Mafuriko:Vodacom waanza kampeni ya simu; kuchangia Vod. Foundation

Watu wamechukizwa sana na kitendo hiki kwa kuona kuwa Vodacom inajaribu kwa kutumia nguvu yake kusabotage juhudi za kuchangia Red Cross Society ya Tanzania. Tumeona watu wakijiunga kwenye kampeni yetu kwa sababu sasa wanaalewa. By the way, mafuriko mengine kongwa yamesababisha watu zaidi 300 kukosa malazi. Guess what? Wanasubiri Chama cha Msalaba Mwekundu kuwasaidia...
 
hawa jamaa ni wezi watupu, hakuna lolote wanalofanya wanajitangaza tu ili walalahoi wajue wanawajali, ni kwanini msitumie part ya faida yenu mnayopata kusaidia hao wahanga badala ya kendelea kuwakamua wananchi??????
 
Hebu tuangalia kwa sekunde chache...
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kijamii wa Vodacom Foundation, umetoa msaada wa Milioni 20 ili kuboresha mahitimu ya wananchi waliopatwa na madhara ya kulipukiwa na mabomu Mbagala jijini- Mwandishi Wetu

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia Mfuko wa Jamii, Vodacom Foundation, imekabidhi msaada wa madarasa matatu yenye thamani ya Sh milioni 24 kwa sekondari ya Masquaroda, Hanang, Manyara. Msaada huo ulikabidhiwa jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Geofrey Ngatuni na Mkuu wa Mfuko huo, Mwamvita Makamba, kwa niaba ya uongozi wa shule hiyo. - Habari Leo, Machi 5, 2009
Kampuni ya simu za mkononi ya VODACOM imetoa msaada wa chakula kwa watoto yatima, wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 65 ambao utagawiwa kwa vituo 30 vya kutunza watoto yatima na wasiojiweza hapa nchini, katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya. - Radio One Habari, 16 Disemba, 2008

Hiyo ni mifano michache tu ya jinsi Vodacom imekuwa ikitoa misaada mbalimbali. Hata hivyo hii ni mara ya kwanza (kwa kumbukumbu yangu) kwa Vodacom ambayo imekuwa ikidai kuwa inatoa misaada hiyo kama sehemu ya "social responsibility" ya kampuni kuanza kukusanya fedha kutoka kwa wananchi halafu kuzirudisha tena kama sehemu ya misaada!

Kwa maneno mengine, kwa kufanya hivyo Vodacom haitagusa faida yake au fedha zake yenyewe kusaidia majanga haya au ya huko mbeleni na badala yake itatumia mtandao wake wa simu kukusanya fedha na baadaye kuzirudisha kama sehemu ya msaada. Unless pia wasema kuwa wanamatch shilingi kwa shilingi ya michango inayotolewa hapo watakuwa kwa kiasi fulani wamenivuta nikubali..
 
Leo ni siku ya pili lakini magazeti ya tz bado hawajaandika hii day light robbery, jamani waandishi mnafanya nini au mpaka mpewe bahasha ndio mtaandika

labda tusubiri vodacom watatoa tamko lao kuhusiana na hili
 
Ndugu zangu hata hivyo vodacom foundation imekwepo kwa kipindi kirefu kwahiyo wanachokifanya sio cha kushangaa ni vizuri na jf nayo kushirikiana na tpn kuanzisha foundation yao kwa ajili ya kupeleka huduma hizi kwa jamii
 
kwani kuna mtu kabisha juu ya historia ya uwepo wa vodacom foundation? Kwa vile inaonekana unawajua sana, unaweza kutusaidia kukumbuka mara ya mwisho kwa Vodacom kuchangisha watu ili kusaidia Vodacom Foundation kutoa misaada ilikuwa ni lini?
 
Kwenye sikukuu za xmass walichangia vituo mbalimbali vya watoto yatima na kwenye sikukuu nyingi sana huwa wanachangia kutokana na hiyo foundation yao , pia kuna michango mengine sio lazima itangzwe kupitia vyombo vya habari kama wewe unavyotaka iwe - naamini vodacom wanatumia haki na wajibu wao kwa jamii kwasababu hiyo foundation ilikwepo toka kitambo mfano mwanakijiji nikuulize mtu akija kuibuka kusema Uliyoanzisha wewe ni SCAM utaweza kubisha ? unachangisha pesa wewe kama nani ? Kisheria
 
Vodacom Foundation.. ilianza lini kuchangisha (siyo kuchangia); yaani, kuomba watu waichangie ili itoe misaada, mara ya mwisho ilifanya hivyo lini? Foundations karibu zote duniani zinatoa misaada kutoka katika vyanvyo vyao wenyewe siyo kutoka kwenye kuchangisha wananchi walioathirika ili foundation itoe misaada.
 
hebu tuangalia kwa sekunde chache...

Hiyo ni mifano michache tu ya jinsi vodacom imekuwa ikitoa misaada mbalimbali. Hata hivyo hii ni mara ya kwanza (kwa kumbukumbu yangu) kwa vodacom ambayo imekuwa ikidai kuwa inatoa misaada hiyo kama sehemu ya "social responsibility" ya kampuni kuanza kukusanya fedha kutoka kwa wananchi halafu kuzirudisha tena kama sehemu ya misaada!

Kwa maneno mengine, kwa kufanya hivyo vodacom haitagusa faida yake au fedha zake yenyewe kusaidia majanga haya au ya huko mbeleni na badala yake itatumia mtandao wake wa simu kukusanya fedha na baadaye kuzirudisha kama sehemu ya msaada. Unless pia wasema kuwa wanamatch shilingi kwa shilingi ya michango inayotolewa hapo watakuwa kwa kiasi fulani wamenivuta nikubali..

kwa trend hii muda si mrefu tutasikia barrick na geita pia wanahitaji michango kusaidia kumalizia shule walizokuwa wakizijenga...............
 
mfano mwanakijiji nikuulize mtu akija kuibuka kusema Uliyoanzisha wewe ni SCAM utaweza kubisha ? unachangisha pesa wewe kama nani ? Kisheria

huyo mtu si aibuke na kujaribu na kusema ni scam.. halafu utaona nitakachosema.
 
Angalia scam zote duniani zinavyoendeshwa na jinsi hali hii ilivyo sasa au kuna mkataba wa siri kati ya TPN na JF uliowekwa ambao sisi wanachama hatujui ambao unaelezea kidogo kuhusu juhudi hizi za kuchangia waathirika wa mafuriko ? Jamani tusiongelee vitu juu juu tu haya mambo ukianza kuhoji na kufuatilia watu watakimbiana humu
 
wewe wasiwasi wako. Vodacom mara ya mwisho waliomba kuchangiwa lini ili kutoa misaada yao? Mara zote wamekuwa wakitoa misaada kwa watu mbalimbali pasipo kupitisha kikombe cha kusaidiwa kwanini leo wanataka wachangiwe?
 
Watu wamechukizwa sana na kitendo hiki kwa kuona kuwa Vodacom inajaribu kwa kutumia nguvu yake kusabotage juhudi za kuchangia Red Cross Society ya Tanzania. Tumeona watu wakijiunga kwenye kampeni yetu kwa sababu sasa wanaalewa. By the way, mafuriko mengine kongwa yamesababisha watu zaidi 300 kukosa malazi. Guess what? Wanasubiri Chama cha Msalaba Mwekundu kuwasaidia...

Na kuna mengine yametokea kule Idodi mkoani Iringa. Mtu wa kwanza kumsikia amekimbilia kule ni William Lukuvi ambaye ni mbunge wa kule, na msaada pekee ambao umeshatolewa mpaka sasa kwa maelezo yake yeye wenyewe ni sh milioni 2.5, na umetolewa na yeye mwenyewe. Na si kwamba ameutoa kwa ngazi husika za serikali kama ofisi ya waziri mkuu, au mkoa au wilaya au hata kijiji, au hata mashirika yanayojihusisha na matatizo kama haya, amepeleka hizo 2.5m kuwagawia wananchi mmoja mmoja waliokumbwa na mafuriko. Kwanini amekimbia kule wa kwanza, kwanini amewagawia pesa yeye mwenyewe, kwanini serikali haijasikika hata ikisema tu kuna mafuriko, majibu mnayo wenyewe.

Mimi bado nauliza, Ikwapi serikali kwenye yote haya?
 
kwa trend hii muda si mrefu tutasikia barrick na geita pia wanahitaji michango kusaidia kumalizia shule walizokuwa wakizijenga...............

nyie subirini tu; wakishajua kuwa wanaweza kupata faida kwa namna hii wala hawatasita. Vodacom wameingia kwenye mtego mbaya sana. Natamani nizungumze nao na niwaambie wamekosea wapi.
 
Mimi bado nauliza, Ikwapi serikali kwenye yote haya?

utasubiri hadi kiyama; hakuna serikali duniani ambayo ina rekodi nzuri ya kushughulika na majanga, hakuna. Ndio maana tunatumia taasisi za misaada ya kibinadamu kwa sababu zinaongozwa na vitu tofauti na maadili tofauti. Unafikiri kama Haiti wangekuwa wanasubiri hadi serikali ya Marekani ilete meli zake na misaada yake unadhani chakula kingefika lini? kama siyo Red Cross, Unicef na UN ambazo zilifika mapema pale.

Believe me.. when disaster strike don't count on the government.. waulize New Orleans!
 
Kweli lakini hayo mashirika ya misaada hivi karibuni imegundulika na zenyewe na balaa katika matumizi mabaya za fedha za wachangiaje..duniani wenye imani wamepungua kuja haja ya kuweka sheria yenye adhabu kali kwa wezi wa pesa za msaada

taarifa zao zingine zinasikitisha
 
utasubiri hadi kiyama; hakuna serikali duniani ambayo ina rekodi nzuri ya kushughulika na majanga, hakuna. Ndio maana tunatumia taasisi za misaada ya kibinadamu kwa sababu zinaongozwa na vitu tofauti na maadili tofauti. Unafikiri kama Haiti wangekuwa wanasubiri hadi serikali ya Marekani ilete meli zake na misaada yake unadhani chakula kingefika lini? kama siyo Red Cross, Unicef na UN ambazo zilifika mapema pale.

Believe me.. when disaster strike don't count on the government.. waulize New Orleans!

Na hayo madawati yanayotolewa na vodacom foundation pia ni disaster au pia wanafunzi nao watasubiri serikali hadi kiyama
 
Na hayo madawati yanayotolewa na vodacom foundation pia ni disaster au pia wanafunzi nao watasubiri serikali hadi kiyama

unaelewa maana ya neno Disaster? mimi si mshabiki wa misaada ya kijinga. Lakini ni muamini wa utu wa mtu na kwamba utu wa mwanadamu haupunguki kwa sababu serikali yake ni ya kifisadi. Nikiona mtu ana njaa nitampa chakula kwanza kabla ya kumlaumu kwanini ana njaa! Nikimuona watu wameangukiwa na nyumba nitakimbia kuokoa kwanza kabla ya kuuliza kama walifuata kanuni za ujenzi bora!

Ninapoona mafuriko na majanga yanayokuna nayo nitakuwa mstari wa mbele kusaidia badala ya kuuliza "serikali iko wapi".
 
Hawa VODACOM ni wezi kupita maelezo! wao ndio wamegoma kushusha viwango vyo simu baina ya mitandao ya simu kwa kushirikiana na TCRA! Uliona wapi simu unayopiga humuhumu ndani ya nchi garama zikwa tofauti? wanatambakuwa wa wateja millioni sita , hebu kwa mahesabu rahisi kwamba kila mteja anatumia Efu tano kwa mwezi . Hii nisawa na pato la 30,000,000, 000,000.Je hii ndio wanayodeclare TRA? na VAT (18%) yake ambayo ni %,400,000,000/- wanaremit TRA?
Kwanini hiyo wanayowakamua Watanzania wasoine aibu angalau wakatoa hata 10% kusaidia waathirika kuliko kutukamua tena na wakati hata udhibiti wa hiyo michango haueleweki!
 
Kuna tatizo gani Vodacom kuanzisha michango kama hii? Nilitarajia tungehamasisha na akina Zain, Tigo, Zantel, Sasatel, TTCL nao waige mfano huu. Muhimu ni kujua wataiwakilisha wapi michango hii ili iwafikie walengwa. Haiti imechangiwa na wasanii, wanamichezo maarufu, taasisi za kidini, mfuko wa marais wastaafu Bill Clinton na George HW Bush,......Au ni kwa kuwa kuna RA na EL mle?
 
Back
Top Bottom