Mafuta hayakamatiki zanzibar..

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kuna habari kuwa kwasasa mafuta ya petrol na diesel yamekuwa bidhaa adimu sana Visiwani Zanzibar.Bei ya ulanguzi ya nishati hiyo imefikia shilingi elfu sita kwa lita badala ya bei iliyokuwepo ambayo ilikuwa shilingi elfu mbili.Wazanzibar wengi wameamua kutembea kwa miguu na wengine kupaki magari yao.Je,ni dalili ya kushindwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko? Je,tatizo hilo nalo ni la kimuungano?

Tujadili...
 
Nadhani tatizo ni la kimuungano kwani lilianza huku kwetu kwa mara nyingi sana
 
Nipo sheli ya mwanakwerekwe sokoni, haap zaidi ya maagri 100 yamepanga foleni tangu juz. kwa ufupi watu wanakesha sheli, mafuta hakuna kabisa ktk sheli zote hapa. bei ya ulanguzi ni 5000 hadi 6000.
bei ya mafuta imefikia hadi 5000.
huko bara mafuta yanatafuta wateja. Jee EWURA inaihujumu zanzibar
 
Unazungumzia bara ya wapi? EWURA imekuwa ni tatizo kote kote.
 
Hapo tatizo ni Wafanyabiashara mkuu EWURA ingeingia kama sheli ingeuza mafuta kwa bei ya juu.
 
Wakitaka waondokane na hili, lazima wavunje muungano. Muungano huu unaongalia maslahi ya viongozi badala ya wananchi ndiyo unaleta shida zote hizi.
 
Nyie wazenj, mafuta ya kuagiza nchi za nje mnasema ni suala la Muungano lakini mafuta ya kuchimba sio ya muungano!! Eboo nyie vipi mnataka kula visheti vyenu halafu mnataka mbaki navyo?
 
nyie si mnajiita nchi,na mnasema mafuta mnayo na si swala muungano,
chimbeni hayo mjiuzie wenyewe kwa bei chee.
 
kwani zanzibar kuna magari? mimi nilifikiri kuna baiskeli na mitumbwi tu...!
we mtu wa aina gani jamaa hata nje ya Tanganyika hujawahi kufika...unaenda kama boya tu:poa

images

Mandhari na harakati za kila siku katika eneo hili la Darajani Mjini Zanzibar, kama linavyoonekana pichani wakati wa kazi asubuhi ndivyo linavyokuwa na pirika pirika za hapa na pale na msongamano wa magari na watu wakiwa katika shufghuli zao.
 
....Jee EWURA inaihujumu zanzibar
EWURA?

Nyinyi mlisema mmeondoa mafuta katika orodha ya mambo ya Muungano, sio? Sasa bado mnategemea EWURA?

Ina maana siku mlipotangaza mnajiondoa kwenye muungano wa mafuta hamkuanzisha EWURA yenu? Hahahahahahaaa....

Nendeni Dodoma mkatangaze mnataka kufanya kila kitu kivyenu. Kila kitu!
 
Nyie wazenj, mafuta ya kuagiza nchi za nje mnasema ni suala la Muungano lakini mafuta ya kuchimba sio ya muungano!! Eboo nyie vipi mnataka kula visheti vyenu halafu mnataka mbaki navyo?

Recipient not found
-delivery error
 
Back
Top Bottom