbili hivi na wahusika walikuwa wameshaanza kulishughulikia suala hilo hata kabla mgawo haujaanza. Agizo la Kikwete kwa akina Ngeleja lilitolewa siku ambapo walipeleka taarifa Ikulu kuwa kutakuwa na mgawo wa umeme, na hili lilifanyika hata kabla mgawo haujaanza. Hivyo suala hili lilianza kushughulikiwa zamani isipokuwa tu haiukuelezwa hadharani ni nini kilikuwa kinafanyika.
Naona wakati wanatangaza walifanya kosa jingine kuwa hawakueleza kuwa suala hilo liliashaanza kushughulikiwa siku nyingi, hilo linatufanya wananchi wengi tulio nje tukadhani kuwa serikali ilianza kushughulika pale agizo la Kikwete lilipotolewa publicly
 
Kuna uwezekano wa kuwepo na neno, hata hivyo aina nyingine ya udadisi inatia shaka....
Anyway tuendelee kukata ishu, Vipi huo mgao umeshakwisha? manake huku Zenj haukufika!

.
Hata hakieleweki ndugu yangu,Kila mara namwona ngeleja kwenye Tv akitangaza tarehe tofauti tofauti za kuisha mgawo.Mara aseme mwisho wa Novemba tunatesti mashine, mara kesho,mara mwisho wa mwezi huu.
Makali ya mgawo ndio kwanza yapo palepale ukizingatia na ratiba zenyewe zipo zigzag,pengine na Tanesco nao wamejiundia kaufisadi kao.
mwee kwa kweli Sirikali!
 
Kwenye hili suala la meli kuwahi sio ajabu. Mambo kadhaa yanaweza kuwa yamefanyika mafuta haya yakawahi. Kwanza, International trade ya bulk cargo (mafuta ya magari, mafuta ya kutengeneza sabuni na kula, sukari, ngano, mkaa wa mawe na kadhalika), wauzaji wanaweza kupakia mzigo bila mnunuzi kufahamika. Meli huamua kuelekea ukanda fulani kulingana na mahitaji. Mara nyingi meli hupakia mafuta na kuja ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki, zikakaa hapo kusuburi order. Mnunuzi akipatikana tu, mzigo unakuwa karibu. Ngano inaweza kupakiwa kutoka Canada na kuja ukanda wa Africa mashariki kusubiri Order, Azam wakinunua tu ngano inakuwa karibu kabisa na eneo linalohusika. Haya mafuta ni hayatumiki IPTL pekee, inawezekana yalikwa yanapelekwa sehemu nyingine lakini kutokana na umuhimu TOTAL wakaamua walete kiasi Tanzania baada ya kupewa order na umuhimu wake. Tujue kuwa meli hiyo inabeba mafuta mengi zaidi ya hayo.
Pili, ni speculation za kibishara. Kuwa walitonywa tangu siku ya kwanza ya mgao wa umeme kuwa IPTL itawashwa hivyo wakasogeza mzigo karibu
.

Mkuu Congo unadhani hawa watu hawalijui hilo, wanatafuta hoja za kitoto ilimradi wapate cha kupotezea muda. Hivi kweli mtu na akili zako unaweza kufikiri ati kuna kampuni inayotengeza mafuta kwa ajili ya IPTL tu? au unadhani hawajui huo utaratibu wa cargo za mafuta kuwa karibu na ukanda wa biashara? Binti yangu wa darasa la tatu hata baada ya siku moja rais kuamuru mitambo kuwashwa asingeshangaa kusikia mafuta yanapakuliwa bandarini Dar(labda kwa kuwa tunakaa Kurasini). Hizi ndizo siasa za hapa JF ndio maana kuna wakati full day najivinjari jukwaa la akina masanilo, fidel80, crispin na wale mabinti wengine tunachapa soga za mahusiano kujipumzisha na upupu wa huku aaaaghhrrr
 
Tanzanians should themselves for electing dishonest leaders. Kibaya zaidi, its seems our leaders dont have time to think logically wanapofanya huo ufisadi. Kwangu mimi, I perceive it kama dharau kwa wanannchi
 
Mhh hii ni kali. Kuna kitu hapa.

Tar 21/10/2009 Kikwete alitoa agizo kuwa mitambo ya IPTL iwashwe.

Tar 25/10/2009 tayari meli yenye shehena ya mafuta imewasili Dar kwa ajili ya kutumika kwenye mitambo ya IPTL.


Swali:
Mafuta yaliagizwa lini hadi yawe yameshawasili Dar tarehe 25/10/2009?
hii ina shangaza sana tufanyaje juu ya watu hawa maana kuna ukweli ndani yake Mungu asikie kilio chetu kama alivyo sikia cha wana wa israeli atutumie Musa wa sasa tutoke utumwani laana ilisha sasa inakuwaje
 
wazee hilo wazo duuuh!!, thats why everyday and i l continue to say that tanzania have got a briliant people.
thats our money the find any way writing a document and get that fwedha!!!
we will always fight on jamiiforum
 
Tunawaagiza dr Slaa na Zito Kabwe watutafutie majibu ya swali hili alhamisi hii kesho kutwa moja kwa moja kwa mzee pinda.
 
Mwenzenu ninatatizwa na jambo moja nalo nihili la Umeme na maswala ya Dowans....

Nikifikiri kwa makini na kwakina natatizika, kweli hakuna mkono wa namna namna katika hili swala la kukatika umeme TANZANIA na hujuma ?

Hebu fikiri Rais JK Kikwete (Mheshimiwa) alitoa tangazo kua mitambo ya IPTL iwashwe, kisha tukaambiwa na kina Mh. Ngeleja kuwa Serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL ARABUNI, Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo...na yamefika bandari ya Dar es salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe...

Sasa najiuliza meli toka Arabuni huchukua siku ngapi ? Au mafuta yaliagizwa kabla ya ikulu kuzungumza? Bado najiuliza au tuliishapata dili la IPTL tulichokuwa tunasubiri ni mitambo izimwe nchi iwe kizani ?

Mimi naogopa hapa, na Hisia kua kunakitu nyuma ya sakata zima la umeme Tanzania inanijia...


Ni mawazo yangu.

Inaelekea Zitto aliujua huu mchezo mapema na katika jitihada za pre-emption akashauri serikali itumie mitambo ya Dowans, kama serikali ingekubali bila shaka EL na RA wangefaidika na hivyo kuzidi kuipa nguvu kambi ya mafisadi na kuchochea mgawanyiko zaidi kwa chama chetu na pengine kuwanufaisha wapinzani japo indirectly.

nadhani muungwana akashtukia hiyo na kuamua kutumia IPTL kwa kuwa pengine hana hakika kama EL na RA watamuunga mkono financilally come yr 2010. having said that, inawezekana hii ni dili ya muungwana kutengeneza pesa kwa ajili ya uchaguzi come yr 2010...who knows...si wanasema siasa ni mchezo mchafu...pengine huu ndio katika huo uchafu...

maoni yangu tu...
 
Nafikiri wakati hili linaendelea kujadiliwa( yaani hili la kasi ya ajabu katika uwajibikaji wa serikali ya awamu hii), hebu tuwatafute hawa wafuatao na ku-connect the dots:-

Wamiliki na wanahisa wa IPTL ni wakina nani?
Watu wa serikali walioipigia pande IPTL mpaka wakafanikiwa ni kina nani?
Wakati IPTL inapikwa nani walikuwa; Waziri wa Nishati na Madini
Naibu waziri-Nishati na madini,
Katibu Mkuu- Nishati na madini.
Waziri wa fedha
Katibu mkuu-Hazina na
Mwanasheria mkuu?

Leo hao wahusika wako wapi? Ikiwa kipindi hicho walipewa chochote kitu na IPTL leo watashindwaje kutengeneza mgogoro utakao wapa kula nyingine tena?
 
Kwani kutoka Huko Uarabuni hadi DSM ni umbali gani? au meli huwa inachukua muda gani hadi kufika huku ikitokea uarabuni, Msidhani meli ni baiskeli jamani, siku hizi technolojia imekua si kama zamani waarbu walikuja kwa mashua mkadhani hali ni ileile.
Ulizeni hizo fedha za kununua hayo mafuta zimetoka wapi na misingi ipi. Suala la Meli kuwahi ni nafuu kwetu. ingechukua mwezi kuja hapa ingekuwa kero.
Halafu serikali imeagiza mafuta kupitia kampuni ya Total Tanzania wao wanajua hiyo meli walipoitoa

Hiyo technology ya kufanya meli itoke arabuni hadi dar in 4 days ni ipi? Process zote za kuanzia kuagiza, kununua huko arabuni, kupack, na kuanza safari mpaka dar in 4 days?
Jamani tusidanganyane na technology
 
Nafikiri wakati hili linaendelea kujadiliwa( yaani hili la kasi ya ajabu katika uwajibikaji wa serikali ya awamu hii), hebu tuwatafute hawa wafuatao na ku-connect the dots:-

Wamiliki na wanahisa wa IPTL ni wakina nani?
Watu wa serikali walioipigia pande IPTL mpaka wakafanikiwa ni kina nani?
Wakati IPTL inapikwa nani walikuwa; Waziri wa Nishati na Madini
Naibu waziri-Nishati na madini,
Katibu Mkuu- Nishati na madini.
Waziri wa fedha
Katibu mkuu-Hazina na
Mwanasheria mkuu?

Leo hao wahusika wako wapi? Ikiwa kipindi hicho walipewa chochote kitu na IPTL leo watashindwaje kutengeneza mgogoro utakao wapa kula nyingine tena?

Hapa umenena kweli kabisa, majibu ya maswali haya yakipatikana itasaidia sana kujua ni vipi IPTL ina nguvu nchini.

Binafsi nionavyo hii serikali haiwezi kujitenga na mambo yote yanayo endelea.

Wanajamii wenzangu kuhusu IPTL na mauchafu mengine yote yanayoendelea nchini majibu sahihi hayawezi kupatikana kutoka kwenye hii serikali. Huo ndio ukweli wenyewe.

They are part and parcel of all ufisadis! Period.

Haya tuendelee kujifariji;

Njimba
 
Tumuulize NGELEJA palepale Tegeta kuna mtambo mpya wa TANESCO utakaotumia gesi ambao utatoa MW 20.Umechelewa kuanza kazi kutokana na vifaa KUCHELEWESHWA BANDARINI.JEE KWA NINI SERIKALI HAIKUCHANGAMKIA KUTOA VIFAA VYA MKANDARASI HUYO KAMA ILIVYOCHANGAMKIA MAFUTA?Jee kwenye hii order ya mafuta ilifuata taratibu za manunuzi ya PPRA?KWA NINI SERIKALI HAIFIKIRII KUPATA UFUMBUZI WA KUDUMU mfano RUFIJI BASIN inaweza kutoa MegaWatts za kutosha nchi nzima na ziada.MELI NINA UHAKIKA ILIKUA TAYARI KTK PWANI ZETU, HILI NI DEAL!!?
 
Back
Top Bottom