Mafuriko Dar, mvua kali ikiambatana na radi yanyesha, umeme wakatwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CPA, Dec 20, 2011.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 18
  Mvua kubwa ikiambatana na radi kali inayoendelea kunyesha usiku huu, imezua kizaa jijin dar es salaam. Kila sehemu ni mafuriko, barabaran magar hayaendeki, hizi barabara zetu za uswahili wala usidhubutu kupitisha gar lako, cjui wenzangu wa tandale na magomen wamelalaje? Radi ni kali mpaka umeme umekatika. Hali ya usafiri utakuwa wa taabu sana. Ikinyesha hiv cku 2, itakuwa kama indonesia
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,568
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38
  haya matatizo tunayataka wenyewe.......ufumbuzi wa swala la mafuriko liko wazi kabisa.........
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 43,970
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa linalosababisha mafuriko Dar ni hii Serikali taahira ambayo pamoja na kuliona tatizo hili kila mwaka lakini hadi hii leo haijachukua hatua yoyote ile muhimu kuhakikisha Jiji linatengewa fungu kubwa la pesa ili kujenga drainage system ambayo itaweza kuhimili ongezeko kubwa la wakazi wa jiji na pia kuzuia kabisa mafuriko kama haya yanayosababishwa na mvua kubwa hata za muda mfupi tu.

  Juzi tu wametumia Shilingi bilioni 64 "kusherehekea" miaka 50 ya uhuru. Imagine pesa kama hizi zingeamuliwa kutumika katika kujenga drainage system ya nguvu ili kuondoa kabisa tatizo la mafuriko katika jiji la Dar....Kupanga ni kuchagua...hii ndiyo ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya iliyoahidiwa na msanii.
   
 4. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 933
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hizi radi za leo si za kitoto.kwa wanaotumia mbavu za mbwa nadhani hali ilikuwa mbaya zaidi.nawapa pole wote walioathirika.
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38
  Bilioni 64 ni wizara moja tu. Watu walio ndani ya system wanasema matumizi ya nchi nzima yanafikia Tsh Trilioni 1
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 6,280
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Hii mvua ni balaa! Nawaonea huruma waliopo mabondeni.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu JF Platinum Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 55,812
  Likes Received: 961
  Trophy Points: 113
  Bongo Nyu Yoki!
   
 8. bombah987

  bombah987 JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na wale wanaoishi pale jangwani cjui itakuwaje?
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 43,970
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 0
  ....Na pia wamekwiba pesa nyingi sana katika hiyo Trilioni moja.
   
 10. amakrey

  amakrey Senior Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 8
  huku mbagala hali ni tete,mpaka ifke saa nadhani tutakuwa kwa kisiwa chetu kama kawaida
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 25,936
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 83
  sijui kama nitafika kwenye mihangaiko leo! foleni ya kutisha daladala haziendi! Mfukoni nina buku 2 tu!
   
 12. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,273
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 38
  CPA unareport kana kwamba umeyaona mafuriko.
  Ni kweli inakamua lakini bagamoyo rozd kupo shwari mpaka muda huu.

  Watu huchelewa mvua ikinyesha ili kukamilisha majukumu ya chumbani....
   
 13. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,176
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38
  nimeipita hiyo barabara na maeneo mengi maji yamejaa!! Wenye gari ndogo wanapata sana tabu
   
 14. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,273
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 38
  Rejao wapi kulikojaa maji bmoyo/ali mwinyi road?, mie nimepita na kivitz changu....
   
 15. f

  fungamesa JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Leo kama Indonesia tutafute mitumbwi
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,184
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 38
  mvua hii balaa. Hapa reli mwananchi pamegeuka bwawa. Attachment haziappload la sivyo ningewarushia mapicha
   
 17. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,176
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38
  Mi nilipita asubuhi mvua ikiwa inanyesha! Kuna gari ndogo mbili zimezima kwenye dimbwi kabla ya Salenda, hapa baada ya palm beach kabla ya Joly/Las vegas nako maji yalikuwa yamejaa....nimesogea Red Cross nako kulikuwa full maji! Kuingia Ohio maeneo ya wizara ya mambo ya ndani nako kulikuwa kumejaa maji!
   
 18. N

  Nyadunga Senior Member

  #18
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 6
  Ya Dar yanakera sana. Hata huku DOM nusu jangwa mvua ikinyesha tu kubwa mafuriko. Vp Tanz tumejiandaa vip na disaster? Je kuna kile kiitwacho disaster preparedness? Ya dar hadi ikulu ipitiwe na kimbunga ndo watashtuka! Nawakilisha
   
 19. Maranzana

  Maranzana JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  Old Bagamoyo road pale maeneo ya TMJ Hospital kama kawaida yake ni balaa tupu
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji JF Platinum Member

  #20
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,246
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 83
  kwanini maeneo hayo yote yamejaa maji hivyo?
   
 21. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #21
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 834
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kikwete kama chura hupenda sana hali hii.
   
 22. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #22
  Dec 20, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu unanichungulia nn? Maana mpaka zoezi halijaisha.
   
 23. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #23
  Dec 20, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa nn viunga vya lkulu maji hayajai?
   
 24. amakrey

  amakrey Senior Member

  #24
  Dec 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 8
  Napita sasa hapa pia,TIOT raia wanashangaa vyombo ktk daraja dogo lililojaa na mwananchi ni mafuriko jamani,
   
 25. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #25
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 23,730
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 63
  Tumethubutu,tumeweza na tunasonga mbele
   
 26. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #26
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,815
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  old bagamoyo road darajani JKT hapapitiki daraja limeharibiwa
  maji ya mto mbezi yanapita juu ya daraja ni hatari kweli!
   
 27. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #27
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 15,405
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 38
  Tutakaa hivyo hivyo.
   
 28. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #28
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,724
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Walioko maeneo husika, mtusaidie picha tuweze kuweka kumbukumbu wakuu kwa siku zijazo. Hii itasaidia kuepukana na majanga wakti mwingine!
   
 29. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #29
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 7,681
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 48
  Nikiweka kando siasa, naongea kutoka upande wa utaalamu.

  1. Miundombinu (barabara, mifereji, bomba za maji safi na majitaka, nguzo na transfoma za umeme ) katikati ya jiji la Dar haijabadilishwa tangu miaka ya 1990 ili kuendana na wingi wa watu na majengo, ilhali idadi ya watu na majengo vimeongezeka sana kuliko uwezo wa miundombinu hiyo.
  2. Wingi wa majitaka kutoka katika mapaa ya majengo, ukichanganya na majitaka kutoka katika majengo hayo, haviwezi kupita kirahisi katika miundombinu ya majitaka iliyopo, hivyo sehemu kubwa ya maji haya hupita juu ya barabara (kv. barabara ya pamba, Nnamdi Azikiwe, Ohio na A.H. Mwinyi), ndio sababu hata harufu za kinyesi haziishi mjini, mfano mzuri pale Haidery Plaza, chemba za majitaka zinafurika kila siku, na hakuna anayejali pamoja na kwamba tunalipa kido kwa ajili hiyo.
  3. Baadhi ya majengo ya maeneo mengi ya jiji, yamezuia mapitio asili ya maji ya mvua, hivyo kubadili mikondo ya maji hayo na/au kutuamisha maji kabisa na kusababisha kero. Mfano ni pale Quality Plaza/Kiuta (wameparekebisha hivi juzi baada ya kelele zetu walipa kodi).
  4. Ushauri wa kitaalamu kuhusu kuboresha miundombinu ya jiji letu hautiliwi maanani na wenye mamlaka, badala yake siasa zinapewa kipaumbele. Vinginevyo, katika nchi nyingine, hakuna mtu mwenye akili zake timamu angekubali ujenzi wa majengo ya ghorofa zaidi ya 20 katikati ya jiji la Dar ilhali maegesho hakuna, miundombinu ya maji safi na taka haitoshi na umeme hautisho kutokana na transfoma kuzidiwa kutokana na wngi wa majengo makubwa.
  Wataalamu wengine wajazie penye mapengo.
   
 30. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #30
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 27,733
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 63
  ............Ni kazi ya mungu, haiepukiki!!
   

Share This Page