Mafuriko Dar, mvua kali ikiambatana na radi yanyesha, umeme wakatwa

CPA unareport kana kwamba umeyaona mafuriko.
Ni kweli inakamua lakini bagamoyo rozd kupo shwari mpaka muda huu.

Watu huchelewa mvua ikinyesha ili kukamilisha majukumu ya chumbani....

Mkuu unanichungulia nn? Maana mpaka zoezi halijaisha.
 
old bagamoyo road darajani JKT hapapitiki daraja limeharibiwa
maji ya mto mbezi yanapita juu ya daraja ni hatari kweli!
 
Walioko maeneo husika, mtusaidie picha tuweze kuweka kumbukumbu wakuu kwa siku zijazo. Hii itasaidia kuepukana na majanga wakti mwingine!
 
kwanini maeneo hayo yote yamejaa maji hivyo?

Nikiweka kando siasa, naongea kutoka upande wa utaalamu.

1. Miundombinu (barabara, mifereji, bomba za maji safi na majitaka, nguzo na transfoma za umeme ) katikati ya jiji la Dar haijabadilishwa tangu miaka ya 1990 ili kuendana na wingi wa watu na majengo, ilhali idadi ya watu na majengo vimeongezeka sana kuliko uwezo wa miundombinu hiyo.
2. Wingi wa majitaka kutoka katika mapaa ya majengo, ukichanganya na majitaka kutoka katika majengo hayo, haviwezi kupita kirahisi katika miundombinu ya majitaka iliyopo, hivyo sehemu kubwa ya maji haya hupita juu ya barabara (kv. barabara ya pamba, Nnamdi Azikiwe, Ohio na A.H. Mwinyi), ndio sababu hata harufu za kinyesi haziishi mjini, mfano mzuri pale Haidery Plaza, chemba za majitaka zinafurika kila siku, na hakuna anayejali pamoja na kwamba tunalipa kido kwa ajili hiyo.
3. Baadhi ya majengo ya maeneo mengi ya jiji, yamezuia mapitio asili ya maji ya mvua, hivyo kubadili mikondo ya maji hayo na/au kutuamisha maji kabisa na kusababisha kero. Mfano ni pale Quality Plaza/Kiuta (wameparekebisha hivi juzi baada ya kelele zetu walipa kodi).
4. Ushauri wa kitaalamu kuhusu kuboresha miundombinu ya jiji letu hautiliwi maanani na wenye mamlaka, badala yake siasa zinapewa kipaumbele. Vinginevyo, katika nchi nyingine, hakuna mtu mwenye akili zake timamu angekubali ujenzi wa majengo ya ghorofa zaidi ya 20 katikati ya jiji la Dar ilhali maegesho hakuna, miundombinu ya maji safi na taka haitoshi na umeme hautisho kutokana na transfoma kuzidiwa kutokana na wngi wa majengo makubwa.
Wataalamu wengine wajazie penye mapengo.
 
Unajua hii mvua imewasaprise watu,kwani wengi walikua wamelala na kilichowashtua usingizini ni radi zilizokua zinapiga utadhani zilikua kwenye mashindano.Maeneo mengi ya makoka na kibangu maji yameingia ndani na mpaka muda huu watu wanaendelea na zoezi la kutoa maji na kufanya usafi kwenye nyumba zao.Wasiwasi wangu ni kwa watu wanaotokea maeneo ya Tandale kwa Mtogole sijui hali iko vipi huko.
 
Lakini afadhali mvua imenyesha ipunguze joto...labda vikwapa navyo vitatulia.
,........Hili nalo neno, binafsi mimi si muhanga wa hizi mvuwa za leo kwani wakati wa kujenga nyumba nilikuwa najuwa nyumba inastahili ijengwe kwenye mazingira gani.
 
Njia ya kuelekea Msewe kutokea Kibo (barabara ya Morogoro) imefungwa kutokanana na uharibifu wa daraja. Sehemu ya ukuta wa shule ya Ubungo Msewe umebolewa na mvua.
 
,........Hili nalo neno, binafsi mimi si muhanga wa hizi mvuwa za leo kwani wakati wa kujenga nyumba nilikuwa najuwa nyumba inastahili ijengwe kwenye mazingira gani.

Ina maana hujapata adha ya aina yoyote kutokana na mvua ya leo? Umepita angani ama unatumia barabara kama sisi?
 
Hii mvua ni balaa! Nawaonea huruma waliopo mabondeni.
...nadhani magomeni ni moja kati ya maeneo yalioathirika sana na hii mvua. Nimepita katika bonde la kinondoni mkwajuni kuelekea magomeni (moroco hotel) nimekuta polisi kutoka kituo chamagomeni wakijaribu kuwaokoa wahanga wa hii mvua. Inasemekana kun nyumba kadhaa zimefunikwa na maji na idadi kubwa ya watu hasa watoto wamepotea au hawajulikano walipo na wale wengine wanajitahidi kujiokoa kwa kutumia mabeseni ya plastiki.....Wakati mwingine hawa watanzania wenzetu wapunguze ubishi wewe unaambiwa usijenge makazi bondeni unang'ang'ani tu....leo itakula kwenu aisee.:yawn:
 
Nasikia mvua kubwa imenyesha Dsm na imesababisha mafuriko maeneo mengi ya Dsm .aliy karibu atajuze yanayo jiri
 
Nasikia mvua kubwa imenyesha Dsm na imesababisha mafuriko maeneo mengi ya Dsm .aliy karibu atajuze yanayo jiri
Nipo Dar, hakuna mvua yoyote iliyonyesha hivi karibuni. Hakuna mafuriko, jua linawaka na kuna vumbi jingi tu hasa maeneo ya Tabata Relini na Kigogo. Wewe umesikia kwa nani?
 
Kweli kabisa Mvua kali imenyesha jana Usiku kucha ikiwa imeambatana na Radi, kama kawaida wale Waishio Maeneo ya Mabondeni wamepata Maafa.
 
Nipo Dar, hakuna mvua yoyote iliyonyesha hivi karibuni. Hakuna mafuriko, jua linawaka na kuna vumbi jingi tu hasa maeneo ya Tabata Relini na Kigogo. Wewe umesikia kwa nani?

unaweza kutumia busara na kubadilisha hiyo avator yako? weka hata ya Nape au mbatia
 
Back
Top Bottom