Mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2016

Kwa taarifa nilizopata wamepiga simu kwa wale walotuma maombi ili kuuliza utayari wao wa kujiunga katika jeshi coz ni muda mrefu umepita toka maombi yatumwe so walitaka kujua kama bado wanania ya kujiunga na jeshi.

Hawajatoa utaratibu wowote wa usahili wala mafunzo,walichodai ni kuendelea kuwasiliana na wahusika kulingana na muongozo utakavokua.
Kuna mtu kapigiwa inatakiwa kwenda jakata wote....... Wanauliza wapate orodha kamili ya fomu za Jakata
 
Sasa mtu kama mimi nipo chuo sasa ivi namaliza mwezi wa saba shahada na nina mpango niunge jeshi baada ya chuo, lakini tayari nilipita JKT kwa mujibu wa sheria (namaanisha huu utaratibu uliorudishwa wa kumaliza form six unaenda jkt miezi mitatu ), inamaana sisi jeshini hatuendi au kuna utaratibu mwingine? Tafadhali mwenye fununu kuhusu hili msaada....
hapo ni sawa na kumaanisha kua "Asiwe service man au service girl"
wewe ni service tayari kwahiyo hauna vigezo ..wewe ni direct TPDF
 
Kuna mtu kapigiwa inatakiwa kwenda jakata wote....... Wanauliza wapate orodha kamili ya fomu za Jakata
Mbona wale ma Dr hawakupiga jakata?sema walipiga fresher pale Ruvu Na gwanda za jwtz baadae wakaenda zao TMA.Hii ya Jakata huyo jamaa kaambiwa kweli au anahisi?
 
Mbona wale ma Dr hawakupiga jakata?sema walipiga fresher pale Ruvu Na gwanda za jwtz baadae wakaenda zao TMA.Hii ya Jakata huyo jamaa kaambiwa kweli au anahisi?
Hao ni madokta kwa kiwango cha degree kwa kawaida walikuwa wanakwenda moja kwa moja siku hizi hakuna wanataka askari sio atoke mtaani aende TMA
 
hakuna tetesi zozote kwa waliopo oljoro au wanatarajia kupiga kozi kihangaiko?
***** poleni kwa watakao enda kupiga kozi oljoro 833kj asee ile kambi ina mawe babaa!!alafu kuna shamba linaitwa embakasy na dunia dadeki acha kabisa yaani!!nikikumbuka hua ndo istoria yangu mamaee!!
 
basi ukiona hivyo mambo yashanukia mwezi huu au ujao watu wataanza kozi.
Asee kuhusu kozi bado ndhani hadi mwezi wa 2 au 3 kumbuka ukishaenda kuripoti kuna miezi 2au 3 ya uzalendo mwendo wa kubeba kifusi na kumwagilia
Hapo kwenye kumwagilia nakumbuka mimi nilikuwa napenda kitengo cha chura
Kama hujaelewa chira inamaana gani kijeshi usinilize ukija utakuja kujua hilo neno lina maana gani
 
Kozi TMA zinaweza kuanza mwez wa 3 kwaiyo professional watakaingia jakata sa hivi wanaweza kuingia TMA mwez huo
 
Kozi TMA zinaweza kuanza mwez wa 3 kwaiyo professional watakaingia jakata sa hivi wanaweza kuingia TMA mwez huo
Yah inawezekana pia,ila sema mambo ya jeshi hayana formula kabisa anythn can happen at any time.So wazalendo muwe tu flexible kwa lolote.
 
Mbona wale ma Dr hawakupiga jakata?sema walipiga fresher pale Ruvu Na gwanda za jwtz baadae wakaenda zao TMA.Hii ya Jakata huyo jamaa kaambiwa kweli au anahisi?
Waliomaliza fresher juzi kati wameambiwa wasubiri paka mwez wa 3 ili wajiunge na professional wengine pale TMA
 
Back
Top Bottom